Kigamboni hakuna Vituo vya Daladala vyenye kivuli, watusogezee na stendi ya magari ya mikoani pia

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Nilihamia Kigamboni miaka ya hivi karibuni, moja ya kitu ambacho kilikuwa kinanipa uwoga kuhamia pande hizi kwanza ni kuvuka maji na pili niliona kama kumekaa kushoto sana.

Nashukuru Mungu uwoga wangu wa maji umepungua labda yawezekana kwa kuwa navuka sana baada ya kuhamia huku.

Hilo la pili kuwa kumekaa kushoto nafikiri ni kwa kuwa nilikuwa sijapazoea huku.

Sasa kero yangu mimi ni kuhusu vituo vya daladala, mji unazidi kukua watu wanaongezeka na hata magari nayo yanaongezeka lakini hakuna vituo vya Daladala.

Mvua zikinyesha ni balaa, matope kila mahali na hakuna anayejali, kwa ufupi ni kama hakuna viongozi ngazi ya Wilaya.

Kingine ni kuwa licha ya kero hiyo, nauli zinapanda kiholela bila kujali na wanaopandisha ni wapigadebe wale wa pale Kivukoni.

Suala la pili ni maoni, Kigamboni kuwe na Stand ya mabasi ya mikoani, tunapata shida, mtu haijulikani unatoka saa ngapi ufike Kivukoni, uvuke hadi uje ufike Mbezi unakuwa umeteseka sana tena sana.

Viongozi wao hata hawajali hili kwa kuwa hilo haliwahusu moja kwa moja.

Kuna mambo mengi hayapo sawa, viongozi wa Wilaya ya Kigamboni wamelala, hawajali chochote.
 
Mbona basi la Kilimanjaro linaanzia na kuishia Kigamboni. Mbona stendi zote Dar hazina mapaa ya abiria kujikinga na jua na mvua, hata Msanvu Morogoro ni kama uwanja wa mpira, ukitaka kukaa nunua gazeti ukalie.
 
Back
Top Bottom