Mgomo wa Daladala Kigamboni

hakuna cha enzi yoyote, haya yote ni madhara ya utawala wa CCM kutawala kwa aina ile ile miaka nenda rudi - Kwa mfano Halmashauri iliyoongozwa na CCM miaka yote Temeke na sasa Kigamboni hawakujua watahitaji eneo kubwa la stand maeneo ya pale ferry ?
Maeneo yalikuwepo lakini viongozi wakayauza
 
Nchi inarudi kwenye migomo? Iringa wamegoma mwezi uliopita, Mbeya wamegoma juzi, leo hii tena jijin huko duuuu
Na ndio matatizo ya kuongoza nchi kibabe bila kufuata taratibu. Wapinzani walipokuwa wanasema nchi iendeshwe kwa kufuata taratibu mlikuwa mnasema kuwa wanatumiwa na mabeberu, ikawa nchi nzima inafuata maamuzi ya mtu mmoja hata kama ni ya ovyo (kama kuruhusu wamachinga kila mahali)
 
Kwa nilivyockia mm mabas yote yanayotoka sehem zote lazima yapitie pale fery kushusha abiria ambao wanavuka kwa panton, n wanaotaka kupanda yale y machinga wanapelekwa mpaka apo tungi
 
Nchi inarudi kwenye enzi zake
Migomo na maandamano ni njia ya wananchi husika kufikisha ujumbe.
Wenye mamlaka wakae nao watatue changamoto zao.
Vitisho, Kuvunja kibabe maandamano na migomo ni dalili ya serikali isiyo fuata utawala wa sheria.
Naamini hali hii ingetokea miezi michache nyuma viongozi wa huo mgomo tungewatafuta kwenye fukwe za bahari.
 
Nchi inarudi kwenye migomo? Iringa wamegoma mwezi uliopita, Mbeya wamegoma juzi, leo hii tena jijin huko duuu.
Migomo ni sehemu ya ustaarabu wa collective bargaining.

Hao wafanyabiashara wakisema wanaacha biashara, haina maslahi, serikali itawalazimisha?

Kinachotakiwa hapo ni serikali kuwa na mipango mizuri. Wafanyabiashara hawatagoma.

Wafanyabiashara wakigoma hata kwenye mipango mizuri, serikali iwe tayari na mwendokasi za kutosha, daladala zikigoma mwendokasi zinachukua nafasi.
 
Kigamboni kwa sasa ina wakazi wengi sana,ile stend mwanzo ilikua inaleta shida ata kwa watembea kwa miguu,maana daladala ni nyingi,ila waliko amishiwa ni mbali,navy pale kuna kubwa tu sema ndo hivyo eneo LA jeshi haliguswi,
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom