Mgeni achana noti Mwanza Airport ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgeni achana noti Mwanza Airport !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Janjaweed, Sep 8, 2010.

 1. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  Wakuu, Tanzania ni nchi nzuri na watu wake wana heshima ya ajabu... inasikitisha sana kuona mgeni anakuja, anatukana watoa huduma wetu na mengine mengi, lakini mara nyingi sisi kama watanzania hukaa kimya na kufunika kombe

  nimesoma habari moja ya Mpakistani kuchana noti ya Tanzania nikasikitika sana na cha kwanza nilipata hisia kwamba huyu mtu ni sawa na aliyechana bendera au hata mwenye dharau ya kupindukia... hakufanya hivyo akiwa amelewa wala amekuwa provoked

  Nakumbuka miezi kadhaa iliyopita raia mmoja wa kigeni alimtemea mate polisi wwetu na hatukukaa kimya, rai yangu ni kwamba tulaani kitendo hiki lakini tusiishie hapo

  Kiburi hiki kinaletwa na watu wetu wa idara ya uhamiaji kutoa hivi vibali kwa njia mbadala hivyo kujishusha na kushusha hadhi ya nchi, wageni wanaona sisi sasa ni wa kununuliwa kwa dola chache hivyo sawa tu hata kutudhalilisha

  Mgeni huyu ni wa NGO ya kimarekani, si ajabu dharau hizi zinatokana na mitazamo au hata mazoea ya wageni hawa nchini (dharau)... shirika lililomwajiri tayari lina wageni wengine, na inawezekana kabisa dharau hizi zimo ndani ya shirika na hasa kwa wageni waliobaki

  tulaani kitendo hiki
  tumulike haya na-NGO
  Somo la uraia lifundishwa kwa wageni ili waelewe watanzania tuna culture yetu
   
 2. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Ondoeni Chama Cha Mafisadi madarakani ndipo mtakapo kipatia CHADEMA na DK Slaa uongozi wa nchi mtaweza kutatuliwa tatizo lenu, ila kwa sasa vumilia maana mliyataka wenyewe mlipomchagua huyu muanguka majukwaani kuongoza nchi. Nyerere si aliwaonya kuwa kama mnamtaka mkanywe naye chai ninyi mkapitiliza mkampatia uongozi wa nchi?
  Hivi ndivyo anavyoongoza, vumilia!
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwa hili sidhani kama ni siasa zaidi.... ni dharau tu
   
 4. jaxonwaziri

  jaxonwaziri JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2010
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 378
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Kama hamjiheshimu atawaheshimu nani Acid?
  Mtajiheshimu vipi ilhali siasa yenu si safi, haijengi uzalendo na utanzania kwanza na vingine ndipo vifuate?
  We need to know the source hapa......!
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sawa jax

  sasa cha kwanza tumshughulikie huyu ili iwe mfano
   
 6. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #6
  Sep 8, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Jax na hili ndio tatizo la waTZ wengi kuingiza siasa kila mahali, Janjaweed analeta hoja ya msingi ya dharau za wageni kwa nchi yetu, we unakimbilia SIASA,! Ni kweli utawala wa nchi hii hauko makini lakini isiwe ndio sababu ya kila hoja ijayo hapa! let be serious even for a second pleeeease!
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ukiona mtu anafanya ujue ameshamaliza dharau zote kwa colleagues wake, majirani (wabongo) na kadhalika... it takes one arrogance to defy everything around... sitanshangaa huyu jamaa akiendelea kuishi nchini maana ni shamba la bibi na waajiri wake labda hawaoni kama ni tatizo

  source Habari leo
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Sep 8, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  I wish Mwl Nyerere angekuwepo.
  Oh! RIP Mwalimu.
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  Sep 8, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Arudi pakistani kupata huduma festi class wakati nchi karibia yote ni swimming pool!!:mad2:
   
 10. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  duuh..
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kwakweli itakua aibu kama huyu jamaa ataachiwa aendelee kuishi nchini
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Usemayo yana ukweli Acid ni Aibu kubwa
   
 13. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwanini alichana pesa yetu?
   
 14. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #14
  Sep 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hii ni dharau kubwa na kosa la jinai kwa nchi. Baadhi ya national symbols kwa nchi yeyoet ni pamoja na
  ;

  1. National Currency

  2. National Flag

  3. National Anthem

  4.etc, etc

  Sasa basi kama ilithibitiska hivyo, mhusika alitakiwa akamatwe mara moja na kufikishwa vyomo vya dola na hatimaye kufunguliwa mashtaka. Tatizo tanzania civic education haipo na mambo yanayofundishwa hata kwa wale wachache hayatilii msimamo na mkazo kwa baadhi ya mambo. Nchi hii bwana, nachoka kabisa.
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  4. kadhalilisha inchi
  mhusika kakamatwa, lakini nahofia asije akawa kama akina chenge tu, maana tanzania ni zaidi ya uijuavyo
   
 16. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #16
  Sep 9, 2010
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii inatokana na ukweli kuwa serikali ya CCM ya sasa inanunulika na kila mgeni analijua hilo ndio maaana wanakuwa na jeuri hii. Ingekuwa enzi za Mwalimu Nyerere asingethubutu kabisa.
   
 17. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #17
  Sep 9, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280

  Tunahitaji kuona mtu anafungwa hapa hapa hakuna kumrudisha NYUMBANI. Anyee debe kwanza hata mwaka mmoja, na viboko kumi nambili. Siku hizi watu wanachezea sana taifa letu, hata Watanzania hatujali kabisa tena viongozi ni jina tu, "Viongozi".

  Ukienda nchi zingine, cha kwanza ni DO's and DON"Ts pamoja na culture kama namna ya kusalimiana na wenyeji. hiyo inahitajika pia kwetu, kama mtu amekuja kwetu lazima afuate sheria zetu huo ujinga uishie kwenye ndege. So sad to see someone from another country do something like that.

  AFUNGWE, Wala hakuna kesi hapo. :A S-coffee:.
   
 18. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  naskia amelipishwa faini ya shilingi elfu tano tu:mad2:,,,, kuna wakubwa wametetea hapo
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Sep 11, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  ............hii sasa dharau faini ya elfu tano!!!
   
 20. P

  PUNJE JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2010
  Joined: Jul 30, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  .duuuuuuu
   
Loading...