Mgawanyiko wa Barabara ya Mbezi mwisho ni moja ya alama kuu za TANROADS

Agrey998

JF-Expert Member
Jul 8, 2019
398
518
Rip kwa Mzee wetu Magufuli na engineer Mfugale leo nichukue fursa hii kuwapongeza watu hawa pamoja na TANROADS kwa kazi bora ya pale barabara ya Mbezi mwisho.

Nilikuwa napita pale kwa Mishe zangu tu tena maramoja moja sana, nikaja kuona uzi wa mtu huku akitabiri kuwa uwepo wa stand ile utasababisha foleni ya kutisha nami ndipo nilianza kuzingatia muundo wa zile barabara na baada ya kupata washirika wa biashara huku ndipo nikaona engineer wa pale alitumia akili kubwa.

Magari yanayotoka Kinyerezi kwenda stendi ya mabasi njia imejitenga, wanaotokea Ubungo njia ya kwenda stand kubwa na ndogo zimejitenga kabisa, wanaotoka mikoani kuingia stand njia yao imejitenga. Nikakaa nikajiuliza sasa huo muingiliano wa kuleta foleni upo wapi. Binafsi sijaona na sijawahi kamatwa na foleni Mbezi hata ya dakika Moja.

Mliotabiri kutakuwa na foleni Nawakaribisha mniambie ambacho sikijui ili nijifunze kwenu pia .
 
Kile unachokiona kimefanyika pale nahakika ni baada ya thread kibao humu ndani ramani ya mwanzo haikuwa vile na pale yamefanyika marekebisho kadhaa hadi kufikia vile.

Yale madaraja ya juu ni marekebisho baada ya kuona wamechemka na foleni ilishaamia mbezi wakaona waweke madaraja.

All in all kazi nzuri inapendeza balaa lililobakia ni kale kanjia ka kwenda Kinyerezi kutoka pale stand ni kembamba mno na hakawezi kuhimili lundo la gari zile itanuliwe hile njia kabla gharama zaidi kuongezeka.
 
Mngeweka na kapicha kalikopigwa kutoka juu nasi tusioijua daslam tuone panafananaje na tuweze kuchangia wapi pamekosewa!
 
weka picha itakuwa more illustrative kuliko maneno
Mzigo huo
JamiiForums-1208557878.jpg
 
Ile ramani sio ya leo ni tangia enzi za Nyerere ndio maana nguzo za yale madaraja ya mbezi zilikuwa zipo chini ardhini hazikujenga from scratch..
 
Back
Top Bottom