Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 1,932
- 4,086
Habari za wakati huu!
Moja kwa moja nawaelekea TANROADS kuhusu hii barabara ya kimkakati inayoanzia darajani kimara mwisho kuelekea tabata bonyokwa mpaka tabata segerea.
Kwa muda mrefu hii barabara imekuwa ikisahaulika kuwekewa lami ilihali ina umuhimu mkubwa sana wa kupunguza foleni ya magari yanayoelekea ubungo kwa kutoa shortcut nzuri kufika tabata pasi na kupitia ubungo kwa wale wanaotokea mbezi na goba.
Barabara hii imekuwa ikileta usumbufu kipindi cha mvua kutokana na kutokufanyiwa matengenezo yoyote.
Wito wangu kwa wizara ya ujenzi na uchukuzi kupitia TANROADS na TARURA kuhakikisha hii barabara inawekwa lami kwani imekuwa ikitumiwa na magari mengi na ni shortcut nzuri sana kwa wale wanaotokea mbezi kuelekea tabata bonyokwa, segerea,kinyerezi,ukonga na gongo la mboto.