Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Makubi: Wananchi chukueni tahadhari za kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya magonjwa, msisubiri matamko

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,958
141,951
Mganga Mkuu wa Serikali Prof Abel Makubi amewataka watanzania kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza kadhalika wajikinge wenyewe na kuwakinga wengine.

Makubi amesisitiza kuwa hizi siyo nyakati za kusubiri matamko wakati unaona kabisa mbele kuna nyoka, jiongeze chukua tahadhari.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

----
Serikali ya Tanzania imetoa maelekezo jinsi ya kuchukua tahadhari kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.

Tamko hilo lililotolewa Jumatano Februari 10, 2021 na mganga mkuu wa Serikali, Profesa Abel Makubi aliyeeleza kuwa magonjwa hayo ni yale yanayosababishwa na vimelea vya bakteria, virusi na wadudu mbalimbali na huambukiza kwa njia mbalimbali.

Ameyataja magonjwa hayo kuwa ni kuhara, homa za mapafu, kifua kikuu, mafua, malaria, dengue, homa ya bonde la ufa na kufafanua kuwa baadhi ya magonjwa ya kuambukiza yanaenda na vipindi vya majira ya mwaka au kutokea kwa mlipuko.

Wananchi wametakiwa kuhakikisha wanawahi katika vituo vya afya mara tu wanapoona dalili za kuugua kwa namna yoyote mfano kuchoka, homa, kukosa hamu ya kula, mwili na kichwa kuuma na kwamba hiyo itasaidia mtoa huduma kumhudumia mhusika kwa wakati kabla mwili haujachoka na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kupona.

Profesa Makubi amewataka wananchi kuzingatia usafi wa mwili wa mtu binafsi, kunawa mikono kwa maji safi yanayotiririka kwa kutumia sabuni katika maeneo ya kazini, shuleni, vyuoni na nyumba za ibada.

Pia, kuhakikisha wanakunywa maji yaliyochemshwa kuanzia nyumbani na kila sehemu ikiwemo mahala pa kazi, kunawa kwa sabuni na maji tiririka mara baada ya kutoka maliwatoni au wanaposhika uchafu katika mazingira yoyote.

“Faida za utekelezaji wa usafi ni kujikinga na maambukizi kutoka mikononi kuingia ndani ya mwili kupitia mdomo, pua, ngozi.

Utekelezaji wa mkakati huu umeleta matokeo chanya kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita ambapo sasa nchi yetu haijapata visa vya kipindupindu,” amesema.

Kuhusu kuzingatia usafi wa mazingira pamoja na kuhakikisha nyumba zinakuwa safi amesema, “utekelezaji huu utakinga dhidi ya magonjwa ya mafua, homa ya mapafu, malaria, kifua kikuu.

Na matokeo yake ni mwili kuepuka kushambuliwa na maradhi yanayozuilika hivyo nguvu ya mwili kujikinga na maradhi kubaki kuwa imara muda wote.”

Katika tamko hilo, wananchi wametakiwa kuimarisha kinga za mwili pamoja na afua tajwa ambazo zinalinda kinga ya mwili kutotumika vibaya kutokana na kushambuliwa na maradhi ya mara kwa mara hususan yanayozuilika.

Nyingine ni kuzingatia lishe bora kuongeza kuimarika kwa kinga ya mwili akitaja vyakula kama mboga za majani, vyakula visivyo na sukari nyingi, matunda na maji kadri ya mahitaji ya mwili.

“Kufanya mazoezi ya mwili na viungo ni nguzo muhimu katika kujenga nguvu ya mwili kuimarisha mifumo ya hewa na mapafu, moyo na mzunguko wa damu.

Kuimarisha zaidi kinga dhidi ya magonjwa yanayoshambuliwa maeneo haya ya mwili na kujenga kinga yenye nguvu zaidi,” amesema.
 
Back
Top Bottom