Chukua tahadhari kujikinga na magonjwa ya mlipuko

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944
📍Dar es salaam​
◾ 17/01/2024

Habari wana-Dar es salaam. Tunamshukuru mungu kwa kutuamsha salaama siku ya leo. Wagonjwa na wanaopitia changamoto mbalimbali mungu awafanyie wepesi waweze kukabiliana nazo na kuwaponya.

➡️ Naomba tuendelee kuchukua Tahadhara katika mkoa wetu wa Dar es salaam na wilaya zote tano, kata 102 na mitaa 564.

➡️ Tujikinge na magonjwa ya mlipuko (Kipindupindu na Ugonjwa wa macho). Tuchukue tahadhari Mapema

1️⃣ Nawa mikono kabla na baada ya kula kwa maji safi sabuni au tumia vitakasa mikono.

2️⃣ Hakikisha unakula matunda masafi.

3️⃣ Chakula cha moto

4️⃣ Maji safi yaliyochemshwa na salama

5️⃣ Elimisha kuhusu magonjwa haya kuanzia ngazi ya familia yako ili kuchukua tahadhari mapema. Muelimisha mwanao kujikinga awapo shuleni na mazingira mengine

6️⃣ Elimisha jamii iliyokuzunguka kuchukua Tahadhari.

7️⃣ Kinga ni bora zaidi kuliko tiba jukumu la kujikinga na magonjwa ni letu sote na kuhakikisha tuchukue tahadhari mapema.

8️⃣ Tufuate kanuni na miongozo inayotolewa na wizara ya Afya.

⏩ Dar es salaam bila magonjwa ya milipuko inawezekana.

Nawatakia Utekelezaji mwema

UWT imara
Jeshi la mama Samia
kazi iendele

UWT ni kwa wanawake wote

Mwajabu R Mbwambo
Mwenyekiti Uwt Mkoa DSM

WhatsApp Image 2024-01-17 at 16.39.56.jpeg
 
Back
Top Bottom