Mfungwa Lillian aliye Hong Kong

Mfungwa Lillian aliye Hong Kong

Dah nimesikiliza mkasa wa huyu binti mdogo aliyekamatwa na madawa ya kulevya nchini Indonesia Mwaka 2017 na kuhukumiwa miaka 18 jela, story yake inasikitisha sana na kuhuzunisha

kitu ambacho anakijutia zaidi ni kukamatwa wakati akiwa bado hajatimiza ndoto yake ya kumjengea nyumba Mama yake , anadai kama angetimiza ndoto yake hiyo , hiko kifungo kisingemuuma sana Kwani angejua Mama yake yupo sehem salama ila sio sasa hivi ambapo hajui hata anakula nini na anaishi vipi na hajui kama akitoka atamkuta mama yake yupo hai au yeye mwenyewe kufia jela.

Kilichonivutia zaidi ni ujasiri aliokua nao wa kusimulia mkasa huo wa kuogopesha na kutisha bila kuwa na uoga wowote au huzuni.

Mungu amsaidie aweze kutumikia kifungo chake salama na kurudi uraiani


Sent from my iPhone using JamiiForums
Kwa hiyo alikamatwa Indonesia akaenda kuhukumiwa Hong kong?
ila kwa kifupi acha ateseke tu,maana hayo madawa yangekuja kuua vijana wengi sana,yangetengeneza mateja na waporaji wengi mno,ngoja ale matunda aloyapanda mwenyewe,hiyo hela ilomfikisha huko akijenga hata nyumba ya mbavuza mbwa,alitaka kutuulia vijana wenzetu.
 
Hajayajua Magereza ya Tanzania narudia hajayajua!
Ni jehanam iliyoko duniani, kule si analala kwenye vitanda, vyumba vina AC ana mashuka, vyumba vina rangi tena unaweza kukuta ana roommate mmoja tu, akiamka asubuhi anakula vinono, anafanya kazi kama mazingira mazuri kama vile watu wa Benjamin Mkapa External!
.
Mwambieni, jela za Tanzania hakuna hata moja yenye AC, yenye vyumba, yenye rangi kwenye cello zake, yenye kazi rahisi, yenye vitanda kama hajawahi kuiona Jehanam na aombe sana serikali imlete hatoamini macho yake
Room yake wako watatu ila msosi ndio hivyo ni mwendo wa wali na mafenesi!😷
 
Ukiwa unafnya biashara haramu inabidi ujiandae kimwili na kiakili
Hupaswi kulalamika maana kete unazobeba kuna mtoto wa mwenzio na yeye anaenda kutumia na kuharibikiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Umesema kweli tupu,yupo mama ambaye miaka ya nyuma,huko alikuwa na uchungu mkubwa wa mtoto wake wa kiume,aliyemaliza kidato cha nne,na alikuwa anafauli vizuri,baadaye akaanza kutumia madawa ya kulevya,bado akiwa Secondary,mpaka mama anakuja kujuwa,mwanawe ni mtumiaji mkubwa wa madawa,mda umepita.Alisikitika sana,na kuwalaani vibaya wauza madawa ya kulevya,mwanawe,hakuweza kumsaidia mama yake,mama aliishi maisha ya tabu,mpaka alifariki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tamaa
Kichwani huwa wanawaza hivi.

Dili likitiki
Nitanunua gari yangu nzuri
Nitafungua biashara zangu
Nitamjengea mama nyumba

Ila wakija kwenye majuto wanaanza
Nilitaka nimjengee mama angu nyumba (hawataji gari nzuri na biashara na kushindana insta na watoto wa mjini)

Atulie atumikie kifungo halal.

Halaf kuna watu wanasema ooh shida zinahamasisha uhalifu.

Niwajibu hivi kwani Tanzania hii kuna maskini wangapi si wapo mamilioni, ingekua hivyo basi crime rates zingekua juu kuliko nchi za america huko.

Tamaaa tu.
Hata kama una mgonjwa kama jambo lipo nje ya uwezo huwezi lazimisha ni kuomba dua tu.

"Kufeli mtihani ambao hukusoma haiumi"
 
Wewe huwa sio mzima unaumwa umasikini na ujinga na bahati mbaya sana ukawa mzaliwa wa Kigoma!!!
.
Iko siku yako, hivi vitu hakuna ambaye huwa anapanga vimtokee, na hata ukikikwepa kama wewe umeandikiwa kuishi jela hakika utaishi kwa namna yoyote.
Hakuna anayeandikiwa kwenda jela...au kufanya uovu..kama ni hivyo tusinge hesabiwa dhambi na kusingekuwa na mahakama!

mbingu na moto tunachagua wenyewe....



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumepoteza vijana kibao waliojihusisha na hiyo deal Erasto wa manzese alipotelea China,Kuna school mate nae tulikua nae Cape alipotelea China,Mwingine alifungwa huko alikomatwa Gaucho alituma ujumbe kuwa anaamini kashapigwa sindano ya sumu alimtumia barua ndugu yake akiwa jela,Dada mwingine yupo Hong Kong maisha hao wadogo waliopelekwa marekani wakina Toshi walipoteza hela baada ya kujiingiza huko na ndugu yake mjomba na ustaadhi huku akiwa na fani yake nzuri kabisa ikawa yeye na jela jela na yeye...tukiwaambia kazeni fanyeni biashara halari walikua wanatuona mafala hiyo sio kazi ya kujaribu wala kufikiri kuifanya nimeona wadogo wengi wakipoteza ndoto zao za maisha huku wangejituma kwa kitu kingine na kuweka muda wangefanikiwa tuu...
 
Nasikia waliachiwa wafungwa elfu 50 huko indonesia kwa ajili ya corona Ila Bahati mbaya haikua kwa foreigners

Huyo binti alikua anaomba sana serikali ya magufuli iwasaidie waamishiwe Magereza ya Tanzania kwan huko wanateseka sana na kubaguliwa


Sent from my iPhone using JamiiForums
Huyu atakuwa hajui magereza ya Tz
 
Wewe huwa sio mzima unaumwa umasikini na ujinga na bahati mbaya sana ukawa mzaliwa wa Kigoma!!!
.
Iko siku yako, hivi vitu hakuna ambaye huwa anapanga vimtokee, na hata ukikikwepa kama wewe umeandikiwa kuishi jela hakika utaishi kwa namna yoyote.
Unapenda watoto wako wauziwe madawa ya kulevya? Mfano huyu angefanikiwa unadhani ni vijana wangapi wa huku Kigoma wangeharibiwa maisha.
Grow up my fair lady
 
Mimi najiuliza ni kwanini hawawataji waliowabebesha!!...maana mtu kashafungwa sijui kwanini anamuonea aibu aliyembebesha


Sent from my iPhone using JamiiForums
Boss acha kabisa kufikiri hivyo, drug dealers sio wenzio wana network mpaka magerezani. Wewe jifanye mwehu uwataje huchukui hata siku moja ukiwa jela wanakuua.
Iko hivi mule Kuna watu kibao wenye kesi hizo hizo za madawa, kazi rahisi kwao Ni kutoa mpunga kwa waliomo ndani wanalipwa wategemezi wa wafungwa wanaopewa kazi ya kukumaliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom