Mfungo wa Ramadhani ufanywe kuwa utaratibu wa kila Siku wa ulaji. Soma Faida hizi za pendekezo hili.

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,577
15,337
Mimi ni mkristo. Nimewahi kushiriki kama wiki nzima kushiriki Mfungo huu.

Asubuhi SAA 9-11 tulifuturu Msosi mzito. Wali, nyama,samaki,tambi,uji,juice,matunda mbalimbali, maji ya kunywa, mboga za majani na Kachumbari mzigo.
Jioni SAA 12 tulifuturu vitu simple simple tu futari.

SABABU KWA NINI MFUMO HAUKUPASWA KUWA SIKU 40 NA ULIPASWA UWE KILA SIKU.

1: Katika maandiko haijaandikwa tule Mara ngapi. Na sijui nani alisema tule Mara tatu. Ila ukila asubuhi vzr kama hivi hauhitaji kula chochote maana unapata nguvu za kutosha kuitafuta saa 12:00 jioni.

2:Kupenda kula hovyohovyo katikati ya mlo ni sababu watu wengi kushindwa kuwa na misimamo. Ndio maana wadada wanaopenda kula kula kila dakika rahisi kuwa wazinzi. Pia sio salama unachanganya mfumo wa uchakataji wa chakula.

3: Unatakiwa kulisha Seli sio Kujaza tumbo. Ni mtazamo potofu eti kushiba ni kujaza tumbo maana tumbo ni kakiungo kadogo sana. Kushiba ni kulisha virutubisho sahihi ambavyo vitazajisha nguvu zitakazokuvusha Siku nzima.

4: Kiafya haishaurili MTU kula muda umeenda sana maana kama ambavyo viungo vyako usiku vinavyopumzika na tumbo linatakiwa lipumzike. Kula jioni hadi unalala tumbo nitakuwa limechakata tayari Msosi.


NINI KITAKUPATA

1: Utakuwa na akili nyingi.

2: Afya njema

3: Kama ni ugonjwa Utayeyushwa maana mfumo huu hautaunga Mkono ugonjwa.

4: utakuwa na nguvu Siku nzima

5: Utakuwa na uwezo wa kusema hapana ukaisimamia bila kuyumbishwa.

6: Rahisi kwenda Peponi.


Ni hayo tu.
Nimepata haya mafunuo nikasema Ni share na jamii yangu hapa.

TAHADHARI
Mfumo huu ni wale ambao kipaumbele cha mapato yao ni chakula kwanza mengine baadae.
 
Back
Top Bottom