Kumbukumbu ya Mfungo wa Ramadhani 3: Futari ya Ally Sykes na Sinia la Kunde za Bibi Titi

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,265
KUMBUKUMBU YA MFUNGO WA RAMADHANI 3: FUTARI YA ALLY SYKES NA NA SINIA LA KUNDE ZA BIBI TITI

Binti yangu kaanda meza katuwekea futari.

Tumetoka msikitini tukakaa mezani tunafuturu.

Kipindi kimepita ghafla mwandaaji katutokea anakagua meza.

"Mbona hii mihogo haijaguswa?"

Mwandazi anauliza.

Kimya.

Kasimama jicho linapitia sahani moja moja.

Kimya.

Sasa sioni dalili ya mwanangu kuondoka nasi tuendelee na mikono yetu iendelee kule moyo unakopenda iende.

Kimya.

Mimi nikajibu, "Tumetembelea kote."

Mwanangu hakujibu akanyanyua sahani moja kuelekea jikoni.

Ukweli ni kuwa tumechota muhogo lakini kiduchu sana kiasi unaonekana kama vile haukuguswa.

Hili hakupenda.
Walaji tumefanya khiyana.

Mpishi hakupenda.

Huu muhogo toka jana Chungu Mosi tulitengewa lakini tukadonyoa.

Leo tumewekewa tumedonyoa.

Binti yangu kaghadhibika kidogo bila ya kuonyesha hamaki.

Lakini ujumbe umetufikia walaji sawia.

Nikakumbuka futari ya Ally Sykes na sinia la kunde la Bibi Titi Mohamed.

Bwana Ally katualika futari kwenye nyumba yake Ursino Estate.

Katambua akitualika futari nyumbani kwake Mbezi Beach atatutaabisha.

Yapata saa miaka 40 imefika.

Miaka hiyo Mbezi Beach kulikuwa mbali sana hakuna usafiri wa umma unaofika huko.

Baraza imejaa watu wa Gerezani rafiki zake Bwana Ally toka utoto wao.

Halikadhalika watu wakubwa wapo wanajichanganya na wananchi wapiga kura.

Enzi hizo chama kimoja siasa ni Ujamaa Vijijini na Kujitegemea.

Tuko kwenye shughuli ya Ally Sykes anafuturisha.

Kamata kitu kimoja kutoka kwangu.

Hapa ni Who is Who.

Nani ni nani Dar-es-Salaam.
Jua limetua.

Pameadhiniwa tumefungua kwa kahawa, tende juisi baridi na maji baridi.

Pamekimiwa.
Tumesali.

Sahani zimetandazwa kote mazuliani.

Kila mtu na sahani yake na mbele yake vyombo vilivyojaa vyakula kuanzia kuku, samaki, hadi sambusa, katlesi, chapati maamri, njegere, mbaazi...

Waswahili tuna msemo hukuweko malaika wako alikuwako.

Tumeziinamia sahani tunazungumzanazo.

Mungu atupe nini sisi waja wake.

Mfungo unakaribia kukatika futari yetu makwetu ni muhogo, kunde na maharage.

Enzi hizo tunapanga foleni kupata kilo ya unga wa njano.

Leo Bwana Ally anatumwagia kuku, mchone, sambusa, katlesi...

Sisi wana wa nchi hatuzungumzi na mtu tunazungumza na changu na nguru.

Ghafla Bwana Ally kasimama na sinia kubwa kainyanyua juu anatunadia, "Jamani Bibi Titi katuletea kunde, kunde za Bibi Titi."

Bwana Ally anapita ananadi, "Kunde za Bibi Titi, kunde za Bibi Titi."

Anapita anawapakulia watu kwenye sahani zao.

Ikawa sasa anaitwa kila mahali watu wanataka kula kunde za Bibi Titi.

Mimi nimekaa na Juma Mwapachu tumeelekezana.

Kaka Juma ananiuliza, "Mohamed vipi niite kunde za Bibi Titi?"

"Kaka Juma kunde za Bibi Titi zitaniwia radhi.

Mimi hapa mkono kwenye chapati mkono kwenye kuku samaki."

Juma Mwapachu akaangua kicheko.

"Kaka Juma kunde hiyo ndiyo futari yangu kila siku itaniwia radhi leo naipumzisha."

Allah warehemu wazee wetu hawa kwa baraka za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani."
 
FUTARI NYENGINE
430618935_319241924503768_5539577996712903630_n.jpg
 
Huyu mzee anaishi dunia yake tu yaani
Anachofikiria sijui nini. He is missing a point. Kuna mambo yakishatokea, ndio byebye. Yeye anang'ang'ana kuyabadili. Inachekesha sana lakini. He lives in the world of fantasy which he slowly and over time, has created for himself. Inatia huruma na kusikitisha sana
 
Babu Mada zako zote zunahusu Uislamu na Waislamu.

Hivi watu wa Imani nyingine unawaonaje?

Unaweza kumpenda kwa dhati mtu asiye Mwislamu?
Huyu mzee anaishi dunia yake tu yaani

Huyu anatamani Nchi iendeshwe kidini yaani.

Kwani nyinyi mbuzi za kigalatia mmekatazwa kuanzisha mada za maji ya upakao wa mwamposa na kubarikiwa na papa
Inawauma nini yeye akielezea mambo ya dini yake
Idiotas!
 
Babu Mada zako zote zunahusu Uislamu na Waislamu.

Hivi watu wa Imani nyingine unawaonaje?

Unaweza kumpenda kwa dhati mtu asiye Mwislamu?
Che...
Kwanza tuanze na hili la ''Babu.''

Mimi kwa umri wangu wa miaka 72 watoto wako ndiyo wanaweza kuniita mimi babu.

Wewe unakuwa mwanangu.

Hivyo ikiwa unataka kuniadhimisha kwa umri wangu unatakiwa kuniita ''Baba.''

Mada zangu kuwa ni za Waislam ni kwa kuwa ndiyo jamii niliyozaliwa na kukulia hapa Dar es Salaam.

Kwa ajili hii najua mengi sana katika mji wa Dar es Salaam, wakazi wake na historia yao.

Watu wa imani nyingine nawaona kama watu wengine labda niseme kama wao wanavyoniona mimi.

Kumpenda mtu kwa dhati.
Labda nikuulize kwa nini unadhani inaweza kuwa vinginevyo?

Nimeishi Masaki kwa zaidi ya miaka 30 na nilikuwa nimezungukwa na majirani Wakristo.

Hawakunitaabisha hata siku moja na nakumbuka watoto wetu wakicheza pamoja.

Angalia picha hiyo hapo chini yupo mwanangu katika kundi hilo:

1710793779034.png
 
Anachofikiria sijui nini. He is missing a point. Kuna mambo yakishatokea, ndio byebye. Yeye anang'ang'ana kuyabadili. Inachekesha sana lakini. He lives in the world of fantasy which he slowly and over time, has created for himself. Inatia huruma na kusikitisha sana
How did the Hutus flipped upside down in Rwanda with their majority ratio of 8:2 ?
It was seen as daydreaming fantasy for the Tutsi that turned out to be nightmare for the Hutus
Never say never!
 
Che...
Kwanza tuanze na hili la ''Babu.''

Mimi kwa umri wangu wa miaka 72 watoto wako ndiyo wanaweza kuniita mimi babu.

Wewe unakuwa mwanangu.
Hivyo ikiwa unataka kuniadhimisha kwa umri wangu unatakiwa kuniita ''Baba.''

Mada zangu kuwa ni za Waislam ni kwa kuwa ndiyo jamii niliyozaliwa na kukulia hapa Dar es Salaam.

Kwa ajili hii najua mengi sana katika mji wa Dar es Salaam, wakazi wake na historia yao.

Watu wa imani nyingine nawaona kama watu wengine labda niseme kama wao wanavyoniona mimi.

Kumpenda mtu kwa dhati.
Labda nikuulize kwa nini unadhani inaweza kuwa vinginevyo?

Nimeishi Masaki kwa zaidi ya miaka 30 na nilikuwa nimezungukwa na majirani Wakristo.

Hawakunitaabisha hata siku moja na nakumbuka watoto wetu wakicheza pamoja.

Angalia picha hiyo hapo chini yupo mwanangu katika kundi hilo:

Sawa Babu.
Ukiwa Babu wacha tu uitwe hivyo na yeyote

Hivi asingekuja Mwarabu na kuleta Uislamu. Wewe Ungekuwa katika Hali gani ?
Ungejikataa nafsi yako ?
 
Kwani nyinyi mbuzi za kigalatia mmekatazwa kuanzisha mada za maji ya upakao wa mwamposa na kubarikiwa na papa
Inawauma nini yeye akielezea mambo ya dini yake
Idiotas!
Wewe nilisha kuambia kule kuwa umashinda.
Yaani kila unachokisema ni sahihi kwako.
Huwa nazungumza na watu wenye upeo Mkubwa
 
Wewe nilisha kuambia kule kuwa umashinda.
Yaani kila unachokisema ni sahihi kwako.
Huwa nazungumza na watu wenye upeo Mkubwa
Mbuzi wewe
Unashinda JF kutwa kuchwa na kwa jinsi unavyojinasabisha na hilo jukwaa la wajinga kujadili dini inaonyesha not only your low academic status bali pia ni low IQ
 
Mbuzi wewe
Unashinda JF kutwa kuchwa na kwa jinsi unavyojinasabisha na hilo jukwaa la wajinga kujadili dini inaonyesha not only your low academic status bali pia ni low IQ
Wewe unajuaje kama mimi nashinda kutwa kucha JF, kama na wewe hushindi humu?

Kwahiyo Waislamu ni wajinga wanaojadili Dini Yao?

IQ ni nini ?
What is academic status?
 
Mzee Mohammed, tunafaidika sana na nyuzi zako kama hizi. Kwani zinatupa nadharia maisha yalivyokua jijini miaka hiyo na watu mashuhuri waliokuwepo.
Sijaona lolote la udini hapa zaidi ya mtu mashuhuri amewakirimu watu kwake.
Kuna watu humu wakisikia hata neno 'futari' basi dira ya akili zao inaelekea kwenye udini.
Mzee wetu endelea kutujuza na Mungu akulinde. Tumejifunza mengi kutoka kwako.
 
Babu mufisi, mdini aliyepitiliza, nje ya uislam ni mweupe pee
Ha, ha, ha.
Ninavyojua Babu ana maumivu makubwa moyoni.

Waislamu ndio walio dai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Lakini Leo wametelekezwa kabisa.
Anayekula matunda ya uhuru ni Roman Catholic.
Mimi sio Romani Cathoric.
Babu anaka wote tuwe Waislamu na Sharia itawale.

Au Waislamu wapewe kipaumbele kwenye mambo yote ya nchi.

Nampenda Ni Mwislamu safi kabisa.
 
Wewe unajuaje kama mimi nashinda kutwa kucha JF, kama na wewe hushindi humu.

Kwahiyo Waislamu ni wajinga wanaojadili Dini Yao?

IQ ni nini ?
What is academic status?
This is only first page of your search history, only today
Now tell kama hushindi humu?, then unalala humu ?
1710795097493.png
 
Ha, ha, ha.
Ninavyojua Babu ana maumivu makubwa moyoni.

Waislamu ndio walio dai uhuru wa Tanganyika na Zanzibar.
Lakini Leo wametelekezwa kabisa.
Anayekula matunda ya uhuru ni Roman Catholic.
Mimi sio Romani Cathoric.
Babu anaka wote tuwe Waislamu na Sharia itawale.

Au Waislamu wapewe kipaumbele kwenye mambo yote ya nchi.

Nampenda Ni Mwislamu safi kabisa.
Anataka wawe kundi maalum kama viti maalum?

Wamshike elimu
 
Mzee Mohammed, tunafaidika sana na nyuzi zako kama hizi. Kwani zinatupa nadharia maisha yalivyokua jijini miaka hiyo na watu mashuhuri waliokuwepo.
Sijaona lolote la udini hapa zaidi ya mtu mashuhuri amewakirimu watu kwake.
Kuna watu humu wakisikia hata neno 'futari' basi dira ya akili zao inaelekea kwenye udini.
Mzee wetu endelea kutujuza na Mungu akulinde. Tumejifunza mengi kutoka kwako.
Huyu Babu, kama angejitambulisha katika nchi ya Iran, angepiga pesa ndefu sana.
Iran wanapenda watu wanapenda Dini kama huyu Babu.

Cha msingi akusanye maandiko yake ayapeleke Iran.
Lazima atapata majukumu ya kueneza Uislamu Afrika na Ulaya.
 
Back
Top Bottom