Mfumo wa elimu wa Tanzania na ongezeko la wasiokuwa na ajira

Neyat20

New Member
Jul 23, 2022
1
0
MFUMO WA ELIMU WA TANZANIA NA ONGEZEKO LA WASIOKUWA NA AJIRA

UTANGULIZI:
Elimu ni ule ujuzi ambao mtu anabaki nao baada ya kusahau yale aliyojifunza shuleni(Albert Einstein).
Lakini tukirejelea mfumo wa elimu wa Tanzania haumuandai muhitimu kuja kubaki na ujuzi ambao utakuja kumsaidia hapo baadae kukabiliana na changamoto za kimaisha.

Kwani mfumo wetu wa elimu umeegemea katika kutoa ujuzi ambao unamuandaa na kumjenga mhitimu moja kwa moja kwaajili ya kuajiriwa kuliko kujiajiri. Kutokana na hili imepelekea wasomi wengi kubaki tu mitaani na vyeti vyao bila ajira na wanashindwa kukabiliana na Maisha.

UHUSIANO KATI YA MFUMO WA ELIMU WA TANZANIA NA ONGEZEKO LA WATU WASIOKUWA NA AJIRA.
Elimu yetu haiwaandai wahitimu kujitegemea zaidi ya kuajiriwa, Mfumo wetu wa elimu elimu hauwapatii wanafunzi ujuzi na stadi ambazo zitawasaidia kujitegemea kimasha zaidi ya kuwaanda kwaajili ya kusubiri ajira.

Masharti magumu wakati wa utoaji wa ajira kwa waombaji.

JINSI YA KUONDOKANA NA TATIZO LA ONGEZEKO LA WASOMI WASIO NA AJIRA.
Serikali inatakiwa ifanye marekebisho na maboresho katika sekta ya elimu kama vile kuandaa mitahala ambayo itakuwa inatoa ujuzi na stadi endelevu ambazo zitawasaidia wahitimu kujitegemea zaidi kuliko kutegemea kuajiriwa na serikali."Siyo kila kukicha kuwaambia vijana wajiari/wajitegemee wakati hawana ujuzi wa kujitegemea.

Pia wapunguze masharti magumu wakati wa utoaji wa ajira, Kwa mfano unakuta tangazo linasema mwombaji awe na uzoefu kuanzia miaka mitatu hadi mitaani.Sasa kwa akili ya kawaida huo uzoefu wa kazi atakuwa nao vipi wakati hajawaihi ajiriwa au kufanya hiyoo kazi

Pia serikali iwekeze na iweke kipaumbele katika elimu ya mafunzo ya ufundi(VETA) ili kuweza kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
 
Back
Top Bottom