Mfumo wa elimu Tanzania wafumuliwa.

Mfumo wa elimu Tanzania wafumuliwa.

Veta hawafundishi ufundi?..hujaona kila shule kuwepo watu wa veta kwenye hiyo taarifa?
Idadi ya veta na shule zilizokusudiwa?
Halafu usidhani tunakosoa kama lengo la serikali ni baya,ila mikakati Yao ndio mibovu.
Mifano tunayo mashuleni,walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ni wachache.
Kuna upungufu wa vifaa vya maabara nk.
Baadhi ya shule zimeshindwa kufundisha computer science kisa hakuna mwalimu na vifaa.
Kwa hiyo hili suala wamekurupuka japo lengo ni zuri
 
yote sawa ila somo la Tanzania na maadili ni la kufuta hawa watoto hamtoweza kama mlivyoweza kutubrain wash sisi wahenga. Eti unamfundisha Gen z rangi za bendera mqra ngao ya taifa .. ni kupeteza nguvu
 
Bado imeegamia kwenye nadharia zaidi. Kwa namna fulani ilibidi ufundi iwe mandatory. Ukienda kusoma Physics ulazimishwe kusomea ufundi fulani kama ni mechanics, electronics, etc etc ili ukitoka hapo uwe na uwezo wa KUFANYA.​
 
Waweke msisitizo kwenye uandishi watu wanamaliza vyuo hawajui tofauti ya R na L. A na HA. Uandishi umekua janga la taifa kama somo la Hisabati.
Hii siyo uandishi per se bali ni uduni wa elimu nzima. Huu mfumo wao mpya walishirikisha wataalam na kuangalia elimu za wengine au ndiyo wamekurupuka kama kawaida yao? Walishafanya matayarisho? Ujinga unaoendelea nchi sasa hivi ni matokeo ya Nyerere kufumua mfumo wa elimu waliyoacha wakoloni na yeye kubuni mfumo wake. Si ajabu hata sasa hivi tunafanya tena kosa jingine linalofanywa kwa mihemko ya wanasiasa ucharwa.
 
Bado imeegamia kwenye nadharia zaidi. Kwa namna fulani ilibidi ufundi iwe mandatory. Ukienda kusoma Physics ulazimishwe kusomea ufundi fulani kama ni mechanics, electronics, etc etc ili ukitoka hapo uwe na uwezo wa KUFANYA.​
Hicho kitu kitabaki hivyohivyo,wasoma historia ya ufundi na historia ya sayansi,vitendo 0
 
Muulize profesa Mkenda

😆😆
Eti elimu! ukiwa unasoma humu utadhani wana hizo shule za kufundishia watoto! Waka
Muulize profesa Mkenda

😆😆
Utadhani kuna shule na mazingira ya kufundishia watoto wetu! Jamani hawa viumbe hawana aibu shule zenyewe ni magofu tu hata hiyo physics inayosemwa haina uhusiano na mahala inaposemwa itafundishwa
 
Hii siyo uandishi per se bali ni uduni wa elimu nzima. Huu mfumo wao mpya walishirikisha wataalam na kuangalia elimu za wengine au ndiyo wamekurupuka kama kawaida yao? Walishafanya matayarisho? Ujinga unaoendelea nchi sasa hivi ni matokeo ya Nyerere kufumua mfumo wa elimu waliyoacha wakoloni na yeye kubuni mfumo wake. Si ajabu hata sasa hivi tunafanya tena kosa jingine linalofanywa kwa mihemko ya wanasiasa ucharwa.

Hadi Nyerere anaondoka madarakani, elimu ilikuwa nzuri. Mtu akimaliza darasa la saba alikuwa anajua kusoma, kuandika na hesabu vizuri, na angeweza kuingia kwenye soko la ajira. Elimu ilianza kuvurugika zaidi enzi za JK wa Msoga. Tangu hapo, shule nyingi zinapika mabomu tu, na wahitimu wetu wanapata shida ku-compete globally, wakisikia wakenya au wageni wanaloa.
 
Mkuu nakubaliana na wewe. Kipindi cha Nyerere ilikuwa afadhali. Lakini ni afadhali kulinganisha na sasa na siyo kuwa ilikuwa ya kiwango kizuri ukilinganisha na nchi nyingine. Kuhusu huyu mzee wa Msoga, ndiyo mwasisi wa ujinga wote unaoendelea Tanzania sasa hivi. Angekuwa ameingia Salum pengine tungekuwa bado tuko vizuri,
 
Ni kama shule za kata zilivyopingwa,siku hizi zinatoa one na two kibao
Taratibu tutafika,tafuta watu wa computer science,it fundisha ualimu miezi sita sukuma kafundishe watoto coding
Unadhani ni rahisi mtu kasoma Computer Science degree , alipata div one ya 3,4,5 Advance aende kuwa mwalimu kwa mshahara wa 900K?
 
Back
Top Bottom