Mfumo wa elimu Tanzania wafumuliwa.

Mfumo wa elimu Tanzania wafumuliwa.

Hivi coding ni nini?..najua bill gates hakutengeneza codes za Microsoft bali alinunua kwa mhadhiri wa chuo na hela alipewa na wazazi wake $50k na huwa naeleza kweli kwenye kahawa kwa confidence ya juu,lakini sijui coding ni nini
Coding ni tendo ambalo mtu ambae amemaster kutumia aina fulani ya lugha ambayo computer anaweza ielewa ili computer aweze kufanya kazi inayokusudiwa .
 
Tungeweka tu michepuo mitatu tangu O-Level.
Sayansi.
Biashara.
Utumishi.
Halafu ni mwendo wa kazi kwa vitendo, kama ni biashara ya kilimo mtu apewe eka ya shule kabisa ni mwendo wa kulima, kuvuna, kusafirisha na kuuza, akifanya mara 10 kwa mafanikio apewe cheti aende chuo, huko nako akapewe eka 100.
 
MABADILIKO MAPYA YA MITAALA YA ELIMU SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO 2025

MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU:

1. Mtihani wa darasa la Saba utafutwa ifikapo 2027.

2. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize Kidato cha nne. Hii itaitwa Elimu ya Msingi.

3. Kutakuwa na Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la sita (STANDARD SIX NATIONAL ASSESSMENT) ifikapo 2027.

4. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza Kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza. Hii itaanzia Secondary ambapo kutakuwa na mikondo miwili; Jumla na Amali.

5. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa kama somo kwa Shule za Kiswahili Medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa Shule za English Medium.

6. Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 tofauti na ya sasa miaka 7.

8. Elimu ya Awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5. Mwanzoni elimu ya awali haikuwa rasmi na shule za Serikali haikuwepo. Sasa itakuwepo kwa utaratibu huo.

9. Masomo ya Elimu ya Msingi yatakuwa ni KKK(Kusoma, Kuhesabu, Kuandika), Jiografia, kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati, Sayansi, historia ya TANZANIA na Maadili, Dini na kiingereza na Stadi za Kazi itachomekwa.

10. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

11. Shule zenye uwezo zitafundisha angalau somo moja la lugha za kigeni kama Kichina au Kifaransa.

12. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na Amali (Ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo, matakwa na malengo yake ya baadaye.

13. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani zifuatazo:-


14. Mwanafunzi wa Mkondo wa Amali atatakiwa kuchukua Masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

15. Masomo ya jumla ya wanafunzi wa Amali ni:-


16. Wahitimu wa Amali watapata vyeti viwili yaani:-


17. Kila shule itakuwa na Wakala wa VETA ili kusimamia masuala ya Ufundi.

18. Kila shule haitakuwa na Mikondo zaidi ya miwili ya Ufundi, hii ni kwa ajili ya Ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

19. Kutaanzishwa somo jipya la Mawasiliano ya Kitaaluma (ACADEMIC COMMUNICATION) katika A-level na Ualimu.

20. CODING itafundishwa Shule za Msingi.

21. INFORMATION and COMPUTER STUDIES (ICS) itabadilishwa na kuitwa COMPUTER SCIENCE.Somo limesukwa upya.

22. CIVICS itaunganishwa na Historia ya TANZANIA na Maadili kwa O-level.

23. O-level Masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

24. Katika O-level Masomo ya Biology na Geography yatakuwa Masomo ya kuchagua pia kwa sababu Maudhui yake yamekuwa kwenye Masomo ya Jiografia na Sayansi ya Shule ya Msingi kwa mfano Afya ya Jamii, Afya ya Uzazi, Magonjwa ambukizi nk.

25. Civics, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadili yamefutwa, Maudhui yake yameingia katika somo la Historia ya TANZANIA na Maadili.

26. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na Maudhui yake yatawekwa katika Somo la Historia ya TANZANIA na Maadili na Mawasiliano ya Kitaaluma.

27. Kufuta baadhi ya Masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudiarudia kwa Maudhui.

28. Michepuo katika Elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9).

Michepuo iliyoongezeka ni:-


29. Masomo ya O-level yatakuwa:-


30. Astashahada ya Ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (DIPLOMA) ya Elimu ya Awali, Ualimu wa Msingi na Ualimu wa Elimu Maalumu.



31. Walimu wa Sekondari wote watakuwa na Shahada (DEGREE). kwa sababu nchi nyingi zinaenda na mwelekeo huu.

32. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (DIPLOMA) ya Ualimu wa Sekondari vitatumika kutoa continuous Professional Development.

#Wizarayaelimu
#ortamisemitz
#Kigoma
#kigomandiokwetuupdates
Imekaa njema ila wasije wakabadilisha badilisha kama alivyokuja MUNGAI na kumixxByYas masomo ya biashara na syansi.
 
Maazimio ni mazuri, utelelezaji sasa.

Tuko nyuma zaidi ya sana katika kufikia SGDs namba 4 ambayo ni Quality education
 
Ila serikali imezingua kwanini somo la biology liwe option wakati linafundisha afya na mazingira
Wako sawa kabisa tena ikiwezekana hesabu tu ndio iwe compulsory mtu asome kitu atakachobobea tu, Lundo la masomo la nini?
 
Ni kama shule za kata zilivyopingwa,siku hizi zinatoa one na two kibao
Taratibu tutafika,tafuta watu wa computer science,it fundisha ualimu miezi sita sukuma kafundishe watoto coding
Inshu sio kutoa one na two, inshu ni ubora wa hiyo elimu
Mimi mwenyewe nilitoa one ya kata, tena one moja tu shule nzima, ila ubora wa elimu nilioipata niliujua vizuri baadae.

Naihakika hata mtoto wako mwenyewe kama unae hujampeleka kwenye izo shule za kata. Hao CCM wenyewe wanoo tutengenezea izo shule za kata na kutupangia iyo mifumo ya elimu familia zao wanasoma wapi ?.
 
Maazimio ni mazuri, utelelezaji sasa.

Tuko nyuma zaidi ya sana katika kufikia SGDs namba 4 ambayo ni Quality education
Mamkwe umepiga kwenye mshono.

Mimi nasisitiza sana kwenye ujuzi wa lugha zote za kigeni na Kiswahili.

Tena iwe ni ujuzi kweli kweli sio mambo ya ubabaishaji.

Siku hizi ni kawaida sana kukutana na wanafunzi hata wa chuo kikuu wasiojua hata Kiswahili.

FutaRi mtu anakwambia FutaLi.

Au maRinda mtu anakwambia maLinda.

Huu ni upuuzi sana mamkwe.
 
Mamkwe umepiga kwenye mshono.

Mimi nasisitiza sana kwenye ujuzi wa lugha zote za kigeni na Kiswahili.

Tena iwe ni ujuzi kweli kweli sio mambo ya ubabaishaji.

Siku hizi ni kawaida sana kukutana na wanafunzi hata wa chuo kikuu wasiojua hata Kiswahili.

FutaRi mtu anakwambia FutaLi.

Au maRinda mtu anakwambia maLinda.

Huu ni upuuzi sana mamkwe.
Niongee kwa kusimama au kwa kukaa 😂😆

Kingereza meyoo, kiswahili pia meyoo!
 
Siku hizi degree anayo hata ambaye haujui kusoma Na kuandika..low IQ..imeshusha thamani ya elimu kabisa
 
Back
Top Bottom