Mfumo wa elimu Tanzania wafumuliwa.

Mfumo wa elimu Tanzania wafumuliwa.

Hivi coding ni nini?..najua bill gates hakutengeneza codes za Microsoft bali alinunua kwa mhadhiri wa chuo na hela alipewa na wazazi wake $50k na huwa naeleza kweli kwenye kahawa kwa confidence ya juu,lakini sijui coding ni nini
Coding ni computer programming language ambayo hutumika kutengenezea websites, apps, n.k kwa kutumia python, java script na C++
 
si kuna wanaosema historia yenywe kwanza imekosewa ni ya upande fulani huku upande fulani ukiwa historia yao haijaandikwa vyema
Imefichwa, harakati za TAA na TANU kabebeshwa Nyerere,wazee waliopambana na mjerumani hawaandikwi kwa majina yao ya kiarabu mfano mkwawa haandikwi abdallah,songea mbano haandikwi Abdul rauf,kinjekile haandikwi Abu bakri,kuna agenda nyuma ndiyo ila tunaweza rekebisha
 
Wakati huu shule zina waalimu mpaka wawili walimu haswa msingi hata sec wanafundisha masomo sita hata zaidi..

Je hizi ngonjera zote wana mpango gani kuongeza idadi ya waalimu?

Bila kujali sana ikiwa wamefunzwa mambo ya kisasa maana mtu akifaulu ualimu ameiva katika kumshape mwanafunzi ndio maana kuna wakati walimu wa sec walishushwa wakapelekwa kufundisha msingi.

Ila wakifanya siasa wakaacha kuongeza nguvu kazi wakati gari linanock engine itakuwa yaleyale ya akina Mungai na Mama Sitta...ℹ️🥱
Sioni mafanikio ya hili jambo zaidi ya mikurupuko square
 
Bado masomo ni mengi, na bado muda wa kuingia shuleni ipunguzwe mpaka miaka 5, halafu mtoto akishamaliza elimu ya msingi iwe lazima asome hio amali, achague mchepuo kabisa kama ni computer science asome mpaka achoke Nigeria tu hapo mtoto wa miaka 18 ana degree, mwanzo mzuri lakini kijana masomo ya msingi yasizidi ma 3 + fani yake atakayochagua imetoka hiyo, dunia haina muda tutengeneze experts tu maisha mafupi mno mtu kukaa shuleni wakati mtaa ndio una experience zaidi
 
Imefichwa, harakati za TAA na TANU kabebeshwa Nyerere,wazee waliopambana na mjerumani hawaandikwi kwa majina yao ya kiarabu mfano mkwawa haandikwi abdallah,songea mbano haandikwi Abdul rauf,kinjekile haandikwi Abu bakri,kuna agenda nyuma ndiyo ila tunaweza rekebisha
sawa warekebishe sasa ili malalamiko yaishe au kuna kikwazo?
 
Bado masomo ni mengi, na bado muda wa kuingia shuleni ipunguzwe mpaka miaka 5, halafu mtoto akishamaliza elimu ya msingi iwe lazima asome hio amali, achague mchepuo kabisa kama ni computer science asome mpaka achoke Nigeria tu hapo mtoto wa miaka 18 ana degree, mwanzo mzuri lakini kijana masomo ya msingi yasizidi ma 3 + fani yake atakayochagua imetoka hiyo, dunia haina muda tutengeneze experts tu maisha mafupi mno mtu kukaa shuleni wakati mtaa ndio una experience zaidi
umeongea la maana na by the way AI inafanya kazi nyingi sana ambazo awali ilikuwa zinafanywa na watu wengi sana
 
Hayo masomo ni yaleyale,vimeongezwa vitu na vimeondolewa baadhi,wizara ya elimu kuna wataalam wa elimu,punguzeni ujuaji
Mkuu,umesoma Uzi lakini au wewe nawe ni msomi uchwara,
Hao wataalamu kipindi Mungai anavurunda hawakuwepo?
Kuna masomo mapya mtoa mada kaandika,Kuna masomo ya ufundi hapo,je walimu walishaandaliwa?
 
MABADILIKO MAPYA YA MITAALA YA ELIMU SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO 2025

MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU:

1. Mtihani wa darasa la Saba utafutwa ifikapo 2027.

2. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize Kidato cha nne. Hii itaitwa Elimu ya Msingi.

3. Kutakuwa na Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la sita (STANDARD SIX NATIONAL ASSESSMENT) ifikapo 2027.

4. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza Kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza. Hii itaanzia Secondary ambapo kutakuwa na mikondo miwili; Jumla na Amali.

5. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa kama somo kwa Shule za Kiswahili Medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa Shule za English Medium.

6. Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 tofauti na ya sasa miaka 7.

8. Elimu ya Awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5. Mwanzoni elimu ya awali haikuwa rasmi na shule za Serikali haikuwepo. Sasa itakuwepo kwa utaratibu huo.

9. Masomo ya Elimu ya Msingi yatakuwa ni KKK(Kusoma, Kuhesabu, Kuandika), Jiografia, kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati, Sayansi, historia ya TANZANIA na Maadili, Dini na kiingereza na Stadi za Kazi itachomekwa.

10. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

11. Shule zenye uwezo zitafundisha angalau somo moja la lugha za kigeni kama Kichina au Kifaransa.

12. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na Amali (Ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo, matakwa na malengo yake ya baadaye.

13. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani zifuatazo:-

14. Mwanafunzi wa Mkondo wa Amali atatakiwa kuchukua Masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

15. Masomo ya jumla ya wanafunzi wa Amali ni:-

16. Wahitimu wa Amali watapata vyeti viwili yaani:-

17. Kila shule itakuwa na Wakala wa VETA ili kusimamia masuala ya Ufundi.

18. Kila shule haitakuwa na Mikondo zaidi ya miwili ya Ufundi, hii ni kwa ajili ya Ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

19. Kutaanzishwa somo jipya la Mawasiliano ya Kitaaluma (ACADEMIC COMMUNICATION) katika A-level na Ualimu.

20. CODING itafundishwa Shule za Msingi.

21. INFORMATION and COMPUTER STUDIES (ICS) itabadilishwa na kuitwa COMPUTER SCIENCE.Somo limesukwa upya.

22. CIVICS itaunganishwa na Historia ya TANZANIA na Maadili kwa O-level.

23. O-level Masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

24. Katika O-level Masomo ya Biology na Geography yatakuwa Masomo ya kuchagua pia kwa sababu Maudhui yake yamekuwa kwenye Masomo ya Jiografia na Sayansi ya Shule ya Msingi kwa mfano Afya ya Jamii, Afya ya Uzazi, Magonjwa ambukizi nk.

25. Civics, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadili yamefutwa, Maudhui yake yameingia katika somo la Historia ya TANZANIA na Maadili.

26. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na Maudhui yake yatawekwa katika Somo la Historia ya TANZANIA na Maadili na Mawasiliano ya Kitaaluma.

27. Kufuta baadhi ya Masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudiarudia kwa Maudhui.

28. Michepuo katika Elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9).

Michepuo iliyoongezeka ni:-

29. Masomo ya O-level yatakuwa:-

30. Astashahada ya Ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (DIPLOMA) ya Elimu ya Awali, Ualimu wa Msingi na Ualimu wa Elimu Maalumu.

31. Walimu wa Sekondari wote watakuwa na Shahada (DEGREE). kwa sababu nchi nyingi zinaenda na mwelekeo huu.

32. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (DIPLOMA) ya Ualimu wa Sekondari vitatumika kutoa continuous Professional Development.

#Wizarayaelimu
#ortamisemitz
#Kigoma
#kigomandiokwetuupdates
Elimu ya msingi inatakiwa kuwa sawa na form 2 tu ....hapo pawekwe mtihani mkukwa sana wa mchujo ...watakao vuka wawe ni wenye uwezp mkubwa wa kukabili masomo mazito ....somo la HESABU LIWE NDIYO SOMO BABA ...MTU YOYOTE ASIWEZE KUSOMA ELIMU YOYOTE YA JUU BILA YA KUFIKIA VIWANGO VYA UELEWA WA HESABU VINAVYO TAKIWA ...
Hivyo elimu ya msingi igawanywe vipande viwili ...yaani
A)PRIMARY 5YR
B)ADVANCE PRIMARY 3YR

...UPUMBAVU WA DINI UFUTWE KWENYE SHULE ZOTE HADI ZA TAASISI ZA DINI ZINAZO TOA ELIMU DUNIA ....HIJABU NA TAKAKAKA ZINGINE ZA KIDINI ZISIRUHUSIWE ...ZINAJENGA TAIFA LENYE MPASUKO NA KULETA USHABIKI WA KIDINI ...
....Kuanzia ADVANCE PRIMARY LUGHA ZA KUFUNDISHIA ZITUMIKE ZOTE MBILI KWA KILA SOMO ..Hapa kuna mfumo maalumu wa jinsi ya kutumia lugha zote mbili kwa masomo yote.

MFUMO WA KUTUMIA LUGHA ZOTE MBILI NI MFUMO BORA SANA . nitakuja kueleza .
 
Ushauri wangu 5(msingi) +3(olevel) +1(Alevel or option)+diploma 2 or degree 3

Angalizo mtoto apendekezwe fani yake tangu msingi akifika sec haina kurudi nyuma kama ni ujenzi, kupaua, football, au chochote alicho chagua msingi ni kuunga tu mpaka degree asipoteze muda, watu wengi tu wanaoajiriwa siku hizi wamesomea ujinga mwingine wana fanya kazi nyingine tofauti kabisa
 
MABADILIKO MAPYA YA MITAALA YA ELIMU SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO 2025

MABORESHO YA MITAALA AMBAYO YANAENDA KUBADILISHA MFUMO WETU WA ELIMU:

1. Mtihani wa darasa la Saba utafutwa ifikapo 2027.

2. Mwanafunzi akianza darasa la kwanza lazima amalize Kidato cha nne. Hii itaitwa Elimu ya Msingi.

3. Kutakuwa na Mtihani wa Upimaji wa Kitaifa wa darasa la sita (STANDARD SIX NATIONAL ASSESSMENT) ifikapo 2027.

4. Mwanafunzi atatakiwa asome fani fulani kabla hajamaliza Kidato cha nne ili aweze kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza. Hii itaanzia Secondary ambapo kutakuwa na mikondo miwili; Jumla na Amali.

5. Lugha ya kufundishia na kujifunzia itakuwa kiswahili, Kiingereza kitakuwa kama somo kwa Shule za Kiswahili Medium na lugha ya kufundishia English, kiswahili kitakuwa Kama somo kwa Shule za English Medium.

6. Elimu ya Msingi itakuwa miaka 6. Mwanafunzi ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka 6 tofauti na ya sasa miaka 7.

8. Elimu ya Awali mwanafunzi ataanza akiwa na miaka 5. Mwanzoni elimu ya awali haikuwa rasmi na shule za Serikali haikuwepo. Sasa itakuwepo kwa utaratibu huo.

9. Masomo ya Elimu ya Msingi yatakuwa ni KKK(Kusoma, Kuhesabu, Kuandika), Jiografia, kiswahili, Sanaa na Michezo, Hisabati, Sayansi, historia ya TANZANIA na Maadili, Dini na kiingereza na Stadi za Kazi itachomekwa.

10. Kiingereza kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwa shule za Kiswahili na kiswahili kitafundishwa kuanzia darasa la kwanza kwanza kwa shule za kiingereza.

11. Shule zenye uwezo zitafundisha angalau somo moja la lugha za kigeni kama Kichina au Kifaransa.

12. Sekondari kutakuwa na mikondo 2, mkondo wa jumla na Amali (Ufundi). Mwanafunzi atachagua kutokana na uwezo, matakwa na malengo yake ya baadaye.

13. Mkondo wa amali (ufundi) utakuwa na fani zifuatazo:-

14. Mwanafunzi wa Mkondo wa Amali atatakiwa kuchukua Masomo manne (4) ya jumla na moja la fani.

15. Masomo ya jumla ya wanafunzi wa Amali ni:-

16. Wahitimu wa Amali watapata vyeti viwili yaani:-

17. Kila shule itakuwa na Wakala wa VETA ili kusimamia masuala ya Ufundi.

18. Kila shule haitakuwa na Mikondo zaidi ya miwili ya Ufundi, hii ni kwa ajili ya Ufanisi na fani ziwe zinaendana na fursa za eneo husika.

19. Kutaanzishwa somo jipya la Mawasiliano ya Kitaaluma (ACADEMIC COMMUNICATION) katika A-level na Ualimu.

20. CODING itafundishwa Shule za Msingi.

21. INFORMATION and COMPUTER STUDIES (ICS) itabadilishwa na kuitwa COMPUTER SCIENCE.Somo limesukwa upya.

22. CIVICS itaunganishwa na Historia ya TANZANIA na Maadili kwa O-level.

23. O-level Masomo ya lazima yatakuwa 6 badala 7 ya Sasa.

24. Katika O-level Masomo ya Biology na Geography yatakuwa Masomo ya kuchagua pia kwa sababu Maudhui yake yamekuwa kwenye Masomo ya Jiografia na Sayansi ya Shule ya Msingi kwa mfano Afya ya Jamii, Afya ya Uzazi, Magonjwa ambukizi nk.

25. Civics, Maarifa ya Jamii, Uraia na Maadili yamefutwa, Maudhui yake yameingia katika somo la Historia ya TANZANIA na Maadili.

26. General Studies (GS) katika A-level itafutwa na Maudhui yake yatawekwa katika Somo la Historia ya TANZANIA na Maadili na Mawasiliano ya Kitaaluma.

27. Kufuta baadhi ya Masomo kumefanyika ili kuondoa tatizo la kujirudiarudia kwa Maudhui.

28. Michepuo katika Elimu ya O-level imeongezeka kutoka minne (4) hadi tisa (9).

Michepuo iliyoongezeka ni:-

29. Masomo ya O-level yatakuwa:-

30. Astashahada ya Ualimu itafutwa kisha itaanzishwa Stashahada (DIPLOMA) ya Elimu ya Awali, Ualimu wa Msingi na Ualimu wa Elimu Maalumu.

31. Walimu wa Sekondari wote watakuwa na Shahada (DEGREE). kwa sababu nchi nyingi zinaenda na mwelekeo huu.

32. Vyuo vilivyokuwa vinatoa Stashahada (DIPLOMA) ya Ualimu wa Sekondari vitatumika kutoa continuous Professional Development.

#Wizarayaelimu
#ortamisemitz
#Kigoma
#kigomandiokwetuupdates
CCM bhana ivi nyie mbona ving'ang'a sana? kama UKIMWI! hatuwataki
 
Back
Top Bottom