Mfanyabiashara wa utalii ajinyonga Moshi

Mfanyabiashara wa utalii ajinyonga Moshi

Kakwepa aibu za kusengenywa kuwa amefilisika si unawajua wamatumbi kwa kufuatilia maisha ya watu tena?
Hata wakikusengenya watanufaika na nini? Jamaa alikuwa na connection kubwa kiasi fulani kwa watalii wake, hata angeshuka bado nafasi ya kuinuka ilikuwa n kubwa mno.
 
Kabisa,Mimi naona wazungu kwenye kujikubali wametuzidi sana,hawajali unasema nini maadamu yeye anafanya kitu sahihi havunji sheria utajua mwenyewe,kama ni ukweli atakwambia ukweli sio kukupamba,ndio maana ni rahisi kutaja analipwa mshahara kiasi gani,anamiliki nini,ana madeni gani,ila waafrika tuna unafiki fulani ambao hauna maana,kumchekea mtu kinafiki badae mnamkalia vikao
Ndio ujinga wetu watu weusi hatuishi uhalisia kabisa.
 
Ila bongo yetu hii. Mtu akijinyonga utaona kila mtu akimlaumu kwa nini hakusema ili apewe msaada ila ikitokea moment ukawa unatoa shida zako. Wote wanakukimbia

Kwa hiyo siwezi kujua sababu zake za kujimaliza ila nature yetu binadamu ya kuwapenda watu wakiwa vizuri. Ndio inasababisha hili
Nachoamini na ndio uhalisia wa maisha kwa wengi ni kuwa unapopitia magumu na kuhitaji msaada mtu pekee wa kuweza kuwa nawe 100% ni wewe mwenyewe. Utakubaliana nami kama umeshawahi kupitia changamoto kubwa ya kifedha.

Tutafute hela sana hao wa kutoa msaada huenda na wao wana yao wanayokabiliana nayo kimya kimya ila tutawaangushia lawama bure kuwa hawawezi kusaidia.
 
Back
Top Bottom