MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

Ntate Magolo, tatizo sio Serikali bali Wabunge. Hata hivyo TRA hawajali kwa sababu kila mwaka wanakuongezea penati na hata ukichinja gari, siku ukienda TRA kwa suala lolote la kodi, watakukaba ulipe kwanza kodi ya Road License na penati zake hata za miaka kumi, uonevu mtupu.

Vv
 
Bonge la ushauri sema wasi wasi wangu kama Mafuta yakipanda bei (hata kwa shilingi 50) basi ujue unga, Mafuta ya kula, nyama, nauli, dagaa, maharage nakadhalika nakadhalika vitapanda bei... watakao umia ni tabaka la chini walio wengi.. PROBLEM ya nchi hii siasa imewekwa mbele na hata wateule wa dereva wa roli % kubwa ni mabashite kwa hiyo mawazo kama haya hawana labda wake kuiba humu JF
 
Ntate Magolo, tatizo sio Serikali bali Wabunge. Hata hivyo TRA hawajali kwa sababu kila mwaka wanakuongezea penati na hata ukichinja gari, siku ukienda TRA kwa suala lolote la kodi, watakukaba ulipe kwanza kodi ya Road License na penati zake hata za miaka kumi, uonevu mtupu.

Vv
Kwa ukali bila maelewano,ngumu kuwakaba kwa sababu 1. Wengi wamebadilika kuwa Chingas,na hawalipi. 2. Wamehamia kwenye shughuli zisizo na usumbufu wa kodi mf.kilimo,ufugaji nk. 3. Wamebadili brand za umiliki,anafunga biashara na kufungua kwa jina la mjomba. Hivyo utakuta duka lililokuwa la Mkinga,sasa ni la mpare. 4. Wamehamia nchi nyingine,wanavuna huko,na kurudi kupumzika nchi ya bibi.
 
Wazo ni ziri sana nafikiri serikali ibuni mbinu mujalabu ambao utafanya ulipaji wa kodi usiwe na maumivu kwa walipaji kiasi wakajikuta wanatafuta mbinu za kukwepa kulipa kodi,ulipaji wenye mpangilio mzuri ambao ukawekwa katika mazingira mazuri nafikir utamfanya mlipa kodi kuwa na amani katika kulipa kwake ukilinganisha na mazingira ya sasa
 
Kila kilicho chema huanza na mbegu, wazo lako ni kweli inahitaji maboresho ya kisayansi, imani hii topic itasomwa na ipo siku itakuwa effective
 
Wazo zuri, mimi huu ni mwaka wa tatu tangu nimeifungia bandani gari yangu kwa kushindwa maintenance cost na Road Licence inayodaiwa ndio kabisaa kizungumkuti hata wanunuzi hawarudi tena. Nafikiri hata ulipiaji vighamuzi sio rafiki kwa walalahoi wengi, kwanini isiwe kama laini za simu yaani lipia kadri utumiavyo, kwa sasa startimes, azam, dstv, etc unalipia kama vile ni kodi ya mwezi, hata usipowasha tv mwezi mzima ulicholipia kimepotelea hewani. DHURUMA!!!
 
Wazo zuri saaaana, hebu anejua wahusika na kuandaa michakato ya kitaifa aliwasilishe wazo hili, ni zuri sana tena ongezeko la Tsh.25 tu wala siyo Tsh.50. Big up mtoa wazo, wewe ni mbunifu na muona mbali
 
Wananchi wengi wameanza kuelewa, lakini na walio bado gizani kujua nani analipa kodi bado ni wengi zaidi. Pote duniani mlipa kodi ni mlaji wa mwisho. Kupandisha bei ya petrol kufidia road licence utapata urahisi wa kukusanya kodi, lakini utavilipisha vyombo vingine vinavyotumia mafuta lakini havijui barabara, kama vile generator na boat za uvuvi na meli.

Neno 'road' lisipotoshe maana ya hoja nzuri iliyowasilishwa. Kutokana na manufaa nchi itakayopata jina la hii tozo linaweza kubadilishwa na kuitwa "Tozo kwa vyombo vinavyotumia mafuta" au jina lingine lolote kama itakavyoonekana inafaa. Tuache kukariri vitu
 
Mwaka 1997 wakati Jakaya anaianzisha Mamlaka ya mapato nadhani alikuwa na nia njema sana katika kukuza pato la taifa kupitia ukusanyaji wa kodi. Nina iman kubwa kabisa hata yeye alikuwa akisikitishwa na hawa jamaa kutegemea ulipwaji mkubwa wa kodi kutoka kwenye Sigara na Pombe. Mleta mada upo sawa kabisa pengine ningeenda mbali zaidi upande huo kwamba,
Sisi tunaojiajiri kungekuwa na mazingira rafiki ya hawa wakadiriaji kodi na wafanyabiashara wadogo sidhani kama kuna mtu angekwepa. Mtu umeanzisha biashara ndogo tu ila unataka itambulike kiutaratibu, pale kwa mkadiriaji anakukadiria kimazoea badala ya wao kutoka ofisini na kwenda eneo la biashara wakaangalie mazingira yalivyo ili ukadiriwe vizuri wao wanakukadiria watakavyo wao.
Jakaya alianzisha Mamlaka ya Mapato akiwa na Wadhifa gani 1997?
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!




hapo itabidi hadi magari yao yalipie road licence kwa mtindo huo..wakati wao wanaji exempt kulipia hiyo kitu
 
Una hakika? Waziri wa Fedha wa Mkapa alikuwa Prof Mbiinyi, Daniel Yona na Basil Mramba. JK alikuwa Mambo ya Nje miaka 10 yote!
 
Neno 'road' lisipotoshe maana ya hoja nzuri iliyowasilishwa. Kutokana na manufaa nchi itakayopata jina la hii tozo linaweza kubadilishwa na kuitwa "Tozo kwa vyombo vinavyotumia mafuta" au jina lingine lolote kama itakavyoonekana inafaa. Tuache kukariri vitu

Heshima kwako mkuu! Umefafanua vizuri, jina linafaa kabisa! "TOZO KWA VYOMBO VINAVYOTUMIA MAFUTA"
 
Wanauwezo wakusikia lakini akuna mtaalamu alie peleka wazo. Wote tunaangalia nitashiba vipi.

Kweli mkuu, baadhi ya watendaji wetu katika hizi ofisi ni janga kwa taifa. Sijui elimu yao inalisaidiaje taifa kuondokana na mifumo mibovu.
 
Wananchi wengi wameanza kuelewa, lakini na walio bado gizani kujua nani analipa kodi bado ni wengi zaidi. Pote duniani mlipa kodi ni mlaji wa mwisho. Kupandisha bei ya petrol kufidia road licence utapata urahisi wa kukusanya kodi, lakini utavilipisha vyombo vingine vinavyotumia mafuta lakini havijui barabara, kama vile generator na boat za uvuvi na meli.

Neno 'road' lisipotoshe maana ya hoja nzuri iliyowasilishwa. Kutokana na manufaa nchi itakayopata jina la hii tozo linaweza kubadilishwa na kuitwa "Tozo kwa vyombo vinavyotumia mafuta" au jina lingine lolote kama itakavyoonekana inafaa. Tuache kukariri vitu
 
Road licence ndio Vehicle Licence?? Kama ni ile inayolipiwa kwa mtandao na baadaye unaambiwa uende kwenye ofisi ya mkoa ya TRA kuchukua licence yenyewe na utoe kipande cha kubandika kwenye windscreen yagari mbona inaitwa Vehicle Licence? Hii Road Licence inalipiwa magari gani? Naibu Waziri wa Fedha mbona alifafanua vizuri sana kwa lugha ya Kiswahili kuwa ni kodi kwa kuwa na gari na sio kodi kwa kutumia barabara? Halafu mbona kwenye hiyo karatasi ya licence hakuna mahali palipoandikwa Road Licence? Na ndio maana ikipita mwaka unatakiwa kulipia na hutakiwi kupeleka gari traffic kuchekiwa. Ingekuwa Road Licence, ingekuwa LAZIMA gari likaguliwa na traffic police for road worthiness.
 
Back
Top Bottom