MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

Wakitaka kutenganisha wanaonunua kwa ajili ya jenereta watatengeneza mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi hiyo. Acha tu wenye jenereta watolewe kafara tu.
Haha mkuu umenifrahisha sana,kweli wenye majenereta watolewe kafara tu
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

Mkuu wazo ni zuri sana, lakini hiyo bei per lita naona umetaja kubwa sana. Sh. 50 kubwa ati, hebu fikiria hiyo dala dala ambayo kwa mwaka ingetumia lita 26,880 maana yake kwa mwaka huyu mwenye dala dala itabidi alipe sh 1,334,000 kama Road license kupitia mafuta.
50 kwa kuitamka hivi ni ndogo sana ila kiuhalisia ni kubwa sana. At least ingekuwa tozo kati ya sh 5/- na 10/-
 
Ahsante Mkuu, tuendelee kuipigania nchi yetu ili tupate maendeleo ya kweli. Hapa yupo tena dereva wa roli la cement kupeleka mikoani! Kampuni yao wana maroli zaidi ya 250

Kwa wiki yeye hufanya safari tatu. Mafuta anayopewa ni lita 900 kwa safari moja ya kwenda na kurudi. Kwa hiyo, kwa wiki hutumia lita 2,700 kwa safari tatu. Kwa mwezi lita 10,800. Kwa mwaka lita 129,600.

Sasa kama kodi yetu ingekuwa hiyohiyo shilingi 50 kwa lita. Huyu bwana na roli lake serikali ingevuna kodi ya shilingi 6,480,000/- kwa mwaka kama road license. Jamaa zetu, wasomi wetu na tai zao shingoni wamelala. Wanachoweza, kutoza kodi ya mtaji kwa akina mama na vijana wanaotaka kuanzisha vioski vya biashara. Wanashindwa kuweka mipango madhubuti ya kukusanya kodi kubwa ambayo haimuumizi mtoaji.
Sasa nyie hamuoni kama ni maumivu hayo?yaami ulipie road licence 6m halafu unadai ni pesa kidogo kwa kuwa tu unalipa 50 sh kwa lita ya mafuta?hesabu za biashara hakuna pesa nyingi wala kidogo kila shilingi ina matter tulipe hizo hozo 250 000 ila tutafite utaratibu kwa gari lisilo kuwepi barabarani lwa kipindi kirefu!
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Ni sawa tu, ndo uzalendo kwa nchi. Majenereta mengi hayalipi kodi ya uchafuzi wa mazingira, ndo utakuwa mchango wao huo! Ila wakubwa ndo wanazuia hili maana wao ndo wamiliki wa magari ya mizigo!!
 
Na tuna watu eti wanajiita wachumi lkn wameshindwa kabisa kuwa wabunifu kutafuta vyanzo mbadala vya mpato.
 
Railway Levy msingi wake ni kukusanya fedha kwa ajili ya kujenga mtandao wa Reli. Baada ya kuona kuwa nchi (nadhani pia na nchi nyingine za Afrika Mashariki) zinakosa uwezo wa kibajeti wa kujenga Reli mpya kwa kiwango cha standard gauge, ikaonekana kuwa tukiamua kama nchi kutoza Kodi kwa bidhaa zote zinazoingizwa kutoka nje kwa ajili ya jambo hili tunaweza kufikia lengo. Bahati mbaya nayoiona ni kwamba huenda kod hii haina specific account na hivyo mapato yake kujumuishwa katika mapato ya jumla.

Nilitaraji kusikia waziri wa fedha akitoa updates za mara kwa mara Bungeni juu ya Railway Levy kwa maana ya kiwango kilichokusanywa, changamoto au mafanikio ya ukusanyaji wake ili kubaini kama italeta matokeo yaliyokusidiwa au hapana. Na hii ingeweza kuleta projections. Kwa msingi huo, Railway levy yapaswa kuwa temporary levy ambayo inatakiwa ife tu ikiwa urefu wa kilomita zilizokusudiwa kujengwa na kodi hiyo zimekamilika, nikitumai kwamba Reli ikiwepo, uendelezaji na upanuaji wa line nyingine za reli zinapaswa kufadhiliwa na mapato yatoknyo na Reli hiyo. Tatizo kubwa la mfumo wetu wa kodi ni kutokuwa specific na pia kutofanya evalution ya kutosha kuzibaini kodi zinazohitaji reforms. Bahati mbaya wataalam wetu ni "robots" katika kila kitu.

Thank you DAN.
Well explained.
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

Mkuu, hata kama watatoza shilingi 20 kwenye huu mfano wako, bado watakusanya kiasi shillingi 537,700 kwa mwaka kwa hiyo daladala moja tu.

Najua kuna magari ya watu binafsi hawawezi kutumia kiasi hicho cha mafuta kwa siku. Lakini bado kuna malori yanatumia mafuta mengi zaidi. Kiasi hicho kinaweza kuwa wastani mzuri sana. Serikali kupitia EWURA, wanajua ni kiasi gani cha petroli na diseli kinatumiaka kwa mwaka mzima. Je wakizisha kwa sh 20 wanapata kiasi na walinganishe na hizo za Road Licence!
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

Bravo, bravo bravo

TRA na wanaohuska wengi wanafanya kazi kwa mazoea, kumfurahisha mtu fulani na wanataka hela za haraka haraka

mchango wako ni mzuri sana sana sana tu
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.

in tunr kun kodi za watu wa jenereta unazitoa unajua utawakamatia huku
 
Hapa ndio unaweza kujionea kuwa serikali wanakosea sana kuajiri watu kwa kigezo cha ufaulu na vyeti tu wanasahau inshu ya efficiency, productivity, na creativity......

Serikali wangeweka utaratibu wa kuasses uwezo wa waajiriwa wao na si kukaa na mambumbu yanayovaa suti na kujiita masomi wakati tuna watu kama huyu mleta mada ambaye ametoa wazo zuri sana na pengine likifanyiwa kazi likaleta tija kubwa sana na faida mara mbili kwa taifa.

Hebu ifike wakati na sisi raia tuwe wakali kwa serikali kwenye maswala kama haya ambayo yanaonyesha ni ukosefu tu wa akili za ubunifu.....hao mambumbumbu waliokalia nafasi na hawazitendei haki watolewe mara moja wapishe vijana wenye damu changa na moto wa mabadiliko watumike kuliletea taifa maendeleo......

Naungana mkono na mtoa mada na ameleta wazo zuri sana kwenye meza na hii italeta tija kubwa sana kwenye mapato ya serikali.
Mkuu, kweli hawa ni mbumbumbu wenye suti na tai shingoni! Hawana uzalendo na taifa lao. Wanaziona sheria kama misahafu ya dini, kwamba hauwezi kuzibadili.

Walichokaririshwa miaka kumi, kumi na tano iliyopita ndo hichohicho, hawaoni umuhimu wa kubadilisha kwa manufaa ya nchi yao. Aibu kubwa kuwa na watendaji ambao hawatumii nafasi walizopewa kuisaidia serikali kupata mapato ya kutosha ili iweze kuwahudumia wananchi.

Wanachokiweza, ni kung'ang'ana na mifumo kandamizi na isiyo rafiki kwa mlipa kodi. Kwao, mlipa kodi ni muhalifu anayepaswa kuadhibiwa, kwa sababu tu yeye ni mlipa kodi.

Hawako tayari kupokea wazo mbadala hata kama litakuwa na tija kwa taifa! Aibu kubwa kwa wasomi na wachumi wa kiwango hiki.

Mjadala huu unawahusu sana, mbona hatujaona msemaji wao akitupia hoja yake ili sote tuchangie. Safari bado ndefu, Mkuu wa kaya tusaidie!
 
Hii ni fikra ya ajabu kbs, wewe unadhani kila anayetumia petrol/diesel anagari? wengine wanabodaboda,wengine bajaji,wengine majenereta.

Na ukumbuke wenye vibaby walker wanalipa kidogo kuliko haya magari yetu. utawaonea buree wenye magari madogo

utakuwa ni unyonyaji shahiri dhahir kbs
Hv wewe umeelewa lakini hii mada au basi tu
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
akili nyingi hapa asee..
nenda kwa Mangi agiza bia nakuja kulipa
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

Kweli hawana upeo. Niliwahi kuandika hapa hayo mawazo yako. Pia nikaonana na meneja wa mkoa wangu akasema wamepeleka mapendekezo haya iki yaingie kwenye bajeti ya mwaka 2015 lkn kama unavyoona hata mwaka sidhani kama waziri wa fedha ameyaweka kwenye bajeti yake. Hazina wanazo takwimu za idadi ya magari yakiyoko nchini na yanaingia kila siku. Pia wanazo takwimu za mafuta yanayaingia kwa mwaka. Kuweka hizo tzs 50 kwa lita na kukokotoa ili kujua ni sh ngapi zitakusanywa kwa mwaka na kulinganisha na mapato ya sasa ya road licence inahitaji mtaalamu kutoka undp?
 
Wananchi wengi wameanza kuelewa, lakini na walio bado gizani kujua nani analipa kodi bado ni wengi zaidi. Pote duniani mlipa kodi ni mlaji wa mwisho. Kupandisha bei ya petrol kufidia road licence utapata urahisi wa kukusanya kodi, lakini utavilipisha vyombo vingine vinavyotumia mafuta lakini havijui barabara, kama vile generator na boat za uvuvi na meli.

Tunaangalia cost na benefit ya mfumo. Hiyo hoja yako ni dhaifu kwani generator na boti zinatumia kiasi kidogo sana cha mafuta ya diesel na petroli.
 
Kwa nini tunataka road license ihamishiwe kwenye mafuta na sio ifutwe kabisa?
 
Back
Top Bottom