MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
309
1,000
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

UPDATE UPDATE UPDATE!!

WANAJAMVI JAMAA KAMA WAMETUSIKIA!
Road License yafutwa, sasa kulipwa mara moja

Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na dizeli.
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,786
2,000
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!
Wazo zuri sana, lakini kwa Serikali hii sidhani kama watasikia
 
Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,903
2,000
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
 
Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,042

Wazo zuri. Ina maana kwa style hiyo, basi kubwa au lori,inaweza kufikisha 5M,kwa mwaka
 
Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
309
1,000
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Hapa ni kuweka mfumo mzuri wa usimamizi wakati wa kufanya manunuzi. Mfano, hizo mashine za EFD zinazotumika katika vituo vya mafuta zinaweza kutumika. Pia Tanesco wanaweza kutumia utaratibu wa wakufanya manunuzi yao. Lakini zaidi, watumiaji wa mafuta wengi ni wenye magari na kwa tozo ndogondogo itakuwa ahueni kwao.
 
Wakitaka kutenganisha wanaonunua kwa ajili ya jenereta watatengeneza mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi hiyo. Acha tu wenye jenereta watolewe kafara tu.
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,517
2,000
Hapa ndio unaweza kujionea kuwa serikali wanakosea sana kuajiri watu kwa kigezo cha ufaulu na vyeti tu wanasahau inshu ya efficiency, productivity, na creativity......

Serikali wangeweka utaratibu wa kuasses uwezo wa waajiriwa wao na si kukaa na mambumbu yanayovaa suti na kujiita masomi wakati tuna watu kama huyu mleta mada ambaye ametoa wazo zuri sana na pengine likifanyiwa kazi likaleta tija kubwa sana na faida mara mbili kwa taifa.

Hebu ifike wakati na sisi raia tuwe wakali kwa serikali kwenye maswala kama haya ambayo yanaonyesha ni ukosefu tu wa akili za ubunifu.....hao mambumbumbu waliokalia nafasi na hawazitendei haki watolewe mara moja wapishe vijana wenye damu changa na moto wa mabadiliko watumike kuliletea taifa maendeleo......

Naungana mkono na mtoa mada na ameleta wazo zuri sana kwenye meza na hii italeta tija kubwa sana kwenye mapato ya serikali.
 
kamwamu

JF-Expert Member
May 18, 2014
2,503
2,000
Wananchi wengi wameanza kuelewa, lakini na walio bado gizani kujua nani analipa kodi bado ni wengi zaidi. Pote duniani mlipa kodi ni mlaji wa mwisho. Kupandisha bei ya petrol kufidia road licence utapata urahisi wa kukusanya kodi, lakini utavilipisha vyombo vingine vinavyotumia mafuta lakini havijui barabara, kama vile generator na boat za uvuvi na meli.
 
Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,120
2,000
Ni ngumu. Hata ukichinga gari bado system inaendelea kusoma deni kwenye TIN yako. Utajikuta unadaiwa kwenye issue nyingine kwani TIN yako itakuumbua. Yamenikuta. Sijui kama kuna uwezekano wa kuomba TIN nyingine ili kukwepa madeni ya nyuma
 
bigcell

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
220
225
naunga mkono hoja, ila nijuavyo kuna ile tozo ya barabara ambayo imeingizwa kwenye petrol "Road Toll", sijui imekaaje hapo mana Serikali hii haieleweki kuna kitu kimejificha hapo. Wenye kujua hapo mnijuze.
 
Bila bila

JF-Expert Member
Dec 20, 2016
10,137
2,000
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Sooth imenichekesha hapo kwenye Garage licence.
 
Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
309
1,000
Hapa ndio unaweza kujionea kuwa serikali wanakosea sana kuajiri watu kwa kigezo cha ufaulu na vyeti tu wanasahau inshu ya efficiency, productivity, na creativity......

Serikali wangeweka utaratibu wa kuasses uwezo wa waajiriwa wao na si kukaa na mambumbu yanayovaa suti na kujiita masomi wakati tuna watu kama huyu mleta mada ambaye ametoa wazo zuri sana na pengine likifanyiwa kazi likaleta tija kubwa sana na faida mara mbili kwa taifa.

Hebu ifike wakati na sisi raia tuwe wakali kwa serikali kwenye maswala kama haya ambayo yanaonyesha ni ukosefu tu wa akili za ubunifu.....hao mambumbumbu waliokalia nafasi na hawazitendei haki watolewe mara moja wapishe vijana wenye damu changa na moto wa mabadiliko watumike kuliletea taifa maendeleo......

Naungana mkono na mtoa mada na ameleta wazo zuri sana kwenye meza na hii italeta tija kubwa sana kwenye mapato ya serikali.
Ahsante Mkuu, tuendelee kuipigania nchi yetu ili tupate maendeleo ya kweli. Hapa yupo tena dereva wa roli la cement kupeleka mikoani! Kampuni yao wana maroli zaidi ya 250

Kwa wiki yeye hufanya safari tatu. Mafuta anayopewa ni lita 900 kwa safari moja ya kwenda na kurudi. Kwa hiyo, kwa wiki hutumia lita 2,700 kwa safari tatu. Kwa mwezi lita 10,800. Kwa mwaka lita 129,600.

Sasa kama kodi yetu ingekuwa hiyohiyo shilingi 50 kwa lita. Huyu bwana na roli lake serikali ingevuna kodi ya shilingi 6,480,000/- kwa mwaka kama road license. Jamaa zetu, wasomi wetu na tai zao shingoni wamelala. Wanachoweza, kutoza kodi ya mtaji kwa akina mama na vijana wanaotaka kuanzisha vioski vya biashara. Wanashindwa kuweka mipango madhubuti ya kukusanya kodi kubwa ambayo haimuumizi mtoaji.
 
wehoodie

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
978
1,000
Kupandisha bei ya mafuta kuna madhara makubwa kiuchumi kuliko unavyodhani, hivyo sio njia sahihi kuingiza road licence kwenye mafuta. Mpaka sasa karibu asilimia 50 au zaidi ya bei ni kodi. Vile vile mafuta ni nishati ambayo inatumiwa na viwanda, majumbani na katika uzalishaji mwingine usiohisisha matumizi ya barabara, kwa msingi huo road licence lazima iendelee kuwapo na huu ni mfumo wa dunia nzima.
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,221
2,000
Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

Wale kamatakamata huwa wanashikishwa fedha ili magari yasipelekwe yadi, niliwahi kushuhudia hilo likifanyika, in other words ukiona mfumo fulani unang'ang'aniwa kiujanjaujanja ujue kuna watu wanaponea humo, hebu kumbuka miaka ya 1980+ vituo vya road toll vilineemesha watu

Usishangae hata hapa watakuja na hoja za kukupinga, watakwambia toa siku za mapumziko na service
 
miwani ya maisha

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
1,608
2,000
Tatizo nchi inaongozwa kwa Kiki.
Kuwe na utaratibu hata wateule wa Rais wawe angalao degree moja ili waweze kumshauri huyo Rais awaajiri watu wenye vipaji kama mleta mada hii
Kwa Nini Rais mwenye degree moja na kuendelea ateuwe darasa la saba kama akina Makonda??
 
Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,042
2,000
Wakitaka kutenganisha wanaonunua kwa ajili ya jenereta watatengeneza mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi hiyo. Acha tu wenye jenereta watolewe kafara tu.
Ni vyema nao watozwe. Hata hivyo,rate itakuwa kidogo sana kulingana na matumizi madogo ya mafuta. Pia itafidia madhara ya uharibifu wa mazingira kutokana na "greenhouse emission".
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom