MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

Hili jambo limeimbwa sana humu JF, na ndio ungekuwa utaratibu bora ambapo watozwa kodi wasingehisi mzigo na serikali isingepoteza mapato.
Naona jamaa wameamua kutia pamba masikioni au uwezo wao wa kufikiri ndio umegota.
Hili wazo lina mantiki sana, nimefikiria nimegundua tunatakiwa kulipia kadiri tunavyotumia. Kama umeme tu na hiyo road licence ilipwe kadiri mtu anavyotumia barabara. Mwingine gari yangu natumia weekend tu. Mwingine kila siku na masaa mengi gari lipo barabarani hivyo tunaharibu tofauti. Mfano gari ya kubeba cement Tanga -Dar dereva anatakiwa kufanya safari 18 kwa mwezi na mimi mwenye kubahatisha tenda mara 2 kwa mwezi wote tunalipa sawa wakati uharibifu na matumizi tofauti. Wazo zuri mleta mada.
 
Wakitaka kutenganisha wanaonunua kwa ajili ya jenereta watatengeneza mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi hiyo. Acha tu wenye jenereta watolewe kafara tu.

HATA HIVYO JENERETA HAZITUMIKI SANA KAMA MAGARI WAPIGWE TU
 
Wakitaka kutenganisha wanaonunua kwa ajili ya jenereta watatengeneza mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi hiyo. Acha tu wenye jenereta watolewe kafara tu.

Kabisa , mbona watumia mafuta ya taa walitolewa kafara wakati wa uchakachuwaji....
 
Mkuu mimi nimejiuliza swali hili zaidi ya mara elfu nikaja na uzi kama huu hapa ndani kwa mara ya kwanza
je hawa watu wanao husiana na kodi au mikakati ya utafuataji wa hela za taifa hili wanatumia akili kweli?
Je ni watu halisi ? Au wamepachikwa tu kwenye nafasi hizo..
inakera mno kushindwa kuwaza kwa mapana tumeshindwa na Nchi ndogo kama Malawi tu..
hebu fikiri mkuu.. ni magari Mangapi hayapiti njia kuu barabara za lami yako vijijini huko. Nani anahusika nayo kwenye RL.
gari ngapi zimelala ndani bado unajifanya unazidai RL.
nadhani hatuko serious na mambo yetu Nchi hii tuna maigizo Mengi sana badala ya kufanya kazi..
mwisho kama tutaacha mambo ya ushabiki wa kipumbavu wa kisiasa na kufanya kazi tunaweza kusonga
ni wakati sahihi kuikataa RL
Nimeipenda hii..."gari ngapi zimelala ndani unajifanya unazidai RL"

Mkuu, hao ndo wataalam wetu. Sijiu kama tutafikia malengo tuyatakayo! Hawana muda wa kuumiza vichwa vyao kufikiri, wao bora liende na vikodi kandamizi ambavyo havina tija kwa taifa bali usumbufu kwa raia wema.
 
Hili jambo limeimbwa sana humu JF, na ndio ungekuwa utaratibu bora ambapo watozwa kodi wasingehisi mzigo na serikali isingepoteza mapato.
Naona jamaa wameamua kutia pamba masikioni au uwezo wao wa kufikiri ndio umegota.
Uwezo wa kufikiri umegota. Wanaona ni kitu ambacho ambacho hakiwezekani.
 
Ni wazo zuri na kama nakumbuka vizuri, tulipitia huko miaka fulani nyuma. Ina maana kama tumepitia na hata tukaacha basi ipo sababu nzuri tu ya kufanya hivyo. Tunaposema kutoza sh 50 kwa lita ya diesel, jinsi gani tunaweza kumbana muuza mafuta kutupatia ile sh 50? Hapo ndipo palipo na matatizo, pakitokea mtu akanunua mafuta bila kudai risiti ya mauzo basi TRA wamepigwa la macho. Kwa mtazamo wangu wameridhika na hilo la bora tu wajichukulie hicho kidogo lakini wana uhakika nacho kuliko hilo kubwa litakaloishia mikononi mwa wenzetu wasio waaminifu.
Hilo nalo na risiti za malipo linaweza kuleta utata. Hata sasa ambapo vituo vinalazimika kuweka mashine za kodi, bado wanatoa risiti zenye utata
 
Hili wazo lina mantiki sana, nimefikiria nimegundua tunatakiwa kulipia kadiri tunavyotumia. Kama umeme tu na hiyo road licence ilipwe kadiri mtu anavyotumia barabara. Mwingine gari yangu natumia weekend tu. Mwingine kila siku na masaa mengi gari lipo barabarani hivyo tunaharibu tofauti. Mfano gari ya kubeba cement Tanga -Dar dereva anatakiwa kufanya safari 18 kwa mwezi na mimi mwenye kubahatisha tenda mara 2 kwa mwezi wote tunalipa sawa wakati uharibifu na matumizi tofauti. Wazo zuri mleta mada.
Exactly mkuu, pia ingekuwa na faida nyingine ya kuwafanya watu watumie hivi vyombo vya moto kwa nidhamu na kupunguza msongamano wa magari barabarani, kwa sasa tunalipa "kodi ya kumiliki gari" manake hata mantiki ya "Road" licence imepotea.
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.

Lazima lilipe kodi maaana lilipita wapi hadi kufika nyumbani? yaani kwenye mafuta ndo pahala sahihi kabisa
 
Hilo nalo na risiti za malipo linaweza kuleta utata. Hata sasa ambapo vituo vinalazimika kuweka mashine za kodi, bado wanatoa risiti zenye utata
Kwenye hizi mashine za kodi ndo wanapigwa ile mbaya. Hawataki kufungua macho, labda wanamasilahi!
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

UPDATE: Wabunge wataka Washehereshaji(MCs) na Wapiga picha waanze kutozwa kodi ili serikali iweze kukusanya mapato ya kutosha. Huku mbunge mwingine akiishauri serikali iwakate 10% ya kodi wamiliki na wapangaji wa nyumba kote nchini.

Huu ndio uwezo wa watendaji wetu kufikiri unapokomea! Hivi kuna washereheshaji wangapi kuweza kupata mapato tunayotarajia! Wapiga picha je! Nilipo hapa sijapiga picha miaka zaidi ya 25. Nyumba za kupanga je!

Gharama ya kuikusanya hii aina ya kodi ni kubwa kuliko mapato yenyewe. Mbona vyanzo tunaviona vingi tu tena vyenye kuliwezesha taifa kutimiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo!

USHAURI: WAHESHIMIWA WABUNGE, HUMU JF WAPO WATU WANAWEZA KUCHANGIA MAONI YAO HIVYO KUWAWEZESHA KUVIONA HIVYO VYANZO VYA MAPATO AMBAVYO NINYI MACHO YENU HAYAONI. TENA BURE BILA MALIPO. SOMENI NYUZI ZA JF MTAJIFUNZA MENGI SANA!
Mkuu, mimi sioni tatizo hapa kwenye Road Licence mpaka useme unaona bora ifutwe. Nadhani kikubwa ni 'awareness' iongezeke kwa walipaji kodi hawa. Unakuta mtu gari limepata matatizo analipaki bila kufata taratibu husika. Gharama tunazotozwa ni ndogo na reasonable tu.
 
Serikali si ilikuja na wazo wal kuweka kutoa risit kwenye sheli sijui lilishia wapi
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Lakini ni bora hivyo kuliko Majembe alivuo kuwa ana nyanyasa watu...
 
Kwakweli road license ilikuwa kichefuchefu. Nimefurahishwa zaidi na ule msamaha wa kodi. Though kwa waliolipa ni unfair ila ni bora.
 
IMG-20170608-WA0041.jpg
 
Kwakweli road license ilikuwa kichefuchefu. Nimefurahishwa zaidi na ule msamaha wa kodi. Though kwa waliolipa ni unfair ila ni bora.
Imefurahisha sana... Ilikuwa na unyanyasaji wa ajabu. Kina watu waliamua kuchinja magari yao kwa sababu ya malimbikizo.
Potelea mbali hata kama mimi nililipa jana ila imepunguza kero.
Kama sina hela ya mafuta napaki gari
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

UPDATE UPDATE UPDATE!!

WANAJAMVI JAMAA KAMA WAMETUSIKIA!
Road License yafutwa, sasa kulipwa mara moja

Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na dizeli.
Mtoa mada legeza ubongo kidogo
Swala la kodi lina create chain ndefu unachotakiwa kujiukiza tukilimbikiza kodi yote huko nn kitatokea??

Mfumuko wa bei hapa gharama za uzalishaji zitapanda viwandan kusababisha bei za bidhaa nazo kuongezeka coz unaelewa mashine zinahitaji mafuta ku-operate imagine

gharama ya unga nw ilivojuu kuongeza gharama za uzalishaji unatengeneza kitu gan??

Shifting of burden of tax payer hapa kuna watu wengne wataumia kwa niaba ya wenye hvo vyombo vya moto kwasababu kodi yao imeamishiwa kwenye mafuta so hata mama anaekanda chapati akinunua mafuta yenye hio kodi ilohamishiwa huku anakua amemlipia kodi yao ilohamishiwa huku

Sitoshngaa kuona wenye magar na boda boda wakifurahia hili coz kwao haina hasara tatzo kitakuja kwa wale maskin ambao tunaenda kuwapandishia gharana zao za maisha
 
Back
Top Bottom