MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

Wakitaka kutenganisha wanaonunua kwa ajili ya jenereta watatengeneza mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi hiyo. Acha tu wenye jenereta watolewe kafara tu.
Kimsingi wasitenganishe kati ya wanunuzi wa mafuta wenye magari, jenereta na mashine za kusaga. Kodi hiyo iwekwe kwenye mafuta yote, ili kama mtu ataamua kununua kwa ajili ya mashine ya dizeli ya kusaga basi alipe na anaenunua kwa ajili ya jenereta kama za minara ya simu alipe. Hapo kodi kubwa sana italipwa serikalini, kuliko kukimbizana na road license.
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
hoja nzuri sana mkuu lakini tozo hii sio lazima ibaki na jina 'road-license' ikitafutiwa neno rafiki italeta tija zaidi. zaidi ya hoja ya mleta mada kuna manufaa mapana sana kama tozo hii itaingizwa kwenye mafuta: vyombo vyoye hata vya nje ya nchi na magari mapya 'IT' yatachangia tozo hii. kuhusu jenereta na mitambo ya nyumbani haijalishi sana maana hata matumizi yao ya mafuta sio makubwa. pia kwenue LUKU tunalazimika kuchangia % kadhaa ewura na rea. inakusaidiaje wewe unayewasha umeme kwa ajili ya matumizi ya kawaida nyumbani?
 
Dereva wa lori kasema asikilizi abiria hadi lori litakapofika sasa
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.

hayo majenerata yako mangapi nchi hii? Ukilinganisha na idadi ya magari ni bora hiyo kitu ipelekwe kwa mafuta
 
Hata mimi naunga mkono, haina maana kutoza 'Road Licence' kwa gari ambayo iko garage-labda utoze 'Garage Licence'. Hata hivyo, wanaosema sio kila kitu kinachotumia Petroli/Diesel kinatumia barabara-hivyo wenye jenereta zinazosaidia wakati Tanesco wanapofanya yao wataathirika maana watatozwa kodi ya barabara wakati jenereta liko nyumbani.
Au tractor liko shambani
 
Wananchi wengi wameanza kuelewa, lakini na walio bado gizani kujua nani analipa kodi bado ni wengi zaidi. Pote duniani mlipa kodi ni mlaji wa mwisho. Kupandisha bei ya petrol kufidia road licence utapata urahisi wa kukusanya kodi, lakini utavilipisha vyombo vingine vinavyotumia mafuta lakini havijui barabara, kama vile generator na boat za uvuvi na meli.
Hao wanavyombo vyao, (marine & surface) sumatra inashughulika majini na nchi kavu. Nafikiri meli na boat zitakuwa zinalipa water liences
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!
Ni wazo zuri na kama nakumbuka vizuri, tulipitia huko miaka fulani nyuma. Ina maana kama tumepitia na hata tukaacha basi ipo sababu nzuri tu ya kufanya hivyo. Tunaposema kutoza sh 50 kwa lita ya diesel, jinsi gani tunaweza kumbana muuza mafuta kutupatia ile sh 50? Hapo ndipo palipo na matatizo, pakitokea mtu akanunua mafuta bila kudai risiti ya mauzo basi TRA wamepigwa la macho. Kwa mtazamo wangu wameridhika na hilo la bora tu wajichukulie hicho kidogo lakini wana uhakika nacho kuliko hilo kubwa litakaloishia mikononi mwa wenzetu wasio waaminifu.
 
Wazo lenye tija, big up. Japo presentation ya mtoa mada si nzuri.
 
Ni wazo zuri na kama nakumbuka vizuri, tulipitia huko miaka fulani nyuma. Ina maana kama tumepitia na hata tukaacha basi ipo sababu nzuri tu ya kufanya hivyo. Tunaposema kutoza sh 50 kwa lita ya diesel, jinsi gani tunaweza kumbana muuza mafuta kutupatia ile sh 50? Hapo ndipo palipo na matatizo, pakitokea mtu akanunua mafuta bila kudai risiti ya mauzo basi TRA wamepigwa la macho. Kwa mtazamo wangu wameridhika na hilo la bora tu wajichukulie hicho kidogo lakini wana uhakika nacho kuliko hilo kubwa litakaloishia mikononi mwa wenzetu wasio waaminifu.
Mkuu, ili kuzuia ukwepaji kwa walipa kodi kwa kuacha kuchukua risti au watoa huduma kushirikia na wateja wao kukwepa kulipa hii kodi, njia ipo! Tena ni rahisi sana kama wahusika watakuwa na nia ya dhati kuifanya serikali yetu ipate mapato ya kutosha. Kodi hii inabidi ikatwe pale kwenye mita yanapoingilia mafuta. Pale, serikali ipo hakuna atakaye kwepa. Sasa wauzaji huku kwenye vituo watauza mafuta ambayo tayari kodi ilishakatwa, hivyo wao wataiainisha katika rist za mauzo yao.

Mfano, Lita moja ya diesel shilingi 1920 + kodi shilingi 50 jumla 1970. Hii ndiyo mteja atalipia. Hapa mwenye kituo na mteja wake wote hawana ujanja wa kukwepa.
 
Ahsante Mkuu, tuendelee kuipigania nchi yetu ili tupate maendeleo ya kweli. Hapa yupo tena dereva wa roli la cement kupeleka mikoani! Kampuni yao wana maroli zaidi ya 250

Kwa wiki yeye hufanya safari tatu. Mafuta anayopewa ni lita 900 kwa safari moja ya kwenda na kurudi. Kwa hiyo, kwa wiki hutumia lita 2,700 kwa safari tatu. Kwa mwezi lita 10,800. Kwa mwaka lita 129,600.

Sasa kama kodi yetu ingekuwa hiyohiyo shilingi 50 kwa lita. Huyu bwana na roli lake serikali ingevuna kodi ya shilingi 6,480,000/- kwa mwaka kama road license. Jamaa zetu, wasomi wetu na tai zao shingoni wamelala. Wanachoweza, kutoza kodi ya mtaji kwa akina mama na vijana wanaotaka kuanzisha vioski vya biashara. Wanashindwa kuweka mipango madhubuti ya kukusanya kodi kubwa ambayo haimuumizi mtoaji.
6.5 Milion * malori 250=?
Kweli wasomi wetu wameenda shule kupata vyeti..
 
Nina imani msg zinasomwa humu ndani hao wanazozisoma wafikishe huu ujumbe bajeti ya kesho watoe kero ya wananchi hiyo Road licence na waweke kwenye mafuta itakuwa powa sana mungu ibariki Tanzania na viongozi wenye kuona kesho na kutoa kero za wananchi
 
Wakitaka kutenganisha wanaonunua kwa ajili ya jenereta watatengeneza mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi hiyo. Acha tu wenye jenereta watolewe kafara tu.
Generator inaweza fanyiwa "allowable deduction" wakati wa kufanya hesabu na "return" za kodi.
Kwa namna hiyo hakuna atakayeathirika kwa kodi isiyo halali.
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

UPDATE: Wabunge wataka Washehereshaji(MCs) na Wapiga picha waanze kutozwa kodi ili serikali iweze kukusanya mapato ya kutosha. Huku mbunge mwingine akiishauri serikali iwakate 10% ya kodi wamiliki na wapangaji wa nyumba kote nchini.

Huu ndio uwezo wa watendaji wetu kufikiri unapokomea! Hivi kuna washereheshaji wangapi kuweza kupata mapato tunayotarajia! Wapiga picha je! Nilipo hapa sijapiga picha miaka zaidi ya 25. Nyumba za kupanga je!

Gharama ya kuikusanya hii aina ya kodi ni kubwa kuliko mapato yenyewe. Mbona vyanzo tunaviona vingi tu tena vyenye kuliwezesha taifa kutimiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo!

USHAURI: WAHESHIMIWA WABUNGE, HUMU JF WAPO WATU WANAWEZA KUCHANGIA MAONI YAO HIVYO KUWAWEZESHA KUVIONA HIVYO VYANZO VYA MAPATO AMBAVYO NINYI MACHO YENU HAYAONI. TENA BURE BILA MALIPO. SOMENI NYUZI ZA JF MTAJIFUNZA MENGI SANA!
Mkuu mimi nimejiuliza swali hili zaidi ya mara elfu nikaja na uzi kama huu hapa ndani kwa mara ya kwanza
je hawa watu wanao husiana na kodi au mikakati ya utafuataji wa hela za taifa hili wanatumia akili kweli?
Je ni watu halisi ? Au wamepachikwa tu kwenye nafasi hizo..
inakera mno kushindwa kuwaza kwa mapana tumeshindwa na Nchi ndogo kama Malawi tu..
hebu fikiri mkuu.. ni magari Mangapi hayapiti njia kuu barabara za lami yako vijijini huko. Nani anahusika nayo kwenye RL.
gari ngapi zimelala ndani bado unajifanya unazidai RL.
nadhani hatuko serious na mambo yetu Nchi hii tuna maigizo Mengi sana badala ya kufanya kazi..
mwisho kama tutaacha mambo ya ushabiki wa kipumbavu wa kisiasa na kufanya kazi tunaweza kusonga
ni wakati sahihi kuikataa RL
 
Kuna mtu aliniambia "Ukiona mtu kajijenga,ujue na akili yake imejijenga". Nilimwuliza anitafsirie,akasema " Ukimchukia mtu mwenye nyumba nzuri,ati kaiba,ukampenda asiye nayo,ati siyo mwizi, yeye na wewe mkikaa pamoja hamtakaa mjenge nyumba".
 
Ni wazo zuri na kama nakumbuka vizuri, tulipitia huko miaka fulani nyuma. Ina maana kama tumepitia na hata tukaacha basi ipo sababu nzuri tu ya kufanya hivyo. Tunaposema kutoza sh 50 kwa lita ya diesel, jinsi gani tunaweza kumbana muuza mafuta kutupatia ile sh 50? Hapo ndipo palipo na matatizo, pakitokea mtu akanunua mafuta bila kudai risiti ya mauzo basi TRA wamepigwa la macho. Kwa mtazamo wangu wameridhika na hilo la bora tu wajichukulie hicho kidogo lakini wana uhakika nacho kuliko hilo kubwa litakaloishia mikononi mwa wenzetu wasio waaminifu.

Hiyo itayozwa bandarini kabla mafuta hayajauzwa na inaongezwa wakati wa kupanga bei na siyo vituoni.
 
Hili jambo limeimbwa sana humu JF, na ndio ungekuwa utaratibu bora ambapo watozwa kodi wasingehisi mzigo na serikali isingepoteza mapato.
Naona jamaa wameamua kutia pamba masikioni au uwezo wao wa kufikiri ndio umegota.
 
Back
Top Bottom