MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

MFANO HALISI: Road Licence inavyoikosesha serikali mapato

WISH GRANTED.

WATU WANALIA TU SASA.
 
Hilo ni wazo zuri sana na tena wala wasitoze sh.50 kwa lita hata wakifanya 20 tu watapata hela nyingi sana.
Wazo nzuri sana. Ongezeko la Shs 20 kwa lita hata hao wenye majenereta na matrekta ambayo hayatumii barabara wala hawatalalamika, at the same time serikali ikiwa inakusanya sh 600,000 kwa daladala, shs 300,000 kwa gari ndogo kama Vitz za matumizi binafsi na sh 2.5 million kwa magari kama mabasi na malori.

Tatizo ni kuwa sidhani kama wabunge wetu wataliona hili. Shs 50 kwa kila lita ya mafuta is too much. Hata ongezeko la sh 10 kwa lita lilikuwa linatosha sana na kuzidi kile TRA walichokuwa wanakipata kutokana na kodi ya motor vehicle licence.

TRA walijitetea kuwa hiyo motor vehicle licence si motor vehicle road licence bali ni ada ya kumiliki gari. Kama ni hivyo basi ni halali hata anayemiliki pikipiki, trekta, mashine ya kusaga unga au mashine nyingine yo yote inayotumia motor kulipa hiyo motor machine ownership fee/ licence kila mwaka. Lakini ni upunguani kumtoza mtu ambaye motor machine yake ni mbovu haiwaki, iko stoo tu ikisubiri uwezo wa kuitengeneza. Halafu mashine hiyo isiyofanya kazi unaitoza sawa na ila mpya inayochapa kazi na kuingiza kipato.

Hakika TRA yetu ni mburura katika kubuni kodi. Inahitajika kitengo cha wabunifu wa kodi ndani ya TRA chenye wataalamu stahiki, wenye kubuni wakishirikisha wadau mbali mbali, kwa scientific research za kitaifa na kimataifa.
 
Waseme Wanaongeza Kodi Kwenye Mafuta Na Wanafuta Road Licence, Full Stop. Wasilete Siasa Zczo Na Kchwa Wala Miguu, Kwan Mmeambiwa Hayo Mafuta Yanatumika Na Vyombo Vya Barabarani Tu?
 
Kama mimi ningelikuwa ndo mkuu wa hii kaya Tanzania ningelifuta "Road Licence" mara moja! Sababu, inaikosesha serikali mapato halali na makubwa.

Leo nimetembelea machinjio ya magari mabovu nikiwa na rafiki yangu akitafuta vipuri kwa ajili ya daladala lake. Nimekuta daladala nyingi zimechinjwa, na zinauzwa kama vipuri kwa wahitaji.

Nilivyojaribu kudadisi, wengi wanachinja baada ya kushindwa kulipia Road License kutokana na kulimbikiza kutokana na ajari au gari kiharibika hivyo kuchelewa kilitengeneza kwa wakati na hivyo kujikuta deni la road license kuwa kubwa.

Nimejaribu kuumiza kichwa kuona hivi kama hiyo road license kama ingetozwa kwenye mafuta pekeyake, serikali yetu ingepata kiasi gani. Hapa kuna dereva wa siku nyingi katika daladala anasema, hutumia wastani wa lita 80 za mafuta kila siku. Sasa hebu tukokotoe kidogo, lita 80 kwa siku, kwa wiki itakuwa lita 560, kwa mwezi lita 2,240, na kwa mwaka ni lita 26,880 za mafuta kwa daladala moja katika hali ya kawaida.

Sasa, kama watu wa hazina na TRA wangekuwa na upeo wa kuunga mkono serikali katika kuhakikisha inapata mapato ya kutosha, hili ndo pendekezo wangepeleka kwenye wizara husika. Lakini, wapi wapowapo kama vile hawakuenda shule.

Sasa, tufanye TRA wakusanye shilingi 50 tu kwenye kila lita moja ya mafuta. Utaona kuwa, daladala letu linalotumia lita 26,880 za mafuta kwa mwaka litakuwa limechangia kodi ya shilingi 1,344,000/- ambayo haiumizi kichwa kwa mchangiaji!

Huu ni mfano halisi jinsi TRA na mifumo yake ya ukusanyaji kodi unavyoigharimu hii nchi kwa kuikosesha mapato! Hawana hata upeo wa kupambanua ipi kubwa kati ya shillingi 250,000/- ya road license na shillingi 1,344,000/- kama itatozwa kwenye mafuta.

Swali la kujiuliza, kwanini kung'ang'ana na mfumo unaoikosesha serikali mapato!

Ninawasilisha hoja!

UPDATE UPDATE UPDATE!!

WANAJAMVI JAMAA KAMA WAMETUSIKIA!
Road License yafutwa, sasa kulipwa mara moja

Amesema uamuzi umechukuliwa ili ada hii ilipwe mara moja pale gari linaposajiliwa na baada ya hapo iendelee kulipwa katika ushuru wa bidhaa katika mafuta ya petroli na dizeli.
Uko sawa wengine wanalalamika hawajui.
 
Waseme Wanaongeza Kodi Kwenye Mafuta Na Wanafuta Road Licence, Full Stop. Wasilete Siasa Zczo Na Kchwa Wala Miguu, Kwan Mmeambiwa Hayo Mafuta Yanatumika Na Vyombo Vya Barabarani Tu?
acha kulalamika, huku kijini tulishazoea kununua lita kwa2700/= na hatuoni shida zaid ya sh 400 kabisa leo 50sh unalalamika? kuwa na uzalendo ww, kwan mtuwajeneleta hapaswi kulipa kodi? kwanzahata ushuru sokon kapunguziwa ,ngoma imebalance kabisaaaa
 
Daah! Uliyeandika huu uzi una akili sana. But majenereta na majiko ya mafuta ya taa je?
 
Hivi Tanzania hatuna mfumo wa Tax return kama nchi zingine.

Kurudishiwa kiasi cha kodi tunayolipa kila mwezi inapofika Mwisho wa mwaka kama asante kwa mlipa kodi na hasa ya kulipa kodi
 
Watanzania tunapotafuta unafuu, tusijaribu kukwepa ama kupunguza kodi, mara zote tulenge kuongeza pato la serikali, kwa huu ubunifu wa serikali wa kufuta motor vehicle licence iwe chachu ya kuongeza mapato na siyo kupunguza au kuanza kupiga hesabu eti tutalipa zaidi! Kila mtanzania awe tayari kulipa zaidi endapo utawekwa utaratibu husio na kero kama huu.
 
Watanzania tunapotafuta unafuu, tusijaribu kukwepa ama kupunguza kodi, mara zote tulenge kuongeza pato la serikali, kwa huu ubunifu wa serikali wa kufuta motor vehicle licence iwe chachu ya kuongeza mapato na siyo kupunguza au kuanza kupiga hesabu eti tutalipa zaidi! Kila mtanzania awe tayari kulipa zaidi endapo utawekwa utaratibu husio na kero kama huu.
Asante kwa mawazo chanya
 
Back
Top Bottom