Mfalme Zumaridi akamatwa na Polisi Mwanza

Mfalme Zumaridi akamatwa na Polisi Mwanza

Zaidi ya kupigia majirani kelele sioni kosa lake hapo.
Hilo kanisa anao usajili
Kujiita mungu ni hiari yake na siyo kosa
 
Halafu wanaomba msaada wa upelelezi..
Tumekosa utu tunapenda kuumizana tu raia wako ana makosa ukimwambia aje kila siku polisi tatizo lipo wapi kwa makosa ya kelele ndio ya kuwekana ndani na kutangazia Umma.
 
Huyo ni
Chizi flesh kama
Nabii Tito:
Wampeleke tu Milembe kumthibitisha:
Ni Mwendawazimu wa wazi kabisa:
Ni mgonjwa wa akili: 100%
 
View attachment 3334921

Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza linapenda kutoa taarifa kuwa leo tarehe 15.05.2025 majira ya saa nne asubuhi huko mtaa wa Buguku, kata ya Buhongwa, wilaya ya Nyamagana, limemkamata na linaendelea kumhoji Diana Edward Bundala ambaye pia hujitambulisha kwa jina la Mfalme Zumaridi, miaka 42, mkazi wa mtaa wa Buguku, kata ya Buhongwa, ambaye ameyageuza makazi yake kuwa kanisa, anatuhumiwa kuendesha shughuli za kidini bila usajili pamoja na kufanya mahubiri kwa waumini wake kwa sauti ya juu katika eneo hilo ambalo ni makazi ya watu na kusababisha usumbufu kwa majirani wanaoishi karibu na makazi yake.

Aidha, mwanamke huyo anahojiwa kuhusiana na taarifa inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii akionekana kwenye picha mjongeo akiwa na kundi la watoto wenye umri mdogo wa jinsia ya kike na kiume akiwaeleza kuwa yeye ndiye Mungu wao ambaye ana uwezo wa kuwatenganisha na kifo.

Uchunguzi kuhusiana na tukio hili unaendelea, Jeshi la polisi katika uchunguzi huo litashirikiana na taasisi nyingine za serikali; hivyo linawaomba wananchi wenye taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia uchunguzi wa tuhuma hizi wafikishe kwa Jeshi la polisi. Uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zinazostahili zitachukuliwa.


View attachment 3334876
huyu apelekwe mahakamani kwa kesi yeyote ya jinai, akifika pale utaratibu wa kijinai uchukue mkondo wa kupelekwa mental institution kwenda kupimwa akili, apelekwe isanga, wakileta jibu toka isanga, wampeleke mirembe akakae huko na machizi weee tuone kama akirudi mtaani atarudia uchafu wake huu.
 
kwa kelele hizo hyo n zaid ya kero hyo nyumba serikar wataifishe tu ikiwezakana japokua kuna makanisa yanakelele mtaani watu hatulali
 
Kwan walivyomkamata kwa mara ya kwanza wakati ule ikawaje akawashinda kesi. Na serikali inashindwaje kumdhibiti yule binti? Si wapoge utepe hilo eneo mwaka mzima.
Kipindi kile alifungiwa kanisa lake baada ya kuachiwa akahamishia kanisa nyumbani kwakwe.

Ila hoja ya kujiita yeye ni Mungu inafaa waje na uthibitisho hilo kuwa yeye sio mungu.
 
Hao watoto hawana wazazi mpaka wapotoshwe na mama huyo? Wana umri gani?
 
Back
Top Bottom