Mfalme Zumaridi aachiwa kwa dhamana, uchunguzi waendelea

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,369
Reaction score
18,684
Polisi mkoani Mwanza limemuachia kwa dhamana Diana Bundala maarufu ‘Mfalme Zumaridi’ huku uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili ukiendelea.

Zumaridi, ambaye alikamatwa kwa tuhuma za kugeuza makazi yake kuwa kanisa, kuendesha shughuli za kidini bila usajili, kuhubiri kwa sauti ya juu na kudaiwa kuaminisha watoto kuwa yeye ni mungu wao.

Soma, Pia: Mfalme Zumaridi akamatwa na Polisi Mwanza

1747495071192.png
Akizungumza na Mwananchi, leo Jumamosi Mei 17, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema Zumaridi alikidhi masharti ya kisheria ya dhamana, na hivyo ameachiwa ikiwa ni haki yake ya kisheria.

“Mtuhumiwa alipewa dhamana siku hiyo hiyo (Mei 15, 2025), tulipomkamata, ambayo ni haki yake kisheria. Uchunguzi bado unaendelea," amesema Mutafungwa.

Zumaridi, ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Buguku, Kata ya Buhongwa jijini Mwanza, alikamatwa Mei 15, 2025 kutokana na tuhuma za kuendesha shughuli za kidini kwa sauti ya juu, huku akidaiwa kusababisha usumbufu kwa wakazi wa eneo hilo.

Aidha, Zumaridi anadaiwa kuhubiri kwa watoto, akieleza kuwa yeye ni mungu wao na ana uwezo wa kuwaokoa na kifo, jambo ambalo lilijitokeza kupitia picha mjongeo zilizokuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii.
 
duh 。。。!
P
 
Polisi wamuonyenyeshe mungu wao

Ova
 
Back
Top Bottom