Mwaka 235 A.D kule Roma aliuwawa Kaisari aitwaye Severus Alexander. Aliuwawa kwa hila za majasusi wake waitwao The Praetorian Guard ambao walikuwa ndiyo kikosi cha ulinzi na ujasusi cha watawala wa Roma. Mtu ulikuwa huwezi kutawala Roma bila kutumia hichi kikosi.
Makaisari wa Roma walikuwa wanaheshimika kama miungu (Demi-gods), na hata kuwagusa ilikuwa ni sawa na kupingana na amri ya miungu. Utulivu na mafanikio ya dola la Roma, ulitegemea sana uimara wa kiti cha Kaisari. Makaisari wengi wa Roma kabla ya mwaka 235 A.D walikuwa ni lazima watokwe kwenye familia kubwa Roma (Roman Aristocracy) ambapo walifundishwa mambo ya utawala na siasa tangu wadogo.
Severus Alexander alivyoingia kwenye kiti alianza kufanya mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi, kisheria na kisiasa ambayo yaliifanikisha mno Roma ndani ya muda mfupi. Japo alikuwa na udhaifu mwingine mkubwa kwamba, alikuwa ni mtoto wa mama (Mama's Boy) ambaye hakuwa na uzoefu wowote wa vita. Hivyo alisoma mambo ya vita bila kwenda uwanja wa vita kama ilivyokuwa lazima kwa vijana wote wa Roma.
Hili tatizo ndilo lilimletea changamoto kwasababu alishindwa kusimamia nidhamu ya jeshi lake. Wanajeshi walikuwa wanafanya vitu vya hovyo lakini yeye kwakutokuwa na uelewa akawa anafanya nao mijadala tu. Watawala kabla yake walikuwa wanafahamu siasa za jeshi na waliweza kulidhibiti. Severus Alexander akiwa kijana mdogo alizidiwa na jeshi, kisha yeye na mama yake wakauwawa.
Baada ya kuuwawa, jeshi likamuweka madarakani askari mwenzao Maximius Thrax kama Kaisari mpya. Huyu hakuwa ametokea familia za watawala, na alikuwa hana elimu ambayo ingemsaidia kutawala. Katika utawala wake Roma ikaanza kuporomoka na ambapo kwa miaka 50 nchi haikuwa na mfalme anayeweza kumaliza muda bila kuuwawa na wanajeshi au majasusi. Hiki kipindi wanahistoria wanakiita The Third Century Crisis.
==================================================================
Kila nchi huwa na utaratibu wake wa kiutawala. Huo utaratibu ukivunjwa lazima madhara makubwa yawepo. Kwenye The Third Century Crisis walikuwepo watu zaidi ya 50 waliouwawa kwa kutaka kukalia kiti cha Kaisari ndani ya kipindi cha miaka 50. Kiufupi Roma ilikuwa imejaa vurugu kama utekaji, mauaji ya kutisha, vita, rushwa na dola kugawanyika.
==================================================================
IKO HIVI: Tokea mwaka 1961-2021, Tanzania imekuwa ikishikiliwa na kiti cha Uraisi. Raisi ni Baba, Raisi ni Mfalme, Raisi ni mungu-mtu, Raisi ni Jalala la lawama, Raisi ni alama ya umoja wa kitaifa na Raisi ni nguzo ya matumaini. Hii ndiyo Tanzania aliyoijenga Mzee Nyerere. Raisi anaweza akawa na madhaifu lakini tunamsitiri na kumstahi tukiwa na matumaini kwamba atamaliza muda wake halafu atakuja mwingine kurekebisha.
Ukweli mchungu ni kwamba miaka ya 1960's-1980's bara la Afrika liligubikwa na mapinduzi na muaji ya Maraisi. Mzee Nyerere alipona mara nyingi. Siyo kwamba alikuwa na nguvu, lakini watu wa ndani ya vyombo vya dola walikuwa wanamchukulia kama BABA YAO MZAZI. Wengi walijiuliza kwamba Mzee Nyerere akitoka nini kitafuata ???
Hata alipokuja Mzee Mwinyi ambaye Mzee Nyerere na kina Imran Kombe walimfanyia vimbwanga vingi kwasababu walikuwa hawamkubali, ukweli mchungu ulikuwa ni kwamba lazima amalize muda wake. Hili lilikuwa siyo suala la majadiliano bali mustakabali wa nchi.
Tatizo likaja mwaka 2005 alipoingia kaingia Cheki-Bobu Ikulu. Alivurunda mno nchi ikafika hadi kipindi wakafanya jaribio la kumleta Dikteta kurekebisha. Cheki-Bobu na udhaifu wake wote alivumiliwa na muda wake ukaisha. Mwaka 2015, aliingia Dikteta kwelikweli. Alifanya makubwa ndani ya muda mfupi huku akiacha vilio na maumivu mengi pia.
==================================================================
Bahati mbaya sana, wengi hawakumpenda na hawakumvumilia ambapo ilitakiwa mwaka 2025 awe anaondoka madarakani. Mbaya zaidi Tanzania kuna utamaduni wa pande mbili kupokezana miaka 10/10. Hivyo ni lazima Raisi amalize muda wake, mpende au msipende. Utamaduni huu ndiyo umeleta utulivu na amani kwa kipindi kirefu nchini.
Anaweza akaingia mvaa kobasi akasemwa sana, lakini hawezi kutolewa kwasababu lazima Raisi amalize muda wake. Kama hamumpendi msingepitisha jina lake kule NEC. Hivyo hata Wagalatia watasema na kutoa matamko, lakini hawafanyi jambo la kijinga kwasababu wanafahamu zamu yao itakuja.
Huu utaratibu unaweza kuonekana ni una ufedhuli mwingi lakini ndiyo ambao unafanya kazi kwa taifa changa kama letu (The Only Practical Method to Ensure Political Stability). Ni lazima mzani uwiane (Balance of Power), usipowiana ni lazima mtapata matatizo.
==================================================================
SHIDA INAANZA HAPA: Watu walio karibu na Raisi masaa 24/7/365 ni Majasusi na Wanajeshi. Hawa ndiyo humsaidia Raisi kutawala. Hapa Tanzania hili kundi tokea mwaka 1964 hadi 2021 lilijengwa kwa dhana kwamba Raisi hagusiki, hata iweje. Raisi ni mungu-mtu. Raisi ni Nchi. Raisi ni Baba. Hivyo kama kumdhuru subirini amalize muda wake ndiyo mtamgusa lakini mkimgusa akiwa madarakani mtayumbisha nchi nzima. Hili hata wale wenye falsafa tofauti ndani ya mfumo walikuwa wanakubaliana.
Baada ya mwaka 2021 utaratibu ulibadilika vibaya mno. MKUU WA NCHI aliguswa, kukawa na minong'ono, huku mahasimu wake wakajisifu hadharani kwamba "Sasa Bahari Iko Shwari" na kutamba kwa kejeli nyingi. Hakuna aliyewakeme. Miaka michache baadaye tunasikia minong'ono kwamba MKUU WA NCHI kweli alihujumiwa.
Ndiyo alikuwa Dikteta, Ndiyo alikosea mambo mengi tu. Lakini kwanini mlimpitisha mkifahamu tabia zake fika. Kwanini hamkusubiri amalize muda wake kama ambavyo mlimvumilia CHEKI-BOBU aliyekuwa anafanya mambo ya ajabu Ikulu yenye madhara makubwa kwa nchi ???
=================================================================
Tokea mwaka 2021 yametokea muaji makubwa ya kutisha kuwahi kutokea hapa Tanzania. Hayatakuwa mwisho kwasababu mzani wa madaraka haujakaa sawa. Mbaya zaidi imefahamika kwamba MKUU WA NCHI naye anagusika vizuri na haliwezi kutokea jambo lolote lile kubwa. Historia inaonesha kwamba mara nyingi mapinduzi makubwa, huzaa mapinduzi mengine. Nchi huchukua muda mrefu mno mpaka ije kutulia:
Mwaka 1651 waingereza walipindua mfalme wao na kumnyonga ila nchi ilikuja kutulia mwaka 1688 baada ya kuanzisha utaribu mpya wa kiutawala.
Mwaka 1789 wafaransa walipindu mfalme wao na miaka zaidi ya 30 nchi ilijaa damu na vita, ikaja kutulia mwaka 1814.
Mwaka 1776 makoloni 13 ya Marekani yaliasi dhidi ya Mfalme, na nchi ilikuja kutulia mwaka 1815 baada ya kumaliza ugomvi na Muingereza.
==================================================================
Hata hapa Afrika mchezo ni uleule tu:
RWANDA: walimfukuza Mfalme Kigeri ila mpaka leo kila utawala mpya umeingia kwa kumwaga damu. General Kayibanda, General Habyarimana na General Kagame, wote wameingia kwa bunduki. Ila makosa yalianza kule kwa Mfalme Kigeri.
UGANDA: walianza na kumtoa Mutesa. Akaja Obote akatolewa. Akaja Amini akatolewa. Akarudi Obote akatolewa. Sasa yuko Museveni naye akiondoka haijulikani Uganda itakuwa kwenye hali gani. Hakuna anayeweza kuvaa viatu vya Museveni.
ZIMBABWE: nako ni hivyo-hivyo tu. Mubage alitolewa akaingia Munangagwa.
NIGERIA: walau kipindi hiki wametulia na wanapokezana kimakabila na kidino
==================================================================
Tanzania na Kenya, MUNGU alitupendelea mno. Jinsi tulivyokuwa tunayaangalia madaraka (Approach Towards Leadership) mbali na madhaifu yetu mengi imakuwa ni kuvumiliana mno (Tolerance). Siyo kwamba sisi tuna kitu cha ziada kuliko wenzetu lakini tuna kiwango kikubwa cha kuvumiliana.
GHANA, South-Africa na Botswana ni mataifa ambayo yameanza kukomaa hapa Afrika linapokuja suala zima la kuvumiliana kisiasa. Sisi hapa Tanzania tunarudi miaka ya 60's kuishi maisha ambayo hatukuyaishi. Maisha ya machafuko (Political Instability). Kitakachotokea Tanzania kipindi hiki ni kwamba kiti cha Uraisi kitatingishwa mno kwa miaka mingi, hata huyu wa sasa akitoka.
Tumeshatengeneza BAD PRECEDENT, na kutulia mpaka pande zote ziumie na kupata hasara kubwa ndiyo tutarudi kuwa kawaida. Ila kwasababu NOBODY IS SAFE. Kiufupi hata uweke wanajeshi barabarani, muda wako utafika tu. Mlichokianzisha mwaka 2021 lazima mkinywee, tena mtakinywea vibaya sana.
Siasa ndivyo ilivyo, historia imejaa ushahidi wa hichi nachokisema kuanzia Rome, The Rashidun Caliphate, Mongol Empire, Tang Dynasty n.k Kumuua mfalme (Mzuri au Mbaya) na machafuko yasitokee huwa ni nadra mno.
====================================================