Mfahamu dereva aliyetumia saa 12 Dar - Songea miaka 90

Mfahamu dereva aliyetumia saa 12 Dar - Songea miaka 90

Naona jamaa alikuwa anakanyagia sana aisee. Naomba kuuliza pia barabara Dar to Songea ilikuwa lami full au?
Yes. Barabara ile ilijengwa na wajaa walikuwa wanaitwa BAFOBITI (spelling sina uhakika). Ilainza kujengwa mwaka 1980 na ikaisha 1985.
 
Hakuna kitu cha namna hiyo usidanganywe! Labda kama alikuwa anaendesha helkopta! Basi likiondoka Dar saa 12 asubuhi linaingia Njombe saa 12 jioni, na toka Njombe hadi Songea ni masaa matatu na nusu hadi manne. Unamdanganya nani wewe!
Wewe unazungumzia leo..!! Enzi hizo kuingia SOngea muda huo haikuwa ishu
 
Ni miaka ile ya 90. Ni Likungu Trans, ISUZU MV 118, TZK6150, Dar Njombe Songea. Dereva Selepion huyo wa Katikati na aliyeshika kiuno ni Juma Ndang'o.

Alisumbua sana njia ya Songea - Dar. Alishawahi kuingia Songea saa 12 kasoro jioni akitokea Dar, dereva, alikuwa ni Selepion.

Ilikuwa ni vigumu sana kuamini kama ISUZU inaweza kukimbia hivyo. Lakini Likungu ndiyo ilikuwa hivyo. Hatari sana, watu wa Songea hawawezi sahau hii gari.

View attachment 2327670
Mwenye mabasi haya aliamini ushirikina sana..!! Alilipeleka hilo basi kwao Paradiso kama unaelekea Lituhi kufanya tambiko...!! Lilifanyiwa huku likiwa na mnailoni yake kwenye siti
 
Miaka ya 2000 mwanzoni enzi hizo Marcopplo Andare Class ndio zinaingia.
Nilijisogesa zangu Msamvu pale nichukue gari kuelekea Dar. Nikawa nasubidi gari zinazotoka mikpani ilikua kama mida ya saa 11 hivi.
Mata ikaja Mohammed Trans ya Dodoma. Nikakata tiketi nikaingia ndani. Gari bado mpya siti zins nailoni bado kitu Andare Class.
Kidogo ikafika Sumry ya Tunduma ikiwa imeongozana na Hekima ya Tunduma. Hazikuchelewa zikatoka na sisi tukatoka hivyo tukawa tumeongozana gari tatu mbele Sumry ikifuata Hekima na Mohammed Trans nyums.
Aisee mashine zilikua zinatembezwa bampa tu bampa mpaka Mikese mizani. Baada ya kutoka hapo zilipigwa gia mpaka chalinze gari zote hazikusimana zikapita chalinze ikawa kuitafuta mlandizi.
Sasa kile kipande cha vigwaza mbele kulikua na Lorry, Sumry akapunguza spidi kdg, Hekima hakupunguza akaovertake Sumry na Lorry kwa pamoja na Mohammed Trans pia akapita Sumry na Lorry
Hapo Sumry ikabaki nyuma Hekima mbele.
Dah ile gari ilikua inatembea sio masikhara hili Polo psmoja na kuws ni jipya lakink halikuweza kuipita ile mashine mpk tunafika picha ya ndege Mohammed Trans ikaingua petrol station kujaza mafuta
Hekima nilikua naikubali sana. Zilitokaga pamoja na New force. Niliipanda around 2008 tokea Makambako

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Safina na zile Scania zake nyekundu aisee. Nissan Diesel (Saitama na Yokohama) zilikuwa ni special kwa njia ya Mbeya Sumbawanga
Scania zile nyekundu, moja iliitwa TAHFIFU VIDEO COACH....zilikuwa zinakamua kinoma...

Kuna moja Nyeupe nimesahau jina ila ubavuni iliiandikwa "COLD MIRINDA". Na hii pia ilikuwa inapiga haswa
 
Mbona huyo cha mtoto, kulikuwa na ligi ya masia express Tzj 3360 matema beach Tzj 7104 , Tawaqal Tzk110 etc , hizi zilikuwa zikikutana dae mnaingia saa nane mchana ,yani kipindi cha dj show ya radio one ya kina mike mhagama ndo kinaanza
Hood ye alikuwa ana game lake la kuingia saa kumi Tunduma ,
Mkwema bus Msm 34 , nayo ilikuwa inaingia Tunduma saa kumi jioni , ikitokea Dar.

Unanikumbuka Ilanga moto?
 
Ni miaka ile ya 90. Ni Likungu Trans, ISUZU MV 118, TZK6150, Dar Njombe Songea. Dereva Selepion huyo wa Katikati na aliyeshika kiuno ni Juma Ndang'o.

Alisumbua sana njia ya Songea - Dar. Alishawahi kuingia Songea saa 12 kasoro jioni akitokea Dar, dereva, alikuwa ni Selepion.

Ilikuwa ni vigumu sana kuamini kama ISUZU inaweza kukimbia hivyo. Lakini Likungu ndiyo ilikuwa hivyo. Hatari sana, watu wa Songea hawawezi sahau hii gari.

View attachment 2327670
...Nani alihesabu hayo Masaa? Isije ikawa Stori TU za Vijiweni!!
 
Yes mkuu hii Matema Beach Yes ilikua ni moto, pia kiswele route ya dar to songea hii bus nayo ilitamba sana, eti leo unatoka Dar saa 6am na unaingia tunduma 20:00hrs, si bora nipande baiskeli
...Haya, Panda Baskeli ifike Haraka zaidi !! [emoji57][emoji57]
 
Scania zile nyekundu, moja iliitwa TAHFIFU VIDEO COACH....zilikuwa zinakamua kinoma...

Kuna moja Nyeupe nimesahau jina ila ubavuni iliiandikwa "COLD MIRINDA". Na hii pia ilikuwa inapiga haswa
Cold milinda sumbawanga mby alikuwa anaingia saa 4 asubuhi

Sent from my Infinix X665B using JamiiForums mobile app
 
Yes. Barabara ile ilijengwa na wajaa walikuwa wanaitwa BAFOBITI (spelling sina uhakika). Ilainza kujengwa mwaka 1980 na ikaisha 1985.
Balfour Beatty.
 
Mimi niliwahi kupanda Masia kutoka mby-dar tukafika saa 9 chuma ilikua inakimbia balaa
 
Back
Top Bottom