Mtoa mada yupo sahihi.
Mimi ni mmoja wa walioshuhudia mabadiliko makubwa kwenye sekta ya usafiri na usafirishaji nchi hii.
Ni kweli hiyo Isuzu iliwahi kuweka rikodi hiyo, lakini bado haikufikia rikodi zilizowekwa na basi Chiku na Zainabu" maana zilikuwa zinapita Makambako saa saba kasoro mchana kutokea Dar.
Miaka hiyo basi ISUZU iliyoweka rikodi ya juu zaidi ni BAZUU (Da - Arusha - Namanga - Nairobi) na ilikuwa na mashabiki wengi hatari (Sauli ikasome), hebu fikiria, ilivyokuwa inatoka pale Stendi kuu Kisutu (kwa mabasi ya Kanda ya Kaskazini), mashabidi walikuwa wanafunga njia zingine zote ili chuma Bazuu ipite, mbwembwe zake sasa na mlalo wake, hatari tupu.
Kwa kuwa nimeshuhudia mabadiliko ya usafiri na usafirishaji ngoja niseme kidogo...
Ni kwamba, mabasi enzi hizo siyo kwamba yalikuwa yana uwezo wa kukimbia sana kama ya sasa, bali kuna sababu kadhaa zilizofanya mabasi hayo yawahi kufika yaendapo:-
1. Barabara hazikuwa na sehemu nyingi zenye kudhibiti mwendo kikomo 50kph.
Hivyo gari zikitoka stendi kuu za Mnazi mmoja, au Kisutu ama Kariakoo nk zilitembea mwendo hadi Mlandizi (hapa palikuwa ndiyo sehemu kuuu ya kula chakula), baada ya kutoka Mlandizi njia inafunguka na magari ku - maintain mwendo wa juu hadi waendako. Hii ilikuwa kwa safari za usiku.
Baada ya mabadiliko safari zilianza saa kumi na mbili asubuhi, ambapo nako gari zilikuwa zinafungukia Mlandizi na kuendelea.
Dar hadi Morogoro ilikuwa ni kwa saa mbili tu ama saa mbili na dakika chache.
Tz tulifeli kwa kutowazuia wananchi wasifuate barabara kuu na kujenga makazi, matokeo yake 50kph kila kilomita chache, huwa ina 'bore' sana.
(Zambia sehemu kubwa kwenye hili walifanikiwa)
2. Zamani hakukuwa na 'check point' za kizushi kama sasa, hivyo gari zikifunguka zimefunguka, hata kama ni kwa 100kph, lakini ni stendi hadi stendi hivyo kufanya yawahi kufika safari zao.
3. Zamani idadi ya magari barabarani ilikuwa chache, hapakuwa na hatari zilizopitiliza kama sasa, hivyo ilifanya mabasi yatembee mwendo mrefu bila kupunguza mwendo wakati wa kuovateki ama kupishana.
4. Zamani hapakuwa na hofu ya 'kupigwa tochi' au ya kukuta 'mahakama mbele baada ya kuvunja sheria za usalama barabarani, hivyo iliwafanya madereva 'wanyooshe mguu' kisawa sawa.
Hizo ni baadhi ya sababu zilizofanya zamani mabasi yawahi safari zao.
'Imagine' Scaba Scuba ilikuwa inaweza kufanya trip 3 kwa sita Dar - Moro kwa siku moja, leo hii sidhani kama kuna basi zinaweza hivyo ndani ya saa 14.
____
Tanzania tukiboresha barabara zetu na kundoa mwendo kikomo 50kph sehemu nyingi baada ya kuweka mazingira sawa na kuodoa matuta kero, mabasi yangeweza kwenda km 1000 kwa saa 12 bila kuwa na uhatari wowote wa mwendo kasi ulipitiliza.
__
#Tuzingatie sheria na kanuni za usalama barabarani ili kuepusha ajali.