Mfahamu dereva aliyetumia saa 12 Dar - Songea miaka 90

Mfahamu dereva aliyetumia saa 12 Dar - Songea miaka 90

Yes mkuu hii Matema Beach Yes ilikua ni moto, pia kiswele route ya dar to songea hii bus nayo ilitamba sana, eti leo unatoka Dar saa 6am na unaingia tunduma 20:00hrs, si bora nipande baiskeli
hahahaaaa
 
Na watu wanasifia sauli na dazu ya golden ati zinakimbia , huwa nachefuka sana
Adidas ya Tawfiq ilishwahi kukamatwa overspeed mpemba saa tisa alasiri , yani mwamba (almarhum mzee jamali )alikuwa nanaenda kuweka rekodi ya kuingia Tunduma saa tisa na robo
Hamna kitu hapo. Masia ilishawahi ingia Mbeya saa saba mchana Dereva akakamatwa na kuwekwa lock up
 
Hakuna kitu cha namna hiyo usidanganywe! Labda kama alikuwa anaendesha helkopta! Basi likiondoka Dar saa 12 asubuhi linaingia Njombe saa 12 jioni, na toka Njombe hadi Songea ni masaa matatu na nusu hadi manne. Unamdanganya nani wewe!
Wacha ww, Songea zamani kuingia saa kumi na moja ilikuwa kawaida sana, hapo mmetoka Dar saa kumi na mbili. Mind u kipimdi hicho hakukuwa na hizi tochi za 50, traffic wachache barabarani na magari hayakuwa mengi kama sasa, mizani ukipima Dar pale Ubungo mpka Makambako yaami njia ilikuwa ni nyeupe watu wanamwaga moto tu.
 
Giriki alikuwa anapiga fimbo Superstar Dar- Dom ile enzi ya kuondoka saa 2 usiku saa 9 yupo Msimbazi stand
Mbona lilikuwa linachelewa kiasi hiki, ulikuwa mkokoni huo maana mimi nilikuwa natoka na Scandinavia saa kumi na mbili asubuhi dodoma nafika Dar saa tano asubuhi
 
hayajapita masaa 24 toka Tanzanite Bus ichinje watu 10 Singida, ambao bado hawajazikwa wala kutolewa kwenye mabati ya basi, tushasahau, tuko hapa tunawajaza upepo madereva wanaokwenda kasi wazidi kushindana.....

vichwa panzi vya abiria wa dunia ya tatu.... Foolishness distilled...
Doh
Sasa hivi basi zote zipo under control ya Vts kutoka latra , hata hiyo Tanzanite ukienda kuangalia kwenye mkeka wa latra chances are utaikuta ilikuwa katika speed thresholds zao 85km/h
Ajali haziishi kwa sababu the elites wapo busy kutafuta visingiizio badala ya solutions, na wanancchi kwa either kutokujua au kwa ujinga wetu tunameza vitu kama vilivyo , giving them politician decent political millages kwa uzuzu wetu.

Tanzania ndio inaongoza kwa matuta barabarani, askari wa barabarani, zebra crossings and the likes yet bado ajali zinatuandama .
Basi inayotumia masaa 10 kusafiri km965 inakuwa imefanya average ya 96 km/h, south africa zambia namibia limit kwa basi ni 100km/h ,husikii ajali huko kwa wenzetu japo wanafanya speed kubwa kuliko sisi kwa sababu wenzetu wamewekeza kwenye miundombinu madhubuti
Anagongwa mtu barabarani na kufariki wasomi wanaona ni bora kuweka tuta kuliko under pass ambayo ingetatua tatizo forever bila shida.
watanzania hatujui vitu kwa undani wake badala ya tunamezeshwa matakataka na wanasiasa
 
Hakuna kitu cha namna hiyo usidanganywe! Labda kama alikuwa anaendesha helkopta! Basi likiondoka Dar saa 12 asubuhi linaingia Njombe saa 12 jioni, na toka Njombe hadi Songea ni masaa matatu na nusu hadi manne. Unamdanganya nani wewe!
Hujawahi kusafiri miaka hiyo ni bora ukae kimya , kwa miaka hiyo basi njombe zilikuwa zinaingia saa sita mchana
 
Okalla na Yoge wa Kiswele walikuwa wanatoka Dar saa 12 asubuhi na kufika Songea saa 11 jioni

Kadhalika John Africa na Mapunda wa Special couch

Sasa mchizi Rwambo wa Kiswele alikuwa anaingia saa 9:45
Lwambo marehemu umenikumbusha mbali sana... Alikuwa akiingia Morogoro msamvu watu wanalala zig zag anawakwepa wote halafu huyooo... Huku wanashangalia Rwambo Rwambo
 
wakuu samahan et dagaa w nyasa debe linauzwaje kwa sas huko songea?
 
Hakuna kitu cha namna hiyo usidanganywe! Labda kama alikuwa anaendesha helkopta! Basi likiondoka Dar saa 12 asubuhi linaingia Njombe saa 12 jioni, na toka Njombe hadi Songea ni masaa matatu na nusu hadi manne. Unamdanganya nani wewe!
Miaka ya 2012 hapa BUDGET ilikuwa inatoka Njombe saa 0600 inafika Ubungo saa 1530.
 
Miaka ya karibuni walioweza kidogo kuurudisha ule moto walikuwa Nganga, Happy Nation na Majinjah...

Wateja wakubwa walikuwa wafanyabiasha na madavoo wa IT, hapo raia wanawaishwa kuja kufunga mzigo K'koo kesho yake wageuze chap...

Nishawahi kupanda Happy Nation, toka Mbeya na ikafika Dar saa kumi kasoro jioni...(hii ni 2000 mwanzo hapo)...
SEMA wakati huo hamna folen Dar-kibaha
 
Okalla na Yoge wa Kiswele walikuwa wanatoka Dar saa 12 asubuhi na kufika Songea saa 11 jioni

Kadhalika John Africa na Mapunda wa Special couch

Sasa mchizi Rwambo wa Kiswele alikuwa anaingia saa 9:45
Nimegundua kitu. Huu uzi ni mzito sana kwa watoto wa 90's na wenzao wa 2000's.

Hivi huyo Okalla na hiyo miamba mingine iliyotajwa hapo iko wapi saivi?
 
Back
Top Bottom