Roller coaster
Senior Member
- Jan 5, 2015
- 194
- 129
Ukichimba shimo la kutumbukiza watu, chimba uongeze ukubwa kidogo sababu na wewe utatumbukia humo humo.Prophet Muhammad (SAW)
Kwenye huo uzi watu walimponda sana mtoa mada.Wacha maneno kijana pitia hapa uone madudu mengine ya Boss wako!
My little story with Makonda about leadership, kwa faida ya wasiokujua
Sasa kakosea wapi unapoleta suala LA madawa?Mateja mna haha kujificha kwenye hiki kichaka!
mtasema weee, mtakaa kimya
sasa kumbe una gubu lako la miaka na miaka
Mods do needful
Huyo jamaa anaishi kwa upambe na kujipwndekezaSasa nadhani ni wakati muafaka wa Lemutuz kutafuta ajira rasmi maana mirija yake yote inakatwa
Ukabila ndio kigezo mkuuKulikuwa na haja gani kuverify vyeti na kufukuza watu kumbe wapo watu wenye vyeti feki wamekaa offisini???? basi wote warudishwe kazini tuanze moja
Pumba tuDear
Daudi Albert Bashite.
Naanza na salamu na badala ya salamu ni kujua kama umeamka vizuri hapo kwako Masaki,na shemeji yetu naye natumaini ni mzima wa Afya.
Kwa uchache wa Muda naomba niende moja kwa moja kwenye dhumuni langu la kukuandikia ujumbe huu,hakika ujue sikupi pole sababu mambo Mengi umejitakia katika safari yako ya kisiasa,iliyo jaa vishindo na mbwembwe za kila aina.
Vijana wenzio tulibahatika kufanya kazi na wewe Daudi, kwakweli hatukuwahi kujua siri ya "kiburi" chako na "majivuno" yako uliyatoa wapi? Kwa jinsi ulivyokuwa kijana wa "Mission impossible" katika kila matendo ya vijana wa kaida yanayotarajiwa wewe ulitenda yale ambayo watu wasinge tarajia kuona,
Na hayo ndiyo yakawa maisha yako,hukujali wakubwa wanastahili heshima,hukujali kila binadamu anastahili staha,huku jali viongozi kama Mawaziri wa kuu au majaji wataafu walipaswa kulindwa na kuhifadhiwa.
Leo kabla Dunia haijaona mwanzo mpya au mwisho wa safari yako,kwakuwa Kwa namna yoyote vile tuta ulilokutana nalo Masihani mwako halitakuacha kama awali,utabadilika tuh utake usitake Hata kama mabadiliko yako yawe ya Nafasi au Nafsi yanakukuta kwa aibu na fedheha.
Walio karibu yako Daudi wanadai unawakati Mgumu,tukuombee,sitaki kuwa mnafki kwako,Daudi nikwambie tuh sitokuombea bali kabla ujamaliza kujutia Nafsi yako nikukumbushe tuh machache ili uyaingize kwenye sala ya toba.
1.Akilini kwako unamkumbuka baba wa watu? Mkurugenzi injinia mussa Natty,ulivyo muandama mpaka kusimamishwa kazi ulipokuwa DC KINONDONI? huku jali elimu yake aliyosomeshwa na wazazi wake masikini huko shinyanga,kwa UBASHITE WAKO ukamuumiza yeye na familia yake.
2.Je unawakumbuka wahandisi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni?,uliowasemea Mbele ya mheshimiwa Rais,siku ile Pale Biafra,wenzio wakasimamishwa kazi,na kuhamishiwa vijijini,hukujali elimu yao ya kweli si kama yako,waliyo ipata kwa shida wala familia zao masikini zilizo wategemea,Kwa UBASHITE WAKO ukawatokomeza na kuwaharibia majina na kazi zao.
3.Je unawakumbuka Maafisa ardhi? ukitoa amri wakamatwe kule Wazo mivumoni tuh kwa sababu walichelewa kufika eneo la tukio baada yako,hukujali Elimu zao na utaalamu wao wa ardhi waliosotea mashuleni na vyuoni ,kitichako kilikuwa na mamlaka ya kuwalaza wote sita mahabusu kituo cha mabatini KWA UBASHITE WAKO ukajiona wewe ni alpha na omega.
4.Je unamkumbuka yule dada Afisa ardhi uliye Muita "Tahira" kule kwenye mkutano wako mabwepande? Tena mbele za Tv na Radio zikiwa Mubashara,Hukujali mwenzio ana vyeti halali na amepimwa kwenye mitihani na amefaulu, KWA UBASHITE WAKO ukaona hakuna atakacho kufanya wala pakukimbilia.
5.Je unakumbuka ile kauli yako kwamba wewe ufanyalo Dar es salaaam,na kuliamua juu yake ni kwamba ameamua Mungu,Hata watu walipo toa miguno ya kulewa kwako madaraka hukuwahi kujutia kijivika utukufu wa Mungu,wala kujifananisha naye au kujipa unabii juu ya Dar es salaam,KWA UBASHITE WAKO ulidhani na yeye Mungu alipata zero? Au Mungu alinunua vyeti?
6.Je unaikumbuka ile kauli yako ya mara kwa mara uliyopenda kuitoa kwamba "Mimi nimbabe wa vita" ulimaanisha vita vya kufeli na kufanya "manuva" vita ya kutorudia au kukariri Darasa? Na ukazani umevishinda vita kwa kununua jina jipya, KWA UBASHITE WAKO,Ukasahau kuwa wazungu wanasema "There is no short cut in alife" isipokuwa wewe ukazani umeyapitia Denge maisha,wenzio wasome wafaulu,wewe ufeli ujekuwa boss wao.
7.Je unakumbuka Ile kauli yako ya kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam nzima inawafanyakazi 4,wengine wote ni mizigo? ,sasa utawaonea wivu hao mizigo kwakuwa wenzio wanavyeti na walifaulu wapo kihalali serikalini basi huenda utawaacha hapo na wewe mzigo namba moja utaondoka badala yao.KWA UBASHITE WAKO uliona kila mtu aliyesoma vigezo siyo kusoma ila ujanja kama uliotumia wewe.
Na mengine Mengi sababu ya Muda Nikuache na hayo,Niwache na boss wako muamue Mpangiane kazi gani nyingine,na kwa bahati mbaya mfumo wa nchi yetu,mwenye division zero,hastahili kuwa hata Dereva serikalini.
Fedheha na aibu imepanda gari lako la kifahari,imeingia ndani ya jumba lako hapo masaki,walinzi wote polisi na wanajeshi wameshindwa kuizuia,ipo mpaka sebuleni na sasa ujue Dar es salaam haitokubali itawaliwe na kuongozwa na KILAZA.......KUSOMA RAHA SANA
Na
BONIFACE JACOB
Senior councilor ubungo
Mstahiki meya
Manispaa ya ubungo
Vumbi likitulia utajua kuwa umempanda faras au umempanda punda.......homa yetu hapa ni chet cha form 4 we unaanza kutoa utetez wa kipuuz usiokuwa namashiko halaf watetea cheti cha form 6...SAKATA LA VYETI.
Yule Bwana nayedaiwa kwamba cheti chake ndio anatumia Makonda anaeleza.
“Paul Makonda nimemfahamu kupitia habari, na hata jina wanavyolitaja waliotunga taarifa ya mtandaoni wanakosea.... kwani mimi naitwa PAUL PIERRE CHRISTIAN KAGEZI, hatuna uhusiano na makonda, mimi Muhaya na yeye ni Msukuma.”
Kuna watu wanaoanisha majina pasipo kufanya utafiti wa kutosha, hawa wangeuliza kwanza kabla ya kutoa na kusambaza taarifa kwenye mitandao.
“Taarifa hizo (za kumpa cheti Makonda) si za kweli kwa sababu huwezi kutoa cheti wakati umepata daraja la kwanza kidato cha sita, utakwenda vipi chuo kikuu? Sasa niliwezaje mimi kwenda chuo kikuu halafu kwa wakati huo nimpe naye aende chuo kikuu kwa cheti hicho hicho?
katika kidato cha tano na sita nilichukua mchepuo wa sayansi masomo ya Fizikia, Kemia na Hesabu (PCM), hivyo si rahisi kutoa cheti hicho kwani ningeshindwa kumudu huko nilikokwenda.
Hivi kama Makonda hakufanya vema kidato cha nne au hakusoma kidato cha sita, akatumia cheti cha mtu mwingine, angeweza vipi kufanya vema katika mitihani yake ya chuo kikuu?
Watu wamekuwa wakipika na kuoanisha majina,....Kama wanataka kumpata huyo bwanamdogo (Makonda) kwa njia hiyo wamemkosa kwani kutumia cheti kimoja kwa vyuo viwili vya Serikali ni jambo lisilowezekana.... Makonda asingeweza kutumia cheti nilichokuwa nakitumia mimi.
“Sera ya Serikali ni kwamba unapata asilimia 100 ya mkopo, inakuwaje mtu huyo nimpe cheti changu wakati huo naye anakwenda chuo kikuu ambacho nacho ni cha Serikali?”
“Huyo bwana anajitegemea yeye kama yeye, na walichokifanya wao (waliosambaza taarifa mtandaoni) kwa makusudi yao bila shaka wana lengo lao, wao wametaka kuingiza hoja ambazo hazina mashiko.
“Cheti cha daraja la kwanza unauza kwa gharama gani? Nimesoma shule ya msingi na sekondari, (Makonda) alikuwa na fedha kiasi gani za kunipa ili nimuachie cheti? Inaweza kukuingia akilini kweli?.. hata hiyo namba ya Makonda sina".
Unataka kusema anatoa makapi badala ya mbegu?Shemeji naskia toka 2009 ndoa hadi Leo hamjabahatika kupata mtoto na Bashite?
HaswaaaaAnamkumbusha tu mkuu kuwa muosha huoshwa!
[emoji3] [emoji3] halikua na sifaMbona jina zuri sana, sijui kwanini aliliacha ''Daudi Albert Bashite.''
Mteule wa raisi asie na sifa?Muda mwingine mnajivua nguo na kuonesha ukilaaaza wenu kuliko hata huo wa Bashite. Uhalali wa kufanya kazi katika ofisi ya umma unamuhusu nini mteule wa Rais? Duh, jamani kweli uelewa mzuri. Pamoja na Pasco kuwapa elimu bado tuu? Kama hata utumishi wa umma haufahamu mambo mengine utayafahamu kweli wewe?
"unataka kukimbia na hauna brake what do you expect"
"vitu vingine havitakaga ujuaji utajikuta unawatandikia watu jamvi"
Ngoja nikasome tena#5 nimecheka sana hahahahahahahaa
Najua utarudi kuisoma baada ya kuona comment yangu hapa hahahahahaha bashite bwana