Meya Boniphace Jacob amfungukia RC Makonda

Kwa mashambulizi haya ya wazi kwa mheshimiwa Daudi Bashite naanza kuona hofu kuwa hii aibu anayoipata na kujikuta akitengwa na hata wale aliokuwa akiwaamini anaweza kufanya maamuzi kama yale aliyofanya chief Mkwawa alipoona karibu wajerumani watamshika.
Ni vema kuhakikisha kila alipo hakuna kamba.
 
Elimu ni nzuri sana, Gambo ni msomi ndiyo maana anaangalia pakutafutia kick. Anacheza michezo michafu ila kisomi.

Pole yako Bashite, kila siku nawaambieni humu Jf kua elimu ni kitu muhimu sana
 
Daudi or David in English means beloved " sasa kulikana na kuitwa Paulo matokeo yake ndio hayoo
 
Dear
Daudi Albert Bashite.

Naanza na salamu na badala ya salamu ni kujua kama umeamka vizuri hapo kwako Masaki,na shemeji yetu naye natumaini ni mzima wa Afya.

Kwa uchache wa Muda naomba niende moja kwa moja kwenye dhumuni langu la kukuandikia ujumbe huu,hakika ujue sikupi pole sababu mambo Mengi umejitakia katika safari yako ya kisiasa,iliyo jaa vishindo na mbwembwe za kila aina.

Vijana wenzio tulibahatika kufanya kazi na wewe Daudi, kwakweli hatukuwahi kujua siri ya "kiburi" chako na "majivuno" yako uliyatoa wapi? Kwa jinsi ulivyokuwa kijana wa "Mission impossible" katika kila matendo ya vijana wa kaida yanayotarajiwa wewe ulitenda yale ambayo watu wasinge tarajia kuona,

Na hayo ndiyo yakawa maisha yako,hukujali wakubwa wanastahili heshima,hukujali kila binadamu anastahili staha,huku jali viongozi kama Mawaziri wa kuu au majaji wataafu walipaswa kulindwa na kuhifadhiwa.

Leo kabla Dunia haijaona mwanzo mpya au mwisho wa safari yako,kwakuwa Kwa namna yoyote vile tuta ulilokutana nalo Masihani mwako halitakuacha kama awali,utabadilika tuh utake usitake Hata kama mabadiliko yako yawe ya Nafasi au Nafsi yanakukuta kwa aibu na fedheha.

Walio karibu yako Daudi wanadai unawakati Mgumu,tukuombee,sitaki kuwa mnafki kwako,Daudi nikwambie tuh sitokuombea bali kabla ujamaliza kujutia Nafsi yako nikukumbushe tuh machache ili uyaingize kwenye sala ya toba.

1.Akilini kwako unamkumbuka baba wa watu? Mkurugenzi injinia mussa Natty,ulivyo muandama mpaka kusimamishwa kazi ulipokuwa DC KINONDONI? huku jali elimu yake aliyosomeshwa na wazazi wake masikini huko shinyanga,kwa UBASHITE WAKO ukamuumiza yeye na familia yake.

2.Je unawakumbuka wahandisi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni?,uliowasemea Mbele ya mheshimiwa Rais,siku ile Pale Biafra,wenzio wakasimamishwa kazi,na kuhamishiwa vijijini,hukujali elimu yao ya kweli si kama yako,waliyo ipata kwa shida wala familia zao masikini zilizo wategemea,Kwa UBASHITE WAKO ukawatokomeza na kuwaharibia majina na kazi zao.

3.Je unawakumbuka Maafisa ardhi? ukitoa amri wakamatwe kule Wazo mivumoni tuh kwa sababu walichelewa kufika eneo la tukio baada yako,hukujali Elimu zao na utaalamu wao wa ardhi waliosotea mashuleni na vyuoni ,kitichako kilikuwa na mamlaka ya kuwalaza wote sita mahabusu kituo cha mabatini KWA UBASHITE WAKO ukajiona wewe ni alpha na omega.

4.Je unamkumbuka yule dada Afisa ardhi uliye Muita "Tahira" kule kwenye mkutano wako mabwepande? Tena mbele za Tv na Radio zikiwa Mubashara,Hukujali mwenzio ana vyeti halali na amepimwa kwenye mitihani na amefaulu, KWA UBASHITE WAKO ukaona hakuna atakacho kufanya wala pakukimbilia.

5.Je unakumbuka ile kauli yako kwamba wewe ufanyalo Dar es salaaam,na kuliamua juu yake ni kwamba ameamua Mungu,Hata watu walipo toa miguno ya kulewa kwako madaraka hukuwahi kujutia kijivika utukufu wa Mungu,wala kujifananisha naye au kujipa unabii juu ya Dar es salaam,KWA UBASHITE WAKO ulidhani na yeye Mungu alipata zero? Au Mungu alinunua vyeti?

6.Je unaikumbuka ile kauli yako ya mara kwa mara uliyopenda kuitoa kwamba "Mimi nimbabe wa vita" ulimaanisha vita vya kufeli na kufanya "manuva" vita ya kutorudia au kukariri Darasa? Na ukazani umevishinda vita kwa kununua jina jipya, KWA UBASHITE WAKO,Ukasahau kuwa wazungu wanasema "There is no short cut in alife" isipokuwa wewe ukazani umeyapitia Denge maisha,wenzio wasome wafaulu,wewe ufeli ujekuwa boss wao.

7.Je unakumbuka Ile kauli yako ya kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam nzima inawafanyakazi 4,wengine wote ni mizigo? ,sasa utawaonea wivu hao mizigo kwakuwa wenzio wanavyeti na walifaulu wapo kihalali serikalini basi huenda utawaacha hapo na wewe mzigo namba moja utaondoka badala yao.KWA UBASHITE WAKO uliona kila mtu aliyesoma vigezo siyo kusoma ila ujanja kama uliotumia wewe.

Na mengine Mengi sababu ya Muda Nikuache na hayo,Niwache na boss wako muamue Mpangiane kazi gani nyingine,na kwa bahati mbaya mfumo wa nchi yetu,mwenye division zero,hastahili kuwa hata Dereva serikalini.

Fedheha na aibu imepanda gari lako la kifahari,imeingia ndani ya jumba lako hapo masaki,walinzi wote polisi na wanajeshi wameshindwa kuizuia,ipo mpaka sebuleni na sasa ujue Dar es salaam haitokubali itawaliwe na kuongozwa na KILAZA.......KUSOMA RAHA SANA

Na
BONIFACE JACOB
Senior councilor ubungo
Mstahiki meya
Manispaa ya ubungo
Kwel kusoma raha sanaa
 
Bashite anajiona mungu mungu Wa Dar..fitina na majungu na uchonganishi wake .ndio unaomponza .
Zamu yako kuaibika bashite
 
uko sahihi sana mkuu

ila yule dada, yule paul mayenga wangeonekana na kuhojiwa hauoni haina haja hata ya kupiga kelele?

system haiwezi kujidhalilisha mkuu, unless haujui mkuu wa mkoa anapatikana vipi
haya tueleze wewe mkuu wa mkoa anapatikana kwa style gani

umewahi kusikia hata interview ya kazi ya mkuu wa mkoa au wilaya?
 
Mbona ya mbowe hamsemi ? Mti wenye matunda ndio hupigwa mawe makonda piga kazi achana namaneno yawakosaji
Makonda yupi unamwambia apige kazi? yule mtangazaji wa Radio kule Tabora? Mbona Radio yao haisikiki hata Igunga?
 
Nchi inapata aibu Kubwa taasisi iliyokupa wadhifa nayo inapata aibu Kubwa mno.

Jiji zima linanuka aibu hii hamna pa kujificha na hii aibu ,wizara ya Elimu inaona aibu hii ,vyuo alivyosona pia vinapata aibu hii kwa kushindwa kuling'amua.

Aibu aibu aibu.

Kama kweli ikidhibitika ni aibuuuuuuuuuuuuuu
 
Dear
Daudi Albert Bashite.

Naanza na salamu na badala ya salamu ni kujua kama umeamka vizuri hapo kwako Masaki,na shemeji yetu naye natumaini ni mzima wa Afya.

Kwa uchache wa Muda naomba niende moja kwa moja kwenye dhumuni langu la kukuandikia ujumbe huu,hakika ujue sikupi pole sababu mambo Mengi umejitakia katika safari yako ya kisiasa,iliyo jaa vishindo na mbwembwe za kila aina.

Vijana wenzio tulibahatika kufanya kazi na wewe Daudi, kwakweli hatukuwahi kujua siri ya "kiburi" chako na "majivuno" yako uliyatoa wapi? Kwa jinsi ulivyokuwa kijana wa "Mission impossible" katika kila matendo ya vijana wa kaida yanayotarajiwa wewe ulitenda yale ambayo watu wasinge tarajia kuona,

Na hayo ndiyo yakawa maisha yako,hukujali wakubwa wanastahili heshima,hukujali kila binadamu anastahili staha,huku jali viongozi kama Mawaziri wa kuu au majaji wataafu walipaswa kulindwa na kuhifadhiwa.

Leo kabla Dunia haijaona mwanzo mpya au mwisho wa safari yako,kwakuwa Kwa namna yoyote vile tuta ulilokutana nalo Masihani mwako halitakuacha kama awali,utabadilika tuh utake usitake Hata kama mabadiliko yako yawe ya Nafasi au Nafsi yanakukuta kwa aibu na fedheha.

Walio karibu yako Daudi wanadai unawakati Mgumu,tukuombee,sitaki kuwa mnafki kwako,Daudi nikwambie tuh sitokuombea bali kabla ujamaliza kujutia Nafsi yako nikukumbushe tuh machache ili uyaingize kwenye sala ya toba.

1.Akilini kwako unamkumbuka baba wa watu? Mkurugenzi injinia mussa Natty,ulivyo muandama mpaka kusimamishwa kazi ulipokuwa DC KINONDONI? huku jali elimu yake aliyosomeshwa na wazazi wake masikini huko shinyanga,kwa UBASHITE WAKO ukamuumiza yeye na familia yake.

2.Je unawakumbuka wahandisi wa Halmashauri ya manispaa ya Kinondoni?,uliowasemea Mbele ya mheshimiwa Rais,siku ile Pale Biafra,wenzio wakasimamishwa kazi,na kuhamishiwa vijijini,hukujali elimu yao ya kweli si kama yako,waliyo ipata kwa shida wala familia zao masikini zilizo wategemea,Kwa UBASHITE WAKO ukawatokomeza na kuwaharibia majina na kazi zao.

3.Je unawakumbuka Maafisa ardhi? ukitoa amri wakamatwe kule Wazo mivumoni tuh kwa sababu walichelewa kufika eneo la tukio baada yako,hukujali Elimu zao na utaalamu wao wa ardhi waliosotea mashuleni na vyuoni ,kitichako kilikuwa na mamlaka ya kuwalaza wote sita mahabusu kituo cha mabatini KWA UBASHITE WAKO ukajiona wewe ni alpha na omega.

4.Je unamkumbuka yule dada Afisa ardhi uliye Muita "Tahira" kule kwenye mkutano wako mabwepande? Tena mbele za Tv na Radio zikiwa Mubashara,Hukujali mwenzio ana vyeti halali na amepimwa kwenye mitihani na amefaulu, KWA UBASHITE WAKO ukaona hakuna atakacho kufanya wala pakukimbilia.

5.Je unakumbuka ile kauli yako kwamba wewe ufanyalo Dar es salaaam,na kuliamua juu yake ni kwamba ameamua Mungu,Hata watu walipo toa miguno ya kulewa kwako madaraka hukuwahi kujutia kijivika utukufu wa Mungu,wala kujifananisha naye au kujipa unabii juu ya Dar es salaam,KWA UBASHITE WAKO ulidhani na yeye Mungu alipata zero? Au Mungu alinunua vyeti?

6.Je unaikumbuka ile kauli yako ya mara kwa mara uliyopenda kuitoa kwamba "Mimi nimbabe wa vita" ulimaanisha vita vya kufeli na kufanya "manuva" vita ya kutorudia au kukariri Darasa? Na ukazani umevishinda vita kwa kununua jina jipya, KWA UBASHITE WAKO,Ukasahau kuwa wazungu wanasema "There is no short cut in alife" isipokuwa wewe ukazani umeyapitia Denge maisha,wenzio wasome wafaulu,wewe ufeli ujekuwa boss wao.

7.Je unakumbuka Ile kauli yako ya kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam nzima inawafanyakazi 4,wengine wote ni mizigo? ,sasa utawaonea wivu hao mizigo kwakuwa wenzio wanavyeti na walifaulu wapo kihalali serikalini basi huenda utawaacha hapo na wewe mzigo namba moja utaondoka badala yao.KWA UBASHITE WAKO uliona kila mtu aliyesoma vigezo siyo kusoma ila ujanja kama uliotumia wewe.

Na mengine Mengi sababu ya Muda Nikuache na hayo,Niwache na boss wako muamue Mpangiane kazi gani nyingine,na kwa bahati mbaya mfumo wa nchi yetu,mwenye division zero,hastahili kuwa hata Dereva serikalini.

Fedheha na aibu imepanda gari lako la kifahari,imeingia ndani ya jumba lako hapo masaki,walinzi wote polisi na wanajeshi wameshindwa kuizuia,ipo mpaka sebuleni na sasa ujue Dar es salaam haitokubali itawaliwe na kuongozwa na KILAZA.......KUSOMA RAHA SANA

Na
BONIFACE JACOB
Senior councilor ubungo
Mstahiki meya
Manispaa ya ubungo
Kama mlikuwa na stock Kubwa ya huo UNGA wenu mtajua pa kuupeleka,,
Makonda mtamsakama kwa Vyeti lakini mkumbuke Rais alimteua kutokana na utendaji wake wa Kazi mzr.
Kwani hivyo Vyeti vikuwa muhimu San sasa hivi baada ya MAKONDA kuvalia njuga UNGA wenu mlikuwa wapi SK zote kuhoji?

SASA HIVI HATA ANGEKUWA HANA CHETI CHOCHOTE WANANCHI TUMESHARIDHIKA NA UTENDAJI WAKE WA KAZI ACHEZI KIJANA APIGE KAZI.

Eti Vyeti nyie mlionavyo mmefanya nn kulisaidia hili taifa,, Makonda Asiye na Vyeti kaokoa vijana wengi mliowahaliribu kwa UNGA wenu.
Tumechoka na lawama zenu kuhusiana na Vyeti vya Makonda,, kama biashara ya UNGA imebuma basi jaribuni ingine.
 
Mateja mna haha kujificha kwenye hiki kichaka!

mtasema weee, mtakaa kimya

sasa kumbe una gubu lako la miaka na miaka

Mods do needful
tuseme ukweli, kusoma na kupata cheti halali ni raha sana, utalala usingizi mzuri. mtaongea kusingizia kuwa uteja sijui ni nini? mbona wanaopiga vita madawa wengi lakini yeye tu ndio anaandamwa? kumbuka hili, na litaenda kutokea muda si mrefu. Tabia ya Mungu aliyekuumba hata wewe ni kwamba ambeapa kuwashusha chini watu wenye kiburi. ajishushaye atakwezwa, ajikwezaye atashushwa, Neno la Mungu lina sema unyenyekevu tujivike, Mungu huwapiga wenye kiburi lakini huwapa wanyenyekevu neema. Nebukadraza alikuwa na kiburi kama cha Daudi bashite, alipelekwa porini akawa anaishi kwa kula nyasi kama ng'ombe hadi alipojishusha mbele za Mungu. umekuwa nakiburi sana, hakuna asiyejua hilo, na binafsi huwa siamini kama ndivyo ulivyolelewa au ulikipata ukubwani baada ya kuingia kwenye mashetani ya userikalini(tunajua huwa mnapelekwa kwa waganga na wasoma nyota) wakati maskini uliuwa umezoea kuwa mhubiri mzuri mtoto wewe. Mungu akuhurumie, umrudie Mungu, ujue dunia na vyote vinapita. mbona mwenzio nape hayuko kama wewe na mlitoka pamoja, mmepiga wote magitaa kanisani ndugu yangu...mwogope Mungu.
 
Tukikumbushe Bashire alivo panga nuku 10 kudhalilisha watu
 
Kama kweli Boni ameandika haya basi kumbe kijana bado, bado hajaiva kabisaaaa. Meya wa ubungo hakutakiwa kuingia katika siasa za namna hii. Duh, sijui, sijui labda kama hakuna maelekezo ya namna ya kuishi na kutenda ukiwa na wadhifa ndani ya chama.
wana siasa wetu wana fanana wote.
 
Back
Top Bottom