TAJIRI MKUU WA MATAJIRI
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,980
- 22,032
Barua kutoka kwa Maaskofu
UJUMBE WA ASKOFU KWA DR. NCHIMBI JUU YA USALAMA WAKE!
Mpendwa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi!
Pokea salaam kutoka kwetu sisi tulio Askofu.
Tunatambua kuwa wakati huu unapitia katika kipindi kigumu sana katika historia ya maisha yako ya kisiasa na utumishi wa umma.
Tumefuatilia sana mjadala ulio nyuma ya kile kilichoitwa 'kujiuzulu' kwako tumebaini ya kuwa watu wengi sana hawajadili juu ya haki zako za msingi. Watu wengi hawajui ya kuwa unaweza kuwa unapita kipindi kigumu cha kufinywa haki zako ambazo ni haki ya kujumuika (freedom of association) uhuru wa kutembea (freedom of movement), haki ya kutoa maoni (freedom of expression), haki ya kusikilizwa (natural justice) na haki ya kuishi ni haki zako za msingi ambazo sisi tutazipigania.
Ni wazi kuwa hiki ndicho kipindi ambacho watu ambao ni marafiki wako wa dhati watasimama pamoja na wewe bila kuogopa. Lakini ambao ni marafiki wa fursa wameanza kukukana na hata kukukimbia. Watajitokeza pia ambao pamoja na kuwa uliwahi kuwasaidia, wataongeza moto dhidi yako. Ikitokea hivyo, basi soma Zaburi 35.
Hakuna jambo lolote utakalotendwa kwa siri au kutendewa kwa siri litaweza kusitirika milele. Tunatoa wito kwa wenye mamlaka kulinda haki zako ikiwemo ulinzi. Ila sisi hatuwezi kupuuzia minong'ono inayozunguka ya kuwa kuna dalili kuwa usalama wako uko hatihati. Hii inatokana na ukweli kuwa kuna kauli nyingi sana za chuki dhidi yako kutoka kwa baadhi ya makada walio ndani ya UVCCM au CCM kwa ujumla.
Hatutarajii kuona yaliyomfika Balozi Humphrey Polepole yakufike na wewe. Hii ni kutokana na ukweli kuwa siku hizi mtu anayetofautiana na watawala, dawa yake inakuwa kumpoteza au hata kumuua.
Kama kweli watawala hawana mpango wowote ulio mbaya kwako, basi pia tunatarajia kukuona ukijitokeza hadharani na kuongea na vyombo vya habari na kutoa ufafanuzi hasa kuhusiana kujiuzulu kwako.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 28 Agosti 2026; Saa 6:45 usiku.