Meya ashushiwa kipigo kikali kikaoni, aokolewa na walinzi wa Manispaa, akimbizwa hospitalini

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,833
21,466
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi, Zuber Kidumo amejikuta akichezea kichapo kikali kutoka kwa diwani mwenzake, Abuu Shayo, wakati akiendesha kikao cha Kamati ya Mipango Miji na Ardhi katika manispaa hiyo.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa sita mchana mjini Moshi, wakati kamati hiyo ikiendelea na kikao chake, ambapo wajumbe wa kamati hiyo walikuwa wakiuliza maswali mbalimbali kwa Mstahiki Meya huyo ili kupata ufafanuzi wa masuala ambayo wanaona hayako sawa.

Mmoja ya wajumbe wa kamati hiyo, Abuu Shayo, ambaye ni diwani wa Kata ya Mji Mpya katika manispaa hiyo, alihoji mchanganuo wa shilingi milioni 50 zilizotumika kwenye ujenzi wa madarasa mawili ya shule ya msingi, wakati kunafedha kiasi cha shilingi milioni 20 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu ambazo zingetosha kwa ujenzi wa darasa pamoja na madawati yake.

Taarifa zimedai kuwa Meya alimjibu kuwa taarifa za ujenzi wa madarasa hayo zitatolewa kwenye kata yake, hata hivyo diwani huyo alionesha kutoridhika na majibu hayo kwa sababu Meya alimwahidi kumjibu katika kikao hicho.

Diwani huyo hakuishia hapo, aliomba kuuliza swali lingine ambapo alihoji matumizi ya shilingi milioni 920 zilizotumika kujenga ukuta unaozunguka manispaa hiyo usiopigwa hata plasta, wakati kuna jengo la gorofa pamoja na ofisi za watendaji zilizogharamia kiasi cha shilingi bilioni 1, na kudai kuna harufu ya upendeleo kwenye ujenzi wa ukuta.

Swali hilo lilimkasirisha meya huyo, ambapo alishuka kutoka kiti cha mbele alikokuwa ameketi na kumfuata diwani huyo aliyekuwa ameketi viti vya wajumbe na kumkwida kwa kumshika tai akidai amezidi kuuliza maswali ya kuchokonoa vitu kila siku.

Lakini meya huyo alijikuta akiambulia kipigo kikali kwa kupigwa makofi, mateke, kugaragazwa chini, na kupigwa na chupa za maji, na baadaye aliokolewa na walinzi wa Halmashauri hiyo akiwa amelowa chepe.

Askari hao wa manispaa walimwokoa kwa kumtoa nje, huku wakionekana kufurahia kipigo alichokipata. Walisikika wakisema "amezidi kiherehere".

Akiongelea kadhia hiyo, Abuu alisema, "Ni kweli mimi nilihoji kuhusu fedha za umma, lakini nikashangaa mtu anakuwa mkali na kuna fununu kahongwa zaidi ya milioni 30 yeye na mwenzake. Yote hii ni rushwa tupu, sasa nauliza, yeye anakuja nishika shati na kuanza kunishambulia".

Meya Zuber alisikika akisema, "Anamshukuru sana Diwani wa Kiusa na walinzi wa Halmashauri kwa kutuliza vurugu na kumwokoa, na kusisitiza kuwa taarifa zaidi ataitoa akitoka hospitalini."

Hata hivyo, alipopigiwa simu majira ya jioni, alijibu kwa kifupi kuwa hajatofautiana na mtu yoyote na kukata simu.
 
Huko Moshi hiki cheo cha umeya wakitoe tu maana inaonekana wote wanaokishika vichwani ni hamnazo.

Nakumbuka kusoma humu aliyemtangulia huyu nae alihisiwa kuwa ms£πge baada ya kuandaa na kufanya party ya was£πge na kukatika viuno hadharani shanga zikimvuka.
 
MEYA ASHUSHIWA KIPIGO KIKALI KIKAONI ,AOKOLEWA NA WALINZI WA MANISPAA.

AKIMBIZWA HOSPITALINI,AMSHUKURU MUNGU KWA KUNUSURIKA

018ce150481651f8f61db787c459b64c.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom