Mama mmoja, kwa jina la Kalie Robins, ameibua wasiwasi kuhusu namna tool ya Meta AI inavyoweza kutumia taarifa zilizowahi kuchapishwa mtandaoni kukusanya na kuhusisha taarifa binafsi.
Kwenye video hii Robins anasema alichapisha video iliyokuwa ikimuonyesha yeye na binti yake wakiimba ndani ya gari, lakini alishangazwa kuona Facebook ikimpendekezea swali kupitia Meta AI lililouliza, *“Nani huyo mtoto aliyekaa siti ya abiria?”
Baada ya kubofya swali hilo, anasema Meta AI ilianza kuonyesha taarifa zinazohusiana na Mtoto wake, ikiwemo majina, taarifa za kuzaliwa pamoja na picha na video zilizowahi kuchapishwa katika kurasa mbalimbali za familia.
Robins anasema tool hiyo hata ilionyesha picha ya mtoto wake akiwa mchanga ambayo ilikuwa imechapishwa miaka iliyopita kwenye ukurasa wa bibi yake, huku akidai kuwa picha hiyo aliwahi kuifuta kwenye ukurasa huo
Wasiwasi wake uliongezeka zaidi baada ya Meta AI ya facebook kupendekeza swali jingine kuhusu mahali anapoishi. Robins alisema baada ya kulifuatilia, mfumo ulianza kuunganisha machapisho yake ya zamani na mapya ili kubaini maeneo ambayo amewahi kuishi na hatimaye kujaribu kubainisha eneo analoishi sasa.
"And then, Facebook suggests that I ask Meta AI, 'Where does Kalie Robins live?' Are you kidding me? So I clicked that too, and it starts digging through completely unrelated shit from years of my life. Old posts connecting me to where I used to live, newer posts connecting me to where I live now... and then it says, 'Pinpointing Kalie Robins' location.' It pieced together my information to show people where I live"
Robins anasema tukio hilo limemfanya aamue kuondoa picha na video zinazoweza kuwatambulisha watoto wake kutoka kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii. Pia amewataka ndugu na marafiki ambao wamewahi kuchapisha picha za watoto wake kuziondoa.
Anasema awali hakufahamu kuwa taarifa ndogo ndogo ambazo familia imekuwa ikishiriki mtandaoni kwa miaka mingi zinaweza kuunganishwa na teknolojia ya AI na kutengeneza picha pana zaidi kuhusu watoto wake.
Kwa upande wake, mtayarishaji wa video hiyo ameeleza namna AI inavyoweza kutumia taarifa na picha zilizopo mtandaoni kutengeneza maudhui mapya, akidai kuwa suala hilo linaweza kuhitaji hatua za kisheria.
Kuwa Makini, Teknolojia ya AI (Akili unde) inaweza kutumia taarifa binafsi ambazo watumiaji walizichapisha katika nyakati na mazingira tofauti.