Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,850
- 5,490
Habari yenu wanajukwaa, natumai mpo vyema kiafya na mnaendelea vyema na maisha kiujumla. Nami Mungu anasaidia kiasi chake kwenye masuala yangu.
Naomba niende moja kwa moja kwenye hoja, inayogusa matumizi ya AI kwenye maisha yetu ya kila siku. Kiasi kwamba imekuwa ni msaada mkubwa kwenye nyanja mbalimbali.
Wakuu AI inafanya kazi kwa kukupatia wewe na mimi taarifa zilizopo mtandaoni, kupitia sehemu mbalimbali. Ikiwa taarifa ya swali unalouliza haipo kwenye mfumo wowote haitaweza kukupa jibu stahiki. Mara zingime hujibu "najifunza zaidi".
Ikitokea aliyejaza taarifa mtandaoni hakuweka taarifa sahihi, basi na wewe ukija kuuliza kuhusu suala lile basi utapewa taarifa ambayo si sahihi, kwa sababu ndiyo iliyopo.
AI zingine hazina taarifa kwa upana huweza kutoa majibu yasiyo sahihi. Mfano Meta AI ina changamoto hii kuboronga kwenye utoaji taarifa. Sababu ina uhaba wa data wa suala unalopeleka.
Nakiri AI imetusaidia sana kwenye designs, image generation na mengineyo. Ila wadau unapochukua taarifa huko kwa lengo la kuitumia sehemu rasmi, nakusihi hakiki vyema.
AI yetu pendwa inatupa chakula kizuri, penginepo kuna mdau huko mtandaoni kaweka sumu ikakuletea kama ilivyo. Naomba tuwe makini sana na taarifa zao.
Uzuri ni program pia inayokusanya taarifa juu ya mambo mengine mapya yanayoingia mtandaoni lwa namna tofauti ila bado uhakika wa taarifa muda mwingine una shaka.
Ni hayo tu wakuu.