Meremeta & TANGOLD Revealed!

Meremeta & TANGOLD Revealed!

Mkapa Unahatarisha Usalama Wa nchi yetu.............

Kama kawa ni lazima nitaibukia popote kwenye hii mijadala.
Ni wazi kuwa kuna wengi tunashare mawazo lakini approaching ni well.... Tofauti.

Na ndio maana threads zangu zote zinaanza kumake sense sasa hivi na wengi hawayapuuzii mawazo yangu kama walivyokuwa wakifanya kabla.

Nilishasema kuwaweka mafisadi LUPANGO kutaliponya TAIFA kwani issue kuwa wanahatarisha usalama wa taifa kwa kuligawa nilishaiweka wazi toka siku ya kwanza nillipogundua mbinu hizi na mikakati ya kusafishana machoni pa watanzania kwa kuanzia na ziara zao za vijijini!

Sasa Kikwete ni kiongozi gani huyu?

PINDA MTU WA ROZARI...WALIMTUMIA ILI KUWAHADAA WANANCHI ILI TUSIKILIZE PUMBA ZAO KWA KUPITIA KWAKE!

Tatizo ni kwamba hata chinga wenyewe sasa wanajuwa mateso yao yamesababishwa na nani...Pia wanajua wanapigwa bao kwani USHAHIDI WOTE UKO NJE NJE!
 
Leo nakubaliana na Mushi kwamba mafisadi wasipokamatwa na kuchukuliwa hatua watatugawa/tena tumeshagawika.
 
For decades, Pinda was a tried and trusted aid to Presidents.

Hardly learned a thing!

Or, was there anything to learn?
 
Magwiji ehe!! Tafadhalini sana tena sana acheni kumwita huyu jambazi na fisadi namba moja muungwana!!
Ndiyo jina Ambalo analipenda a.k.a Wa kusifiwa na ndiyo maana hata Kabadili Muonekano wake katika Picha.Huyu ndiye anataka aonekane yeye yu safi kwa kuwatumia watu kumsemea.Tunajua yeye ndiye anayewatuma hawa

1.Serukamba
2.Anna Abdallah
3.Mzindakaya
4.Pinda
5.Salva rweyemamu
6.Mbunge kilaza wa Jimbo la Geita
 
si kwa mbali tena, tumeshamjua vilivya na kwakweli hatumtaki tena anatia kichefuchefu tuu....

mkuu unaweza ukatupa angalau mwangaza wa vichwa ngumu vilivyopo kwenye Meremeta yaani list nzima ya vigogo wanao kula mgao huko.
 
kwanza kabisa nahitaji kujua, katuambia kwa misingi ipi?? kwani kazi ya kamati yao mbovu imeisha?? wameshakabidhi report?? nakumbuka merermete iko epa na kazi ya EPA bado kukamilika.... nami kamtuma???
 
mkuu unaweza ukatupa angalau mwangaza wa vichwa ngumu vilivyopo kwenye Meremeta yaani list nzima ya vigogo wanao kula mgao huko.

Kila mtu anajuwa MEREMETA nia ya nani na ndio maana tumemdharau PINDA MOJA KWA MOJA!
BASI TENA.
 
Unajua Jmushi mm nakukubali sana tena kwa juhudi binafsi inavyo fanya humu ndani.
Nakupa pongezi sana.Lakini baadhi yetu tumeanza kugawika kutokana na hii vita kali sana mafisadi wengine wanaishi mijini kwa mgongo wa hawa mafisadi sasa kitu kibaya ni wachache sana wanao pata ofa kama hizo kutoka kwa mafisadi huku wakiwaacha waTanzania walio wengi wakipigika na maisha.
Jmushi wewe ni mkombozi tukaze uzi tu mpaka kitaeleweka.
 
Nasikia raha ya roho,maana Bunge linachemka utadhani tuko Ulaya.Siku hizi wabunge wa CCM wanafoka kwelikweli....na wao...heheheheh...ati hapatoshi hapa.

Ukiona wanapaaza sauti zao bila woga ujue hayo ni mabadiliko makubwa maana wakati wa lile dude liitwalo Mkapa walikuwa kama watoto wa shule ya msingi.

Wakati wa Nyerere Bunge la Chama kimoja wabunge walikuwa ni waumini na Nyerere alikuwa Mungu mtu.mambo serious kama haya yangeweza kumtoa mtu roho wakati huo.Nafurahi kuona mahojiano yakiwaka moto wakati wa awamu ya nne si kwa wabunge tu bali hata wananchi wengine kwenye forums mbalimbali.

Kama hapa naona Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anapewa mkong'oto wa hoja za msingi.hakuna kuambiwa ukakubali na kutiii bali unapewa hoja za wazi.namshukuru mwenyezi Mungu kuwa awamu ya Nne imekuwa ni ya wanamchi kuwaandama mafisadi Bungeni hadi barabarani.This is a step forward in the awakening the peoples minds.

Hapa unakuta watu wanamwita Nyerere fisadi..na wanakupa points...like JMushi.Wengine tunafurahia mijadala ya watu wenye hasira na jinsi mambo yasivyokwenda chap chap kama wanavyotaka wao.
yote haya ni dalili kuwa kunaanza kucha.Akili zinachemka.

Mimi hapa sitajadili mada..ila ndani ya mada naona raha ya mwamko wa watu.Ipo siku watu wote wataamka na kuchukua hatua za kutupatia utawala bora.
 
Magwiji ehe!! Tafadhalini sana tena sana acheni kumwita huyu jambazi na fisadi namba moja muungwana!!

Hata Kalumanzira ana waungwana wake, nafikiri huyu ni mmoja wao.

Also, in satire muungwana ni mtu asiyetaka kuchakalika na kazi za mikono kutokana na class yake na yuko radhi kufa masikini kuliko kufanya kazi demeaning (hence "gentleman's pass" inapatikana na mtu ambaye bado kiduchu angefeli, D- au daraja la kufeli ongeza moja).

Inaonekana Kikwete ni muungwana sana ku fire watu, muungwana sana kufanya kitu chochote serious, amebakia mtu wa gumzo tu na lame duck president.


Hence muungwana.
 
Am total lost
no direction
niliyeanza kumuamini ameanza kupaka rangi uongo ili ionekane kana kwamba ni kweli
Naanza kujichukia
 
hapa sijaelewa, alikuwa na maana ya Jambo Forums aka Jamii Forums?

Ninavyoelewa mimi jambo technical ni jambo lenye ugumu wa kiufundi, kama ukimuuliza Pinda kwa mfano kuhusu mambo ya wagonjwa Muhimbili ambayo yanahitaji ujuzi wa ufundi wa kidaktari anaweza kukwambia "mimi siwezi kujibu jambo technical"

Lakini hii ni excuse kwa sababu Waziri Mkuu ana washauri wenye kujua technical detail, anaweza asiweze kujibu hapo kwa papo, lakini kama ni kitu anachotakiwa kujibu hii siyo excuse ya kutojibu, anaweza kushauriana na washauri wake.

Anatuonyesha zaidi asivyoijua kazi yake.
 
Nafikiri mpaka sasa tunaweza kushuhudia kabisa dhana nzima ya ufisadi na kujua fisadi hawa ni nani?

Kama Mzee Pinda aliyechaguliwa juzi umeona ameelekea hata kumuona Lowassa ni mtu muhimu kwake wakati akijua mahusiano ya wananchi na Lowassa. Basi lazima tujue tuna kazi nzito sana na wale wazuri walioko chama cha Mapinduzi lazima wajue sasa kazi ni ngumu kuliko walivyotegemea.

Fisadi anayeongoza mafisadi wenzake Pinda ametuonyesha rasmi sasa ni sisi wananchi kuangalia mbele na kujua ni nani hao haswa na nani ni kiongozi wao.

Kwa usemi wa pinda aliyeapa kwa nguvu zote kuwatumikia wananchi ningeomba ajiuzuru kwa sababu hataweza kazi hii.

Kazi iliyoko mbele yake ni ngumu mno kuliko uwezo wake. Ndio maana tangia apewe kile cheo ameonekana kupwaya na kuwa mkimya sana. Leo hii amedhihirisha kwa nini alihamua kunyamaza.
 
Dk.Slaa amesimama na kusema mambo ya Ubadhirifu hayana siri.... maelezo baadaye
 
Back
Top Bottom