Meremeta & TANGOLD Revealed!

Meremeta & TANGOLD Revealed!

ndiyo nimesoma sasa hivi, huu ni usanii wa hali ya juu...tutasikia EPA nazo hela zilitumika na Jeshi. Sasa si am-implicate amiri jeshi mkuu kwa kusema hivyo?---->ex-bosi wake BWM
 
Binafsi siwezi kumalaumu pinda, kwa sababu ninaiangalia kwa makini sana our system ya siasa na utawala, who is pinda? Hapa Jf hakuna aliyehusika na kumchagua pinda, alichaguliwa na rais, wengi hapa tulisema tumpe muda tuone, sasa muda umefika na ukweli uko wazii kwamba ni wale wale yaani mazumbukuku na limbukeni wa power,

Anawaogopa waliompa power masikini wa Mungu hajui kuwa akisimamia wananchi anaweza kuwatupa waliompa power na hata kuwafunga, haelewi kuwa yeye sasa ndiye mwenye power, wakatuambia kuwa huyu amefanya kazi na Mwalimu, akaenda mpaka makanisani kupewa Rosary na Mama Maria, ndio maana tulisema hata hawa Nyerere waliobaki nao wameanza kuwa mafisadi,

Sasa huyu naye ni wale wale, hakuna matumaini kabisaa hata hiyo ripoti ya Richimonduli itakuwa yale yale watch atasema kuwa ni ishu ya bunge sio ya wananchi, sasa katika vacuum ya who to trust wananchi tunafanya nini? Tunarudi kuwalilia kina Mwakyembe na mama Kilango kuwa tunawaomba wajitahidi hivyo hivyo kuwapigia kengele mafisadi, na sisi tuko nyuma tunawafichua, ngoja niingie kutafuta dataz ya kinachojiri huko bungeni sasa,

Wananchi tumeliwa kwenye hili la Meremeta!

Maneno yangu kuwa kifo cha mwalimu kilikuwa ndio mwanzo wa MWISHO wa chama cha ccm ni wazi sasa yaenda kuwa kweli!

Na pia FAMILIA YA MWALIMU SASA NI AIBU tupu na ile sifa ya familia yao kwisha mbali tangia siku na wao walipoamua kumkumbatia MKAPA!

Makongoro amekongoroka na kukataa kumtoa MKAPA kwenye heshima ya kuwemo ndani ya familia ya NYERERE NA HAPO ndipo MKAPA alipopata nguvu za kuhudhuria kiakao cha ccm kilichokuja na hili changa la macho la KIMAFIA!

Kama familia ya mwalimu wangekubali kumvua MKAPA heshima ya kuwa mwanafamilia wa NYERERE basi hata wana ccm wazalendo wangepata nguvu.

Walikataa kufanya hivyo na ndio maana nikasema ccm ILIKUFA SIKU WWALIMU ALIPOKUFA...Kwani kama angekuwa hai basi asingekubali MKAPA AENDELE KUWA NDANI YA FAMILIA YAKE.
 
inavyonikera mimi hii ccm ni kuwa imekosa heshima hata kwa wanachama wake wenyewe waliowachagua.
viongozi wanaoweza kuwavunjia heshima waliowachaguwa kwa kuwaona wanaweza kupokea uongo wa waina yoyote, sidhani kama wanashindwa kufanya maovu mengine yoyote.
hapa walipofikia, viongozi wa ccm wanaweza kufanya jengne lolote, baya zaidi ya hilo, na wasishtuke wala kujali.
 
hatatachomoka, hatuta kubali, liwalo naliwe hatuwezi kutukanwa hivi.. tena kila siku... ohh pesa za EPA si za umma oooh meremeta siri ya jeshi, nani alimtuma aibe.. nyie hamjui kuwa si muda mrufu mnasbbsha mauaji ya watu badala ya mkapa pekee afungwe... hivi hamjajifunza yaliotokea tabata dampo juzi usiku????

Hawajui kuwa Muda umewadia. Huwezi kumbana mtu kwenye ukuta siku zote, kuna siku ata-Retaliate, and use whatever means necessary.
 
Hawajui kuwa Muda umewadia. Huwezi kumbana mtu kwenye ukuta siku zote, kuna siku ata-Retaliate, and use whatever means necessary.

Hawa wantuprovek kweli nakwambia....... wamesahau watoto wa pale msikiti wa mwembe
chai magomeni walivowasumbua..........
 
Na Huu Ni Ujumbe Kwa Kina Makongoro,butiku Na Vituko Wengine...kuwa Na Nyie Si Kitu Tena Machoni Petu Wazalendo!
Tena Hata Mwalimu Hana Mpango Tena!
Hilo Jina La Baba Wa Taifa Nyie Mamluki Wa UFISADI YAle Aliyokuwa Akiyapinga Mmepelekea Kuporomosha Umaarufu Wake Na Ndio Maana Hata Huo Mfuko Wa Foundation Wa Butiku Ulikuwa Kapa!
Mnaaibisha!
Mlimpeleka Mkapa Kaburini Kwa Mwalimu Kutambika?
Familia Ya Mwalimu Wanaomkumbatia Makapa Wameidhalilisha Historia Si Tu Ya Tanzania Na Wananchi Wake...bali Mwalimu Mwenyewe!
pamoja na UTU na UBINADAMU!
 
Hawa jamaa ni wasanii. Hakuna jipya hata aje nani. Maana haiwezekani wewe mtu mmoja hata ukiwa malaika huweze kufanya mambo yako kwenye mstari. Pinda hata awe makini vipi watu waliomzunguka ndiyo uleule uozo unategemea nini? Tunaitaji mabadiliko na yawe kote kuoanzia juu hadi chini.

Hivi hawa jamaa hawajui kuwa hili jeshi ambalo wanasema ni usalama wa nchi hela zake ni kodi tunazokatwa kila mwezi then leo mtu anakwambia ni siri! Angalia mambo yao siri hizi mpaka kwenye kununua vitu vibovu Helicopta juzi imeua hawataki kutoa tamko kuwa ni kati ya zile za kifisadi.

Pinda lazima atoe majibu ya kueleweka hii ni aibu kuwa na mzazi anayeongea takataka kwenye chombo kikubwa cha bunge inabidi na familia ziwatenge hawa jamaa maana wanateketeza kizazi kwa kuendekeza matumbo.
 
yaani unapelekwa sehemu ambayo sio yako

Nimekuelewa mkuu...... kuna mengi sana utayasikia toka kwa Pinda. Sidhani kama ni vizuri kukumbushia walichosema watu hapa wakati Pinda ameteuliwa kuwa PM ila kwa mbali sasa inaanza kuonekana.
 
Kama MKAPA BADO ANATAMBULIWA KUWA NI MWANAFAMILIA WA NYERERE LICHA YA KUIUZA NCHI THEN KWANINI TUSISEME MWALIMU NDIYE ALIMTUMA KUFANYA HIVYO NA TO HELL WITH MWALIMU KWANI NA YEYE NI FISADI(MUNGU AENDELEE KUMLAZA PEMA PEPONI)
Kama mwalimu hakuwa fisadi then kwanini alimchagua MKAPA NA YEYE AKAUZA NCHI KAMA MWANAFAMILIA WA NYERERE?
KUSEMA FAMILIA YA NYERERE NA ccm YAO INAYOELEKEA UKINGONI NI MAFISADI NA HATA HAWANA SIFA YA KUWA WANAMAPINDUZI WA TANZANIA MTAKATAA?
 
Brief Details of Mereremeta
Kwa mujibu wa serikali Mereremeta ilifantiwa Usajiri August 19 mwaka 1997,siku ya Jumanne na ilipewa Usjili wa No.registration No. 3424504.

Kwa mujibu wa Taarifa aliyotoa Dr. slaa,Kampuni hiyo ilifanyiwa Usajili October 3 mwaka 1997,ambayo ilikuwa siku ya Ijumma kama Leona lilipewa numbeer ya usajili Certificate of Compliance No.32755.


The reasons for the formation of offshore firms are
1.privacy,
2.asset protection
3. tax savings
4. lawsuit protection
5.flexible business laws
6.Confidentiality


KWa mujibu wa Mkono akihojiwa na Gazeti la Mwananchi alisema Kwamba Serikali imekuwa ikisitita kusema Mmiliki waMeremeta ambaye amechukua pesa nyingi ya Walipa Kodi.Na akiongea na Gazeti la Citizen alisema haya
"I have evidence that this ghost company pocketed a total of Sh181 billion and yet nobody wants to speak about it."


Kama Pinda Kasema anasema Mereremeta ni Kampuni ya Jeshi,

Na kwa kuwa Mheshimiwa Mkono alinukuliwa na Gazeti la The citizen kwamba anafahamu kampuni hiyo ilichukua billioni 181.

Na kwa kuwa hauwezi kufahamu kampuni ilichukua pesa nyingi bila kumjua aliyepewa,Basi Mkono anamfahamu aliyelipwa pesa za Meremeta.

Mkono,Yes I saidTuambie Nani ni mmiliki wa Meremeta sababu unamjua?
 
Hayo majibu yote ni POYOYO za kuwafanya WADANGANYIKA wazidi kukaliwa na wachache vichwani LAKINI tunadhani hatuna mtu wa kutuwakilisha sisi WANYONGE kwani tuliyekuwa TUNAMTEGEMEA ndiyo katoa MAJIBU anayoyaita MAKINI !!!!!! LAKINI HATA HIVYO TUTAFIKA HATA KAMA IKIWEZEKANA KU................................, mwisho wa siku ndio utakaotoa MAAMUZI MBADALA !!!!!!
 
Kama MKAPA BADO ANATAMBULIWA KUWA NI MWANAFAMILIA WA NYERERE LICHA YA KUIUZA NCHI THEN KWANINI TUSISEME MWALIMU NDIYE ALIMTUMA KUFANYA HIVYO NA TO HELL WITH MWALIMU KWANI NA YEYE NI FISADI(MUNGU AENDELEE KUMLAZA PEMA PEPONI)
Kama mwalimu hakuwa fisadi then kwanini alimchagua MKAPA NA YEYE AKAUZA NCHI KAMA MWANAFAMILIA WA NYERERE?
KUSEMA FAMILIA YA NYERERE NA ccm YAO INAYOELEKEA UKINGONI NI MAFISADI NA HATA HAWANA SIFA YA KUWA WANAMAPINDUZI WA TANZANIA MTAKATAA?
 
SIJA edit: Pinda anasema:

MEREMETA, Tangold, Ngeleja naona tutamuonea. Kwa mazingira ya jambo lenyewe suala la Meremeta limejikita ndani ya JWTZ, haukuwa mradi tumeukuta uraiani in unique situation... mimi kuanza kusema kila kitu siwezi.... Ni suala linalohusiana kwa karibu sana na mambo ya ulinzi na usalama wetu, ni lazima tulilinde,,, Kama mtaona inatosha sawa, kama mnataka kunisulubu nitakuwapo pale kwa ajili hiyo

EPA naona ina mvuto mkubwa sana. Kuna fedha ambazo watanzania wanataka kujua zimetokaje BOT, mradi zilikua BoT katika chombo cha serikali, haiwezekani ukamwachia mtu tu akachukua hizo fedha,. Hoja hapa zimekwenda kwa nani, utaratibu umefuatwa? Rais kasema tumwachie, wote tuna interest, sasa kwa mtazamao wangu shauku ni kubwa, watu wangependa leo, nafirikri tufanye subira, muda wenyewe umekwisha labda sana sana watasema muda uongezwe, lakini hapo baadaye tutaulizana maswali oooh zilikuwa za mhindi, ooh zilikua za nani!!! Naomba nitoe rai kwa muda uliobaki tusubiri. Nitakwambia sijui, hata mimi Mwanyika nikimuuliza anasema... Liko la Ballali marehemu na Slaa, serikali itoe taarifa, halafu kuna mahali alisema Slaa, kutotoa taarifa kaa tunachezea, angetamani iundwe kamati ya kuchunguza kifo cha Ballali! Sasa sijui lakini naelewa iko connected kwamba alijua siri, hili wazo kuhusu usiri kama kwamba BAllali ... huyu mtu amefariki na ndugu zake wanasema amefariki, sasa kuendelea kumzungumza huyu marehemu. Kifo chake hofu iko wapi? Labda muombe postmortem, nani asiyejua kwamba hakuwapo. Tungoje taarifa ya mapesa yetu, kama watamtaja basi tungoje, Mkisema niseme, labda ndugu zake, lakini si serikali, hamtutendei haki. Na kwa merehemu akifa, kwa kweli ngumu sana.... Nadhani kwa sasa serikali haioni sababu ya Kamati, EPA kama anahyusika atatajwa tu... Hawa wanasukuma ajenda wana sababu tu. Kama kuna ushahidi zaidi ya tulio nao mtu anaweza kuuleta tukautazama.

KIWIRA nalo mimi najua Dk. Slaa akisema mpaka unaogopa... Wakaniletea maelezo marefu sana. Wakaleta itakusaidia? Mimi siwezi kuingia katika jambo technical, nilidhani ili kuwapa fair pix hii Kiwira, mturuhusu, Ngeleja aje na kauli ya serikali ili apate muda wa kulizungumza kwa upana wake, ili kujua ... Kiwira wakati ikiuzwa ilikua dead proj ilikua katika hali mbaya sana.. Ili tuweze kuwa na benefit ilikuwa smooth exercise ilikuwa interest kupata mwekezaji, ningeomba nipate more details.

Huyu Pinda naye ana mawazo mufilisi. Tangu lini jeshi likajishughulisha na mambo ya madini? Ni nani aliyeamua jeshi lijishughulishe na madini? Kwa mslahi ya nani? Hawa mafisadi waliamua kulitumia jeshi labda wakijua Watanzania tukisikia jeshi limehusika basi tutaogopa kuhoji madudu yote yanayohusika na Meremeta. Si ajabu katika madudu ya meremeta hawa wakuu wa jeshi wa sasa na waliostaafu walihusika na ufisadi huo ili wayafumbie macho madudu yaliyotokea.

Watanzania tunataka majibu yanayoeleweka, tumechoka kuibiwa mchana kweupe na mafisadi wanaojivisha ngozi ya uongozi ili waendelee kutuibia Watanzania huku wao wakiwa matajiri wa kupindukia wakati Watanzania walio wengi kila kona ya nchi wakiishi maisha ya dhiki kubwa. Kama hamna maelezo ya kuturidhisha Watanzania na pia kuwafungulia mashtaka wahusika wote wa EPA, Richmond, mikataba ya madini, Kiwira n.k. basi serikali ni bora ijiuzulu na tufanye uchaguzi mwingine.

Hakuna sababu yoyote ya kuendelea kuwa na serikali madarakani ambayo inaonyesha kabisa kwamba imeshindwa kutetea maslahi ya Tanzania na Watanzania.

Kama Mzee Rukhsa aliweza kujiuzulu kufuatia mauaji yaliyotokea Shinyanga wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani, basi wewe Pinda na JK na serikali yake yote mnaweza na mnatakiwa mjiuzulu kwa kushindwa kutetea maslahi ya Watanzania. Tumechoka na kauli zenu za ubabaishaji.

Alutta Continua!
 
Jamani we are done. We are finished!!! There is no more hope!!

Pinda amechanganya mambo kiasi ambacho conclusion ni kuwa huyu mtu haelewi bunge ni nini??? Yaani hela ziibiwe wewe useme ni Ulinzi na Usalama??? Kwani Bunge si linapitisha bajeti za Jeshi, Usalama, Polisi blah blah?? Sasa hiyo ni reason kweli??

Halafu EPA amesema labda watadai waongezewe muda, muda wa nini???

Ama kweli nimeweka manyanga chini na kuanzia leo nitakuwa nasoma mambo ya bunge kama Ze Comedy.

May God Bless Us All
 
Kwanini leo Sitta Hakuwepo,Huu ndiyo Mgawanyiko tuliokuwa tunausema..Hyu Mama Makinda yupo pale kwa Maslahi ya wezi..Hata kama anasifika Yeye ni mtaalam wa mambo ya Anga.

Aache kutufanya siye Mazezeta..Huu Ni Mtego unasao,

Ndugu watanzania,

Ninazidi kumjua Vizuri Muungwana ni mtu wa Namna Gani,ataki alaumiwe na watanzania ili abaki kuwa shujaa wakati hizi ni siasa za kizamani na zisizo na Msingi.

Magwiji ehe!! Tafadhalini sana tena sana acheni kumwita huyu jambazi na fisadi namba moja muungwana!!
 
Back
Top Bottom