Halisi
JF-Expert Member
- Jan 16, 2007
- 2,802
- 613
Raia Mwema - Muungwana ni Vitendo
Siri za Meremeta kwenye mtandao
Serikali yatikisika, Usalama wa Taifa wafuatilia
Nakala 100 za ripoti hiyo zaandaliwa
SAKATA la kampuni ya Meremeta Limited iliyochota Benki Kuu ya Tanzania Sh bilioni 155 na ambalo sasa serikali imetangaza kwamba inahusiana na mambo ya Usalama wa Taifa, limeingia katika hatua mpya, baada ya kuelezwa kwamba sasa ripoti kamili ya siri kuhusu ufisadi huo itaanikwa katika mtandao.
Taarifa zilizotolewa kwenye mitandao ya Mwanakijiji.com na jamiiforums.com
Mwanachama huyo, ambaye alikuwamo ndani ya serikali wakati wa mchakato wa uanzishwaji wa Meremeta, alielezea kutoridhishwa kwake na maelezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kutaka aeleze kuhusu Meremeta; vinginevyo yeye na wenzake wataamua kufanya kazi hiyo ili kuhakikisha kuwa mjadala wa Meremeta unamalizwa.
Raia Mwema limefahamishwa kwamba tayari vyombo vya usalama vimeanza kufuatilia suala hilo na huenda kukatokea mtikisiko mkubwa serikalini baada ya kusomwa kwa ripoti hiyo.
Taarifa hizo ambazo zinaonekana kama kujichukulia majukumu mikononi, kundi la Watanzania hao limeamua kufichua siri ya "usalama wa taifa" inayohusisha kampuni hiyo ya Meremeta ambayo ilianzishwa kwa kazi ya ununuzi na uchimbaji dhahabu.
Kampuni hiyo, ambayo iliandikishwa Uingereza mwaka 1997 na baadaye kufilisiwa huko huko Uingereza mwaka 2006, imezua malumbano makali bungeni hivi karibuni baada ya baadhi ya wabunge kupinga matumizi mabaya ya fedha kuhusishwa na usalama wa taifa.
Ndani ya mtandao huo imeelezwa kwamba kufichuliwa kwa kampuni hiyo kunatarajiwa siku yoyote wiki hii baada ya uchunguzi wa muda mrefu na ukusanyaji wa taarifa mbalimbali ambao umefanywa na Watanzania hao katika ushirikiano wa aina ya pekee wakiwa wametawanyika sehemu nbalimbali duniani.
Akiandika katika mtandao wake, mwanachama huyo alimwambia hivi Waziri Mkuu:
"Kwa vile suala la usalama linahusu usalama wa Taifa letu na wanaoohoji ni wabunge wa Taifa hilo ambao ni wawakilishi wetu, basi hata kama suala la Meremeta haliwezi kuwekwa hadharani (kwa kurushwa kwenye Luninga) basi Bunge lifunge macho na masikio ya nje na Wabunge wote wawe briefed wazi na moja kwa moja kuhusu Meremeta, umiliki wake na uhusiano wake na jeshi na usalama wa Taifa.
"Na endapo wabunge wataridhika, basi, tutapenda kusikia kuwa wameridhika na maelezo hayo na kama wabunge wapige kura kama wasimamizi wa serikali kuamua kama habari hizo kweli zinatishia usalama wa Taifa na kama wananchi wanapaswa kuziona."
Maelezo ndani ya mtandao huo yameeleza kwamba tangu ombi hilo litolewe hakuna dalili yoyote ya serikali kuwa wazi juu ya Meremeta na kuwalazimu Watanzania hao kuunganisha nguvu zao na raslimali zao kufanya utafiti wa kina wa suala zima la Meremeta.
Kwa mujibu wa mmoja wa washiriki wa watafiti hao ambaye alikataa kutajwa jina lake kwa sababu ya utaratibu wao wa kutojitambulisha, "ripoti hii inakusudia kuchochea jitihada za kutafuta ukweli wote juu ya Meremeta kwa kufunua kwa kiasi kikubwa kile ambacho kilikuwa hakijulikani".
Sehemu ya ripoti hiyo, ambayo mwandishi ameweza kuiona, inagusa mambo mazito ambayo kwa hakika hakuna kiongozi wa kisiasa mwenye akili timamu ambaye angethubutu kuyaachilia hadharani hasa katika mazingira ya kisiasa katika Tanzania na katika maeneo ya maziwa makuu.
Sehemu ya ripoti hiyo inayohoji uhusiano kati ya Meremeta na Mgodi wa Buhemba inasomeka hivi "Kama Meremeta Ltd ni kampuni ya jeshi na Buhemba Gold Mine iko chini ya jeshi ni kwanini basi jeshi hilo hilo liingie mkataba na kampuni yake nyingine wakati vyote viko chini ya Mkuu mmoja na Wizara moja?"
Ripoti hiyo inaendelea kuelezea kwa kirefu juu ya kampuni moja ambayo ndiyo iliingia mkataba na serikali kuanzisha kampuni ya Meremeta. Kwa mujibu wa mdokezaji wetu "kampuni hiyo siyo Triennex ambayo imekuwa ikitajwa mara kwa mara". Hata tulipombana kuelezea ni kampuni gani basi iliyoingia mkataba huo na kwanini haijulikani, mdokezaji huyo alikataa akisema, "tafuta ripoti uisome mwenyewe".
Raia Mwema ilipotaka kujua jinsi ya kupata nakala ya ripoti hiyo aliambiwa kuwa haipatikani bure; kwani imegharimu jasho na muda mwingi wa wachunguzi wa timu hiyo na hivyo wanawapatia wale ambao watachangia kiasi chochote kuanzia dola 30 za Marekani (zaidi ya Sh 30,000) ili kufidia sehemu ya gharama hiyo.
"Tumetumia karibu mwezi mmoja kufanya kitu ambacho kilitakiwa kufanywa na wabunge wetu na watumishi wa serikali yetu; sisi si matajiri kama wao na hatuna raslimali kama za kwao, hivyo katika hali kama hii tunaomba mchango kidogo japo kufidia ile gharama tuliyoingia kwani kujua nako kuna gharama" alisema mdokezaji huyo ambaye alisema kuwa wameandaa nakala 100 tu ambazo hadi jana Jumanne karibu nusu ya nakala zilikuwa zimeshanunuliwa kabla ya kusambazwa.
Imefahamika kwamba baadhi ya watu ambao wanataka kuiona ripoti hiyo ni pamoja na wabunge kadhaa, wakuu wa taasisi za haki za binadamu na Watanzania wengine wa kawaida.
Raia Mwema limedokezwa kwamba, waandaaji wa ripoti hiyo wameshawahi kuandaa mambo mazito zaidi ya kimataifa, baadhi yakiwa na maslahi ya Taifa la Tanzania ikiwa ni pamoja na lile sakata la rada ambalo hadi leo halijapatiwa ufumbuzi na serikali.
Katika sakata la rada, kundi hilo la Watanzania lilifanikisha kuandika barua kwa wabunge wa Uingereza Norman Lamb na Claire Short kuhusu kashfa hiyo ya rada.
Sehemu ya barua hiyo ilisomwa kwenye Bunge la chini la Uingereza na Mbunge Lamb na kuchochea mjadala mkali juu ya Rada kiasi cha kusababisha siku chache baadaye Rais Jakaya Kikwete kulizungumzia suala hilo na kuahidi kuwa kama serikali itakuwa imedhulumiwa katika bei ya rada basi serikali "itaidai serikali ya Uingereza kwani kampuni ya BAE ni ya serikali".
Kashfa ya Meremeta imekuwa ikiisumbua serikali kwa muda mrefu sasa na imeshindwa kutekeleza mapendekezo ya Kamati ya Rais iliyoongozwa na Jaji Mstaafu Mark Bomani, ambayo ilipendekeza kukaguliwa kwa kampuni hiyo.
Taarifa ya awali ya wakaguzi waliokagua BoT, Juni 2006, ziliibua sakata hilo la Meremeta pamoja na kashfa nyingine lakini haikuweza kufahamika ripoti hiyo ya wakaguzi ilivyoyeyuka na kutoanikwa hadharani kabla ya wakaguzi wengine wa nje kuibua suala la EPA pekee miongoni mwa uchafu mwingi ndani ya BoT na serikalini.
Taarifa hiyo ya wakaguzi ilibainisha kwamba serikali ilitoa fedha hizo kiasi cha Sh. bilioni 155 kwa njia ya dhamana ya hazina ambayo inatakiwa kulipiwa riba ya asilimia 14.92 kila mwaka lakini hakukua na makubaliano yoyote rasmi kati ya Serikali na Meremeta hali inayoibua zaidi utata na kuonyesha hakuna njia yoyote ya kuweza kuzipata fedha hizo.
Imeeleza kwamba ripoti hiyo inafuatia kile ambacho kilichukuliwa kama tishio lililotolewa na mmoja wa wanachama wa mitandao hiyo kuhusu kuanika siri ya Meremeta.
SOURCE: Raia Mwema
Siri za Meremeta kwenye mtandao
Mwandishi wa Raia Mwema
Julai 29, 2009

Last edited by a moderator: