Mkuu Wilaya ya Handeni Albert Msando amepotoka

May 11, 2023
4
4
Inashangaza na kustaajibisha DC Albert Msando kutushikilia wachimbaji wadogo ili tusulubishwe na mwekezaji mwenye leseni ndogo ya uchimbaji ndugu Godfrey Bitesigwire...

Mkoani Tanga Wilaya ya Handeni katika machimbo ya dhahabu kijiji cha Kwa ndege pamekuweko na mgogoro wa muda mrefu kati ya wachimbaji wadogo na mmiliki wa leseni ndogo ya uchimbaji ndugu Godfrey Bitesigwire ni aina ya mgogoro unaojirudia mara kwa mara kutokana na mwenye leseni kuwa na tamaa na ubinafsi kwa kutaka kuteka na kutaifisha mashimo ambayo yanakuwa yamechimbwa na wachimbaji wadogo kisha yakafikia hatua ya uzalishaji mkubwa, kwa awamu tatu mfululizo amefanikiwa kuteka mashimo hayo na kwa kila awamu alikuwa akitufukuza wachimbaji wadogo eneo husika na kisha kutupangia eneo jingine kwa ahadi kuwa hatotuamisha tena

Katika awamu hii ya nne imetukuta chini ya DC wetu nguli wa Sheria kijana machachari ambae baadhi ya watu kama GENTAMYCIME walidiriki kumtaja kama 2025 prime minister material ila katika hili anachemka kwa nguvu ya rupia iliyomfikia mezani, tembelea katika ukurasa wake wa Instagram hutakuta popote akizungumzia juu ya mgogoro unaoendelea eneo hili la machimbo na katika vikao vyake vyote na wachimbaji huwa anapiga marufuku yoyote kurekodi chochote kinachoendelea kuhofia maamuzi yake na lugha zake vitisho kuufikia umma wa Watanzania...

Katika mgodi huu na migodi mingine karibu yote yenye leseni za uchimbaji mdogo wachimbaji wenzangu mtakubaliana na mimi huwa hamna mikataba yoyote ya kimaandishi zaidi ya mikataba ya maneno na hii ndiyo tuliyoifanya na mwenye leseni hii ndugu Godfrey Bitesigwire mwaka 2021 hadi leo tumeendelea kuchimba na mgawayo ukipitishwa kwa pande zote bila ya shida yoyote isipokuwa shida hujitokeza pale ambapo mwenye leseni anapochukua hatua za dhulma kutuondoa katika eneo moja kwenda jingine bila ya fidia ama kuruhusu tuvune mwamba tulioutafuta kwa nguvu na jasho letu hadi mwisho...

Katika eneo la 4 tulilopewa na mwenye leseni mnano mwaka 2022 mwaka huu april alidhamiria kutufanyia dhulma kama ilivyo ada yake baada ya sisi wachimbaji wadogo kugundua mwamba mkubwa wa dhahabu na wa kudumu hivyo tarehe 29 April 2023 alitoa agizo kuwa ifikapo tarehe 1 may. 2023 wachimbaji wote wadogo tuwe tumeondoka eneo lile na tuyaache mashimo yote bila kujalisha yanazalisha ama laa na akaahidi atatupeleka eneo jingine tuchimbe bila bughudha ila lile tumwachie yeye achimbe tulijichanga na kwenda ngazi zinazofuata ikiwemo kwa afisa madini wilaya, mkoa yaan RMO na kwa DC Albert Msando ambapo tulipewa barua tumpelekee Bwana Godfrey Bitesigwire kusimamisha zoezi hilo la kutaka kupokonya eneo lile...

Ila cha kushangaza ilipofika tarehe 1 may 2023 jioni bila ya taarifa yeyote mwenye leseni alileta tinga tinga na kuanza kufukia maduara yote yaliyokuwepo eneo lile bila ya kufanya ukaguzi maduarani ama kutoa taarifa watu waliopo chini shimoni wapande, ni dhahiri kuwa tajiri huyu alidhamiria kuyatoa kafara maisha ya wachimbaji wenzetu ila kwa nguvu ya umma na kuhofia kuwa kuna baadhi ya watu pengine wamefukiwa chini wananchi walijitokeza na kuzuia tinga tinga lile lisiendelee kufukia mashimo yale na juhudi za uokoaji zikaanza japo watu wake walizuia shimo lolote lisifukulie kuokoa chochote kilicho ndani na mpaka hapo yalikuwa yamefukiwa mashimo nane....

Tulizunguka ktk kila ofisi husika za madini hadi kufikia hatua ya DC kukubali kuja eneo la tukio kushuhudia ukatili huo kwani mara nyingi alipendelea tumfuate ofisini jambo lililokuwa changamoto kwetu kutokana na gharama za usafiri na malazi cha ajabu alipofika eneo la tukio hakutoa tamko lolote la kumkemea mwekezaji kwa kitendo cha kuhatarisha maisha ya watanzania na wachimbaji kwa kufukia mashimo bila kufanya ukaguzi, kutoa notice ama kumkemea mwekezaji kutotii tamko la serikali alilopewa kimaandishi kutochukua hatua yoyote kuwaondoa wachimbaji wadogo bila ya maridhiano ya pande zote mbili...

Ila cha ajabu alitoa lugha ya vitisho ni kwanini tunasema chini kuna watu wamefukiwa licha ya kwamba mazingira ya ufukiaji hayakufata taratibu zozote za kiusalama pia alituasa kuwa hatuna mkataba wowote wa kimaandishi na mwenye leseni hivyo tuwe wapole atatumia busara zake kumuomba eneo dogo katika vitalu vyake nane ambapo tutapewa tuchimbe kwa uhuru pia alitupa siku 90 tu ambazo tungetumia kufukua wenyewe maduara yaliyofukiwa na kuvuna mwamba ule tulioutafuta kwa muda mrefu kisha tuondoke tuliache eneo lile ifikapo tarehe 6 julai 2023 pia aliunda kamati ndogo ya wachimbaji ambayo atawakutanisha na mmiliki wa leseni ili kuweza kutatua mgogoro ule...

Vikao chini yake vilifanyika bila ya mafanikio ya kupata maridhiano pia wakati huo huo mwenye leseni alipenyeza fitna nyingi ilimradi tu apunguze zile siku 90 tulizopewa za kazi hakutaka suluhu ila alitaka tumpishe ilihali alituruhusu yeye mwenyewe na siku zote amekuwa akichukua mgao wake bila ya shida yoyote ambao kwa kila roba 10 za mawe yeye huchukua roba 5 na tano zinazobaki tatu ni za wenye duara na mbili zilizobaki ni za waponchaji kinyume na utaratibu ambapo alipaswa achukuwe roba tatu tu...

Baada ya usuluhishi kumshinda DC alitufumbua macho kuwa kuna ngazi nyingine zaidi yake tujaribu huko na ndipo tulipoamua 24/04/2023 kumuandikia barua waziri wa madini na nakala tukatuma ktk ofisi nyinginezo

Mheshimiwa waziri alisikitishwa sana na dhulma zilizotendeka kwa muda mrefu na akaahidi atalifanyia kazi baada ya kupokea taarifa toka ngazi za chini hivyo akatuma tena nakala kwa DC na RMO ili wafatilie huo mgogoro na wamtumie taarifa...

Alitutembelea afisa madini mkoa Bi Zabibu Anga na kuitisha kikao kati ya viongozi wetu na wenye leseni ambapo alihitimisha kikao hicho kwa kauli ya kuwataka wenye leseni kutulipa fidia ili tuondoke maana kwa miaka mitatu wametukaribisha na kutugawia eneo la kuchimba na kwa kipindi chote hicho hakukua na ripoti iliyotolewa ya uvamizi wa eneo leo na walichukua migao yao bila shida na zaidi ya yote katika kila shimo lililochimbwa waliongezwa wanachama hewa wanne toka upande wa mwenye leseni ambao hawahusiki na chochote ktk harakati za utafutaji wa mwamba ila katika uzalishaji wanachukua mgao sawa na wale tuliovuja jasho hivyo ni dhahiri palikuwa na makubaliano pande zote

Ila ghafla juzi tarehe 05/06/2023 jioni tulipata taarifa kuwa DC Albert Msando ametuita wachimbaji wote katika ofisi za kijiji ambacho kipo mbali na eneo la mgodi na ingelazimu kulipa nauli ya boda boda kati ya elfu 12,000 hadi 15,000 na ni kutokana na hali ya mvua zinazoendela huku hivyo kufanya boda boda kupandisha nauli kutokana na ubovu wa njia...

Kwa kweli hili lilikuwa ni pigo kwetu kwani kuna idadi ya mashimo 67 ambapo kila shimo kwa idadi ya chini
kabisa ya wanachama ni 10 ambapo kwa mashimo 67 tuna idadi ya wanachama 670 na katika hayo mashimo 67 yenye uzalishaji hayazidi 10 hivyo wengi wetu wapo katika hali duni kifedha hivyo kutokana na gharama za nauli wanachama waliofanikiwa kuhudhuria tulikuwa 17 pamoja na viongozi wetu tulikuwa 30....

Katika kikao DC Albert Msando alianza kwa kusoma barua tuliyoituma kwa waziri ambayo ni mwezi na siku kadhaa sasa tokea apate nakala ya barua hiyo na baada ya kuisoma.....

I) alituangushia lawama wachimbaji kwanini tumeenda hatua ya mbele na kumruka yeye na kusahau yeye ndiye aliyetushauri tuende mbele

II) Alitutishia kuwa tunamuharibia kazi kwa kumtuhumu mwenye leseni kwamba anazalisha zaidi ya kg 30 kwa mwezi ilihali yeye ana taarifa kwa kipindi chote cha miaka mitatu ndugu Godfrey Bitesigwire amezalisha kg 12 sawa na 10g kwa kila siku. Jambo lililotushangaza sana kwani tulitegemea angeunda tume kufanyia uchunguzi tuhuma hizo kama ni za kweli ama laa kisha achukuwe hatua stahiki baada ya kuujua ukweli

III) Pili ametutuhumu kuwa tumeuza dhahabu kidogo sana katika soko la dhahabu na kusahau kuwa dhahabu yote inayopatikana inanunuliwa na mwenye leseni na yeye ndie anaehusika kuipeleka soko la serikali ama kuitorosha

IV) Amekasirishwa na kitendo cha kumtuhumu mwenye leseni kuwa anatudhumu katika mgawanyo wa mawe.
Jambo lililotuacha midomo wazi kwani mwenye leseni hashiriki gharama yoyote zaidi ya kuchukua migao yake ambayo hata mifuko anayojazia mawe ni ya kwetu ambapo wakati mwingine akijisikia hurudisha gharama za mifuko ama asipojisikia hatulipi pia mizigo yote ni sharti isagwe katika karasha zake ambazo hutusagia kila roba tatu kwa shs elfu 25000 badala ya elfu 10,000

V) Ametueleza kuwa hatuna mkataba wa maandishi hivyo ni haki ya mwenye leseni kuchukua hatua zozote dhidi yetu jambo lililotushangaza pia kwani yeye ni mtu wa kati na hili jambo lipo chini ya tume ya madini na kinachohitajika ni utatuzi wa mgogoro na si kutufurumusha na kutukandimiza

Ndugu Godfrey Bitesigwire ni mtu anaeumiza wanyonge bila ya huruma kuanzia vibarua wake katika mashimo yake hadi wachimbaji wadogo aliotutengea maeneo tuchimbe ni vyema mtu huyu akafatiliwa kwa karibu na kuchunguzwa pia kwani inasemekana kutokana na utajiri wake alioupata kupitia jasho letu ana nguvu kubwa serikalini kiasi cha kuwanyamazisha viongozi mbalimbali hadi katika ngazi ya mawaziri

Mwisho baada ya kutulaumu kwa kumtuhumu mwenye leseni mheshimiwa DC Albert Msando alihitimisha kwa kututaka wachimbaji wote wadogo tuondoke eneo la mgodi hadi katika makazi tunayoishi kwa siku mbili na ifikapo ijumaa akija akute miti na ndege tu vinginevyo yatatumika mabomu na nguvu kutuondoa mpaka sasa watanzania wanyonge sisi hatujui tunaelekea wapi tutakapopata makazi ya amani ndani ya Tanzania bila ya kufukuzwa kama wanyama. Kwani tokea ijumaa tulipata taarifa kuwa mwenye leseni analazimisha itolewe stop order katika machimbo haya na haikupita hata wiki tokea tupate habari hizo Jana mheshimiwa DC Albert Msando si kutusimamisha tu katika machimbo Ila hataki hata kutuona tukiishi japo pembezoni mwa eneo hilo

Rai yangu naomba yeyote anaeweza afatilie jambo hili kwa undani ili kupata ukweli wa yote niliyoandika ikiwezekana kufika eneo la tukio wachimbaji tutatoa ushirikiano wa dhati na yeyote mwenye chombo chochote cha habari atutembelee na kupata kujionea na kuufahamisha umma yanayoendelea hapa. Pascal Mayalla

Asanteni
 
Back
Top Bottom