Meremeta 00:00:00. EXTRA

Status
Not open for further replies.
MKJJ,mie nimekaa mkao wa kula,ninamwomba Mungu kesho ifike salama! Kesho Laptop yangu hagusi mtu,nasubiri mwali atoke.Kila la heri wewe na team yako.
 
Na sasa tumeizunguka Yeriko!
Si kwa nguvu ya majeshi
Au kwa utaalamu wa vita
Bali kwa barugumu ya mashujaa
Watangazo ukweli!

Wale wapigao panda bila kukoma
Wasimamao nje ya kuta za Yeriko
Ambako ndani yake ufisadi umesimama!
Na mashujaa walio ndani kama Rahabu
Na wao wataweka alama za kuupenda ukweli
Nao hawataangamia!

Hii basi ni mbiu
Mbiu ya mwanzo wa mwisho wa Yeriko ya leo
Ule unabii wa kuanguka kwa Yeriko
Utaanza kutimia; kwani ni masaa machache yajayo
Sauti za matarumbeta ya walioizunguka Yeriko yatapigwa

Na kuta ngumu zilizojengwa kwa miongo minne
Zitaanza kutikisika; Naam! Zitatikisika kama zile za Yeriko ya kale

Waambie! tumeizunguka Yeriko!
Ambako himaya ya ufisadi imejikita
Na utamaduni wa kifisadi unatawala!

Nayo Yeriko ya leo itaporomoka;
utawala wa kifisadi utakoma!
Kwa wale walioko ndan ya Kuta za Yeriko
"tokeni mkatengwe naye!"

Na. M. M. Mwanakijiji
 
Na sasa tumeizunguka Yeriko!
Si kwa nguvu ya majeshi
Au kwa utaalamu wa vita
Bali kwa barugumu ya mashujaa
Watangazo ukweli!

Wale wapigao panda bila kukoma
Wasimamao nje ya kuta za Yeriko
Ambako ndani yake ufisadi umesimama!
Na mashujaa walio ndani kama Rahabu
Na wao wataweka alama za kuupenda ukweli
Nao hawataangamia!

Hii basi ni mbiu
Mbiu ya mwanzo wa mwisho wa Yeriko ya leo
Ule unabii wa kuanguka kwa Yeriko
Utaanza kutimia; kwani ni masaa machache yajayo
Sauti za matarumbeta ya walioizunguka Yeriko yatapigwa

Na kuta ngumu zilizojengwa kwa miongo minne
Zitaanza kutikisika; Naam! Zitatikisika kama zile za Yeriko ya kale

Waambie! tumeizunguka Yeriko!
Ambako himaya ya ufisadi imejikita
Na utamaduni wa kifisadi unatawala!

Nayo Yeriko ya leo itaporomoka;
utawala wa kifisadi utakoma!
Kwa wale walioko ndan ya Kuta za Yeriko
"tokeni mkatengwe naye!"

Na. M. M. Mwanakijiji

Amen!

Nimetoka bafuni mbio mbio...(thanks to RSS feed)
 
As we have promised.. we are rolling! Here we come. Wote ambao wameshachangia, u'll get ur copy b4 the end of the day (US time). Kutokana na ongezeko kubwa..tunafikiria kuongeza nakala chache kufuatia mwitikio wa leo hasa baada ya baadhi ya magazeti kuchapa habari za ripoti hii.
 
Mkuu nimeskia asubuhi kwenye uchambuzi kuna kitu kimetolewa na Raia Mwema kama sikosei kina husu kijarida hiki mkuu jaribu kufuatilia wanaweza wakawa wametumbukiza nyongo tayari.
 
Mkuu nimeskia asubuhi kwenye uchambuzi kuna kitu kimetolewa na Raia Mwema kama sikosei kina husu kijarida hiki mkuu jaribu kufuatilia wanaweza wakawa wametumbukiza nyongo tayari.

usiwe na wasiwasi!!!!! mwenye kukosa ndiyo keshakosa!
 
Meremeta 00:00:00..
Mzee Mwanakijiji
user_offline.gif
24th July 2009, 05:48 AM

- Tarehe 24th July 2009 - siku serikali na mafisadi walipo-freeze!

- Wiki ya tarehe 24th july - to this date 29th july, bado the freeze goes on huko ndani!

well Mkulu MMJ you are the man na I am down, p/s watch your back maana kuna mengi sana kwa nyuma na hii kitu.

May God bless you na A luta Continua!, Mungu Aibariki Tanzania!

Respect & Out!

Field Marshall Es!
 
Babu yangu mwanakijiji, uchanguzi unakaribia, je hauoni ni haki ya kila mtanzania kujua nini serikari iliyokuwepo zaidi ya miaka 30 imekilea? watu tuchangie kwa kujitolea kwa kazi yako nzuri uliyoifanya ila wape haki kila mtanzania kujua nini kinaendelea. Maana kila mmoja wetu tunauwezo wa kubadilisha kainchi ketu cha Tanzania, iwe kwa njia ya kuchagua raisi na chama tawala au kujitoa muhanga wa ajili ya maendeleo ya kila mtu na watu masikini.

Naelewa unaitaji kurecover cost ila pia watanzania wangapi hasa wapiga kura wenye uwezo wa kubadirisha raisi wa nje wanaweza kuafford?
Ukiwa na maksai wanne ni muhimu kuwapa mahitaji yao muhimu ili kuwawezesha waendelee kukulimia mashamba yako. Usipofanya hivyo, msimu ujao utakupita na kuishia kupata kijunia kimoja cha mahindi au mchele kwa kutumia jembe la chapa jogoo badala ya plao!

Ukiwa na ng'ombe aliyebahatika kuwa anatoa maziwa galoni 2, ni sharti uwekeze nguvu zako kwa kumlisha majani mengi, hata kumpatia jiwe la chumvi na mashudu. Usipofanya hivyo ndama wako atanyaukiana kwa kifaduro na vitumbua utakula kwa chai ya strungi!!
 
Hakika wewe ndiwe yule tuliyekuwa tunakungojea baada ya Kuondoka Nyerere, Natafakari nikuite jina gani, hakika wewe ni MZALENDO kwa maana ya UZALENDO halisi na si uzalendo wa kujibatiza, huhitaji kujiita MZALENDO acha tukuite MZALENDO kwa maana twajua pasi na shaka wewe ni MZALENDO

MUNGU AKULINDE NA AKUZIDISHIE MOYO WA UPENDO KWA TAIFA LAKO TANZANIA!
 
Na sasa tumeizunguka Yeriko!
Si kwa nguvu ya majeshi
Au kwa utaalamu wa vita
Bali kwa barugumu ya mashujaa
Watangazo ukweli!

Wale wapigao panda bila kukoma
Wasimamao nje ya kuta za Yeriko
Ambako ndani yake ufisadi umesimama!
Na mashujaa walio ndani kama Rahabu
Na wao wataweka alama za kuupenda ukweli
Nao hawataangamia!

Hii basi ni mbiu
Mbiu ya mwanzo wa mwisho wa Yeriko ya leo
Ule unabii wa kuanguka kwa Yeriko
Utaanza kutimia; kwani ni masaa machache yajayo
Sauti za matarumbeta ya walioizunguka Yeriko yatapigwa

Na kuta ngumu zilizojengwa kwa miongo minne
Zitaanza kutikisika; Naam! Zitatikisika kama zile za Yeriko ya kale

Waambie! tumeizunguka Yeriko!
Ambako himaya ya ufisadi imejikita
Na utamaduni wa kifisadi unatawala!

Nayo Yeriko ya leo itaporomoka;
utawala wa kifisadi utakoma!
Kwa wale walioko ndan ya Kuta za Yeriko
"tokeni mkatengwe naye!"

Na. M. M. Mwanakijiji
umenigusa roho yangu,Yeriko imebomoka!!!!
Ndikupasya Buno Malafyale anganile Kangi ambokile!!!
 
Mwanakijiji,

Mimi dola 30 zangu ziko njiani (hewani) kuja kwako. Nataka niwe miongoni mwa wale wenye copy hii. Ikifikia hatua ya kuisambaza bure pale jangwani na mnazi mmoja, nitakuwa miongoni mwa paper nuts......IYWI

KAKA MMKJ. Nakupongeza sana.
Naomba niungane na wengine kupongeza kazi nzuri hiyo, lakini kwa taarifa ya Gazeti la Raia Mwema sasa wahitaji wataongezeka na ipo haja ya kuongeza nakala zaidi kutoka 100 hadi kufikia 200 najua linawezekana na wahitaji watafikia huko.

Mimi binafsi nimezungukwa na watu watatu hapa wakihitaji nimejaribu kuwa FFW email ya utaratibu wa kupata ili wafuate maelekezo.

Tayari watu wajiitao kwa sasa 'WALIMU' wameingia darasani kutaka kufuatilia ripoti hiyo mimi niko tayari kuisambaza bure katika mitaa yangu usukumani ikibidi kufabnya hivyo hata kama kamata kamata itaanza.
 
Mkuu,
R the copies sold out?

Very, very good work. I have a copy of Tanzania Daima with me and the report made front page.........i think things have started heating up? :)
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom