- Mkuu u-clean wa Mengi sidhani kama ni hoja hapa. Inawezekana yeye ni dirty kuliko hata hao waliopo serikalini. Aliyomsea mimi nayachukulia kama ni pre emptive strikes, may be anajua zaidi alichofanya na anaona mwelekeo ulipo unaweza kumfikia na yeye. Tofauti ni kuwa yeye hayuko serikalini moja kwa moja, nilikuwa najaribu kuzungumzia wale waliomo serikalini hasa vijana ambao tuliamini kama wanaweza kuwa msaada mkubwa kwenye kurekebisha mambo. Sasa inasikitisha kuona kuwa hawafanyi tuliyotarajia isipokuwa wanafanya kinyume, kumbambikia mtu kesi, kumbambikia mtu kodi ni siasa za kijinga sana, ndio maana kama ukiona post ya kwanza nilisema KAMA NI KWELI, kitu ambacho sitaki kuamini, na nimerecall events na kauli za siku chache zilizopita. KWa hiyo hapa siko in offense ya mtu fulani au defence ya mtu fulani.