Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
Phew, now i'm free. Thanks Invincible 😉

Well, i'm not a big fan of neither Mengi nor Masha, but i really don't think the national debate should be clouded by who wants to do what to Mengi. I think this is the n-th time (n being any number greater than 1) that Mengi has called a press conference to let us know that someone is after him......and i don't think this was the last time.

However, when it comes to "WAZIRI KIJANA" who is ploting against Mengi, only one name comes to mind and that's not MASHA but rather MALIMA. We all remember the controversy surrounding MALIMA during parlieamentary inquiry into Mengi-Manji rivarly, and how Malima was "influenced" to become the mouth-piece and ardent supporter of FISADI Manji. I bet the culprit in this issue is MALIMA, but i may be wrong.
 
Vyombo vya habari naomba kupitia safu hizi za JF amulikwe kisawasawa huyu kijana Waziri. Maskini akipata ****** hulia mbwata...hayo ndio yaliomkuta Masha. Amepewa madaraka makubwa na kuiba mapesa ya kifisadi hivyo kauli zake zinakuwa za utata. Kwa mfano yale ya Albino alivyohojiwa na BBC- ni ishara tosha kuwa huyu hafai kwa nafasi nyeti aliopewa. Namheshimu JK ila kwa hili amwondoe kabisa kwenye nyazifa hizi.
 
Mimi naona nayumba tu kama wengine wanavyo yumba humu ndani kuhusu hii ishu.
Naweza kuamini kuwa wanao mtetea Masha wana masrahi naye binafsi.Kama ametuhumiwa kwa nini umtetee mwite aje au naye atoe utetezi wake.
Huyu Masha si ndo hata kule kwenye tunako jing'ata ulimi anatajwa tajwa sana kule ni kweli watakuwa wanamwonea?

....na pia mtu aliye objective anaweza kusema kuwa wewe na mwingine yeyote anayemshambulia huyu Masha pia mna "masrahi" dhidi yake.
 
Phew, now i'm free. Thanks Invincible 😉

However, when it comes to "WAZIRI KIJANA" who is ploting against Mengi, only one name comes to mind and that's not MASHA but rather MALIMA. We all remember the controversy surrounding MALIMA during parlieamentary inquiry into Mengi-Manji rivarly, and how Malima was "influenced" to become the mouth-piece and ardent supporter of FISADI Manji. I bet the culprit in this issue is MALIMA, but i may be wrong.

Mh. Malima si "WAZIRI KIJANA" bali ni "NAIBU WAZIRI KIJANA". I therefore guess it can't be Hon Malima.
 
Mh. Malima si "WAZIRI KIJANA" bali ni "NAIBU WAZIRI KIJANA". I therefore guess it can't be Hon Malima.

...in swahil semantics and owing to general logic, you may call a Naibu Waziri simply Waziri, especially kwa jinsi Mengi anavyojaribu kutuchanganya akili. But you maybe right.
 
hili la ulevi wa Masha nami nimelisikia kutoka kwa watu wazima (very credible)-mwanza wanalalamika mno kwa ulevi na dharau kwa wapiga kura wake!!!!
 
Naomba kutoa mchango wangu wanabodi;

Sioni shida kwa bwana Mengi kusita kutaja jina but he went further kusema kuwa ni waziri wa wizara nyeti. Wizara nyeti zinajulikana kwa mtazamo wangu kuwa ni pamoja na Wizara ya fedha, maji, kilimo, ardhi, miundombinu na mawasiliano, ulinzi, mambo ya ndani, madini, na maliasili. kama kuna ambazo nimemiss nisaidieni. Nikajiuliza ni nani hao? kwakuwa amesema waziri kamili basi nikajiuliza ni nani? Mawaziri vijana ktk hii awamu nchimbi, masha, ngeleja, malima na mwinyi. Sijawahi kusikia mmoja kati ya hawa wakipinga hata kwa maneno ufisadi but wapo waliohusishwa kwa namna moja ama nyingine. Kwa hio inawezekana.

Nikiangalia mtindo wa uandikaji wa Thisday,kulikoni na Nipashe,the gurdian naona kuna utaofauti mkubwa sana katika managing policies zao. IPPMEDIA na Media Solutions ni vitu viwili tofauti na sina hakika kuhusu umiliki. Naamini mtakubaliana nami kuwa IPPMEDIA is still a one of powerfull and popular media in the country. Mengi kama Mengi still popular and respected person. Hili ukibisha ni shauri yako but that is reality na hata Muungwana anajua hili. Kitendo cha mengi kulalamika naona ni kama ametoa tahadhari na kuonyesha ni jinsi gani watu wamekuwa wavivu wa kufikiri. Nilishawahi kufanya kazi kwenye moja ya project za Mengi. Nakubali kuwa Mengi ni mtu makini na pro active katika biashara zake. anachokizungumza ni kweli kipo kwa jinsi anavyoona na kama tutakuwa ni watu makini. tufanye kazi yetu inayotakiwa kama baadhi yetu tunavyofanya.

Mengi akisema fulani na mwenye dhamana ndo kasema nchi itayumba. Sina maana kuwa tuwalinde waovu ili niwe sehemu yao but busara inatakiwa but lazima tuchukue hatua. Just imagine hawamafounder wa JF tukigundua nao ni mafisadi hivi hapa patakuwa hivi? Just imagine kwa heshima alionayo mengi leo aseme Sitta anamhujumu, au Slaa aseme Zitto ni kibaraka patakalika kweli? Yakitokea nanunua bastola. Hapa hofu na kukata tamaa bado tu?

Kumsema moja kwa moja nahisi ni mapema mno. inawezekana yule tusiemdhania ndo yeye. kwa mtazamo wangu mwenyewe atajieleza tu muda si mrefu. najua ni mmoja kati ya hawa vijana na pia kwa kuwa wanafikiri wanahati miliki ya mamlaka basi wajue wamekosea.

Kama serikali yetu ipo makini, Mengi angeitwa kwa mtu ambaye yeye anamwamini e.g. Muungwana hata Pinda na kumueleza each and everything then hatua zichukuliwe but nahisi hili litapuuziwa na hata kama ni kuchunguzwa ili ukweli ujulikane na mwenye haki apewe. inawezekana imani yetu hata kwa mengi inaondoka na kwa namna moja ama nyingi discipline itakuwepo.
 
Yote haya yanadhihirisha utendaji kazi wa Kikwete. Anajali urafiki kuliko nchi. NO wonder marafiki wake wa karibu (wana mtandao) bado wanapeta mtaani huku akijisifia kuwa anashughulikia mafisadi.


He is a coward!



Hapo ndipo Mengi anapotofautiana sana na watanzania wengi! Yuko tayari kugombana na yeyote anayemgusa! With all his 'weaknesses' nadhani huyu kwenye vita ya ufisadi ni one of the leaders - we cannot ask for more from this one person.

Kwa upande wa waziri - this is the problem ya kuwatunukia watu uwaziri bila kuwafahamu (vet) vizuri! Kila siku JK ataishia kukuna kichwa! - Still learning how to pick the right people for ministers! Kazi tunayo!


Hoja yako imeshiba



.
 
Nafikiri kukata mzizi wa fitina ni nafasi nzuri ya media kuwahoji wotete wawili ili watoe kilicho ndani za nyoyo zao na wakikataa kutoa maelezo tutapima wenyewe na kujua nini kinaendelea.Pia huu ni wakati mzuri wa viongozi wetu kupima kauli zao wanazo zitoa kwani wameona ile kauli ya kusema hata kama mkila majani ............ itanunuliwa tu njinsi iliwaudhi wananchi sana na wakapiga kelele sana na sasa ndio zamu ya kuadhirika hapa hapa duniani kwa wale waliotoa kauli za kudhalilisha wananchi.
 
Ninavyokumbuka huyu jamaa ni mhusika mkuu kwenye TANGREEN. Ila sina hakika kama ana connection na akina BPM na DY. Hata hivyo inawezekna ni maandalizi kwani hata yeye anaweza kuwa na taarifa kwamba naye ndiko anakoelekea. Mwenzio akinyolewa.... So alikuwa anaandaa kichwa kwa ajili ya kinyozi.

Ok kumbe ndio imekaa hivi! Thanks
 
Jakaya toka aingie madarakani uteuzi wake umezingatia zaidi kulipa fadhila na hiyo sio good governance. Masha aliingizwa kwenye madaraka kwa mtindo huo huo; alijitolea kampuni yao ya uwakili kutumiwa kuiba fedha BOT na ndio maana partner mmmoja ameukwaa ujaji na huyu akapewa kwanza deputy na sasa full ministerial post. Kama vetting ingekuwa inafanyika kwa watu wanaoteuliwa kama zamani huyu kijana asingeteuliwa kwa sababu ya historia yake ya kifisadi huko alikoajiliwa kwenye kampunni TOL. Kampuni hii ilikuwa ya kwanza kuwa listed kwenye DSM stock exchange lakini kumbe ilikuwa mufilisi na wakati huo Masha alikuwa Secretary wa hiyo kampuni!! Above all alijipa mshahara mkubwa bila idhini ya board na hata akajaribu kuiibia kampuni nyumba na kesi ikafika Commercial court ambapo hukumu ya his Lordship Judge Harold Nsekela aliamua in favour of TOL!! Sasa hawa mafisadi ndio wengine wanawaita role models wa vijana; huyu kijana has attributes zote mbaya ambazo tusingependa vijana wa generation ya dot com wawe nazo namely:- corruption na Promiscuity which was openly displayed in the now banned " UTAMU" blog.Unfortuantely, Jakaya does not know that people like Masha in his cabinet are not loyal to him but to disgraced Lowassa and the sooner he disbads the Lowassa MAFIA the better for his legacy and the country. I hope wapambe na Ridhwani mtamfikishia muungwana message hii othrwise he is bound to regret not in the very distant future.
 
The original post with commentary by Mwanakijiji is highly prejudicial and has tainted the flow of the discussion on the substance of the press release. Mr. Mwanakijiji should offer more grounds for his assertion that the man in question is Masha or should retract the statement.

We have censored the original nota bene.
 
...in swahil semantics and owing to general logic, you may call a Naibu Waziri simply Waziri, especially kwa jinsi Mengi anavyojaribu kutuchanganya akili. But you maybe right.

anaweza kutajwa rais kijana wa nchi fulani kisha ikawa ina maana makamu wa rais.
Kama ilikuwa inamaanisha naibu waziri basi ni makosa .
 
Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi amekutana na waandishi wa habari na kusema mambo mengi na baadaye kutoa tamko lifuatalo.


TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI


Hivi karibuni waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti alipendekeza nibambikiziwe kodi bandia ya kiasi kikubwa nitakachoshindwa kulipa na hatimaye nifilisiwe kama njia pekee ya kuninyamazisha kabisa eti kama alivyofilisiwa tajiri mmoja mkubwa huko Urusi.

Alidai kwamba vyombo vyangu vya habari vimekuwa mno mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.

Nilitegemea waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi. Angalao angefahamu kwamba anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na siyo mmiliki wa vyombo vya habari.

Kama mkiristo na kama alivyoagiza Bwana Yesu namsamehe kwa vile hajui atendalo. Baada ya kumsamehe ningetaka ajue yafuatayo.

Asiyekemea maovu katika jamii, yeye ni sehemu ya maovu hayo. Waziri huyu na wale wote ambao wamekwishanitumia vitisho wakumbuke kwamba hata kama watafanikiwa kuvinyamazisha kwa hujuma zozote zile, vyombo vyangu vya habari, na hata kama mimi sitakuwepo tena, moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za wanajamii hauwezi kuzimika kamwe.

Ieleweke pia kwamba sauti za maskini na wanyonge katika jamii hazisikiki kwa urahisi. Vyombo vya habari husaidia kupaaza sauti na vilio vyao katika vita dhidi ya maovu. Ni wajibu wa kila mtu aliye na uwezo kusema kwa sauti kubwa kwa niaba ya wanyonge na maskini ili kutokomeza ufisadi.

Nachukua fursa hii kumpongeza sana Rais wetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuguswa na sauti na vilio vya wanyonge na maskini wa Tanzania kuhusu ufisadi na hatua za kijasiri zinazochukuliwa na Serikali yake dhidi ya ufisadi. Sisi sote ni lazima tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa ujasiri, nguvu na hekima nyingi wakati huu wa majaribio makubwa.




____________________
Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
3 Desemba,2008

1. Naungana mkono na Capo di tutti capi wangu kuwa hapa hapajakaa sawa. Mengi mwenyewe, kwa hiari yake, ameamua kuleta hizi habari kwenye public forum. Amesema ushahidi anao wa hayo anayosema. Sasa kwa nini asite kumtaja mhusika na abakie aki-drop heavy hints(kijana, wizara nyeti, msomi sana, wink,wink,wink!) kuwa ni fulani? Ataogopaje libel wakati anasema ushahidi anao? Angefanya kama alivyofanya Slaa au hata Kikwete ( kuhusiana na Gama alipogombea mara ya kwanza) angejijengea heshima zaidi. Kwa kufanya alivyofanya kunazidi kuthibitisha kuwa yeye ni mlalamishi tu anaependa kulia kulia ili aonewe huruma na jamii.

2. Kama mmisheni mwenzake naamini kuwa alichofanya si kile ambacho kiongozi wetu alituambia tufanye. Kiongozi wetu alisema kuwa tukifanya wema tusijitangaze(Mkono wa kulia usijue etc. etc.). Mengi amekuwa kama mfarisaya kwa kupiga kelele kwa sauti kubwa kuwa anamsamehe mbaya wake kama MKRISTO. Sasa iwaje? Kama ilivyoimbwa zamani, "tenda wema uende zako eheee, usingoje........"

3.Mengi anamalizia kwa kumpongeza Rais wa jamhuri hii ambaye ndiye boss wa huyo anayemtuhumu. Hii inanukia kuuma na kupulizia. Kama kweli anaamini anayosema, basi angempelekea tuhuma zake na kungoja azishughulikie. Kwa kuzileta kwenye public forum kunaonyesha kuwa hana imani kuwa haki itatendeka bila msukumo wa ziada. Kiongozi makini hahitaji msukumo huo.

Aandla......
 
kama si masha ni adam malima.adam anahusishwa na mikakati mingi ya kummaliza mengi kwa kutumia propaganda za siasa na dini

Kwa hiyo mkakati wa Adam una fanana na wa baba yake???
 
Wakuu wengine walidhania kuwa waziri huyo ni Adam Malima!! Inawezekana kabisa kuwa they are right kwasababu huyu masha alitoa pendekezo la kummaliza Mengi kwa kutumia TRA wakiwa na jopo la wenzie; sasa kundi la Masha yomo huyu Malima[ Mtoto wa Nyoka ni NYOKA mnakumbuka marehemu baba yake alivyotuliza na yeye wahindi wakamdhulumu akapata stroke ulaya] .Hawa vijana wana CABAL yao ambao ni watetezi wakubwa wa fisadi Lowassa na inaaminika kuwa baada ya kujiuzulu Lowassa alipendekeza majina yao kwa muungwana wakati anatengeneza cabinet mpya na ndo wakaingizwa.Katika hilo kundi lao yumo pia Mbunge wa Kigoma mjini aliyeshindwa Nec hivi karibuni Serukamba.
 
It’s rotten, it can’t be repaired; it needs replacing. Kila unaposhika pameoza! Use by date ya serikali hii ya CCM ilipita kitambo lakini tunaendelea kuikumbatia tu!

We need a new beginning. To paraphrase Obama, let me say that we cannot continue to use the same CCM “leaders” over and over again and expect a different result.

Kama wananchi wa Mbeya Vijijini watachagua mtu wa CCM kuwawakilisha basi nitajua tumekuwa nchi ya vipofu. Utachaguaje samaki kwenye kapu lenye samaki wengi hivyo waliooza? Yako makapu mengine!

Labda JK anajitahidi kukarabati hili liserikali lake. Kwa maoni yangu, halikarabatiki. Ni la kubadilisha (kwa kura za wananchi).



Swadakta!
Man, umegonga penyewe.
icon14.gif




.
 
"waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti "

Mzee wa kijijini na wakuu wengine, kwa hekima zenu mnaweza kutusaidia sisi vilaza kufumbua hilo fumbo hapo juu?

Natanguliza shukrani.

Najua nitatofautiaaa sana bwna sana na wengi katika hili, kuna wakati huwa namshangana mengi kwa jinsi au style yake ya KULIA LIA, sasa mtu mzima kama wewe mwenye kumiliki vyombo vingi vya habari kuliko mtu yeyeto TZ, unasimama kwenye vyombo vyako kulalama ETI WAZIRI MMOJA KIJANA, si amtaje tu na au ampeleke mahakamani? hii tabia ya umbea wa magazeti ya udakau kaiotoa wapi? hata kama ni kutafuta sympathy sio kihivyo.

Akitofautiana na mtu tu, huyooooooooo kwenye vyombo vya habari, anachoogopa nini? mtu atawezaje kukutaifisha bila ya wewe kuwa na kosa? kwanini uogope vitisho wakati wewe ni mtu safi? nakumbuka aliwahi kuwa mmoja wa wadeni wakubwa wa mabenki nchini kabla hayajabinafsishwa huyu. sijui kama alilipa au yalipotea hewani, ndiyo lazima tujiulize mabenki yalikuwa yanatengeneza faida lakini yakakosa pesa za kujiendesha kwa vile zimeshikiriwa na matajiri hawa hawa.
 
1. Naungana mkono na Capo di tutti capi wangu kuwa hapa hapajakaa sawa. Mengi mwenyewe, kwa hiari yake, ameamua kuleta hizi habari kwenye public forum. Amesema ushahidi anao wa hayo anayosema. Sasa kwa nini asite kumtaja mhusika na abakie aki-drop heavy hints(kijana, wizara nyeti, msomi sana, wink,wink,wink!) kuwa ni fulani? Ataogopaje libel wakati anasema ushahidi anao? Angefanya kama alivyofanya Slaa au hata Kikwete ( kuhusiana na Gama alipogombea mara ya kwanza) angejijengea heshima zaidi. Kwa kufanya alivyofanya kunazidi kuthibitisha kuwa yeye ni mlalamishi tu anaependa kulia kulia ili aonewe huruma na jamii.

2. Kama mmisheni mwenzake naamini kuwa alichofanya si kile ambacho kiongozi wetu alituambia tufanye. Kiongozi wetu alisema kuwa tukifanya wema tusijitangaze(Mkono wa kulia usijue etc. etc.). Mengi amekuwa kama mfarisaya kwa kupiga kelele kwa sauti kubwa kuwa anamsamehe mbaya wake kama MKRISTO. Sasa iwaje? Kama ilivyoimbwa zamani, "tenda wema uende zako eheee, usingoje........"

3.Mengi anamalizia kwa kumpongeza Rais wa jamhuri hii ambaye ndiye boss wa huyo anayemtuhumu. Hii inanukia kuuma na kupulizia. Kama kweli anaamini anayosema, basi angempelekea tuhuma zake na kungoja azishughulikie. Kwa kuzileta kwenye public forum kunaonyesha kuwa hana imani kuwa haki itatendeka bila msukumo wa ziada. Kiongozi makini hahitaji msukumo huo.

Aandla......


Of course, waerevu wengine pia watang'amua hilo. Alikuwa anamtumia Raisi ujumbe kumshinikiza kumwajibisha kijana wake. Hii sio mara ya kwanza Mengi kumpa ujumbe Raisi kwa staili hii. Anachomaanisha ni zaidi ya anachokitamka.


Sitarajii kuona Mengi akifanya kufuru.



.
 
wakuu ninaomba kuungana na wachache, lawrence fortunatus masha ni waziri wetu wa mambo ya ndani, reginald mengi ni bepari mtanzania. Kama mengi yeye analipa kodi zote impasavyo press release za aina hii za nini??!! Kama anao ushahidi wa yeye kutishiwa kuuawa na mmoja wa mawaziri vijana wa jmk kwanini suala hili halipo kwa igp mwema na dci manumba na siyo ktk press realease??!! Mengi si mwandishi wa habari, mengi si politician lakini kwa nini kila kukicha anataka tumuone yeye ndiye shujaa wa habari tanzania??!! Kama kuna kutishiana maisha kwa kiwango hiki kwanini mzee mengi bado ana with hold jina la muhusika/ mgomvi wake? Nashindwa kumhusisha waziri yeyote as long yeye mzee wetu mengi ameogopa kumtaja na ni kwa mtaji huo huo ninawaomba wote tuweke msimamo kuwa ktk hili mzee ameuhadaa umma.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom