Mengi Vs Masha tuhuma, vitisho na matokeo!

Status
Not open for further replies.
...huyo Masha kishalewa na kawa mjinga tuu hana lolote,juzi kaenda magereza kufanya ufisadi tuu,wizara yake ndio inaongoza kwa rushwa na huduma mbovu,nilitegemea angefanya improvement kubwa sana kwenye wizara yake especially kwenye IT lakini ni upuuzi mtupu..nasikia kazi yake wanawake tuu na ujiko wa kijinga jinga!

Umesikia wapi na kutoka kwa nani?
 
Amakweli nchi imekwisha sasa,

Unapoona kina mzee ngombale wanawekwa pembeni wanachukuliwa vijana na kupewa nafasi, mtu unapata hope kuwa sasa tutapata new thinking, new way of doing and accomplishing things and thus move faster towards development...

Kumbe ndo unakuta vifisadi vidogo vimepewa meno kila kona...mara Masha, mara Makala, mara nchimbi. Yani wale vijana wa kuleta hope ndo wamekua wafanya madudu ya ajabu...Jk turudishie kina sozigwa tujue moja tumekwama... kuliko vijana walioelimika vizuri ila wameoza inside na hawana wito kwa nchi...Na hapo wana miaka miwili tu!
 
Mkurugenzi wa Makampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi amekutana na waandishi wa habari na kusema mambo mengi na baadaye kutoa tamko lifuatalo.


TAARIFA YA BW. REGINALD A. MENGI, MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP LIMITED KWA VYOMBO VYA HABARI


Hivi karibuni waziri mmoja kijana anayeongoza wizara nyeti alipendekeza nibambikiziwe kodi bandia ya kiasi kikubwa nitakachoshindwa kulipa na hatimaye nifilisiwe kama njia pekee ya kuninyamazisha kabisa eti kama alivyofilisiwa tajiri mmoja mkubwa huko Urusi.

Alidai kwamba vyombo vyangu vya habari vimekuwa mno mstari wa mbele kupiga vita ufisadi, jambo ambalo kwa maoni yake siyo zuri kwa sababu linawanyanyasa baadhi ya watu.

Nilitegemea waziri huyo msomi sana angefahamu jinsi vyombo vya habari vinavyofanya kazi. Angalao angefahamu kwamba anayeamua nini kiandikwe na nini kisiandikwe ni mhariri wa gazeti ambaye taaluma yake ni uandishi wa habari na siyo mmiliki wa vyombo vya habari.

Kama mkiristo na kama alivyoagiza Bwana Yesu namsamehe kwa vile hajui atendalo. Baada ya kumsamehe ningetaka ajue yafuatayo.

Asiyekemea maovu katika jamii, yeye ni sehemu ya maovu hayo. Waziri huyu na wale wote ambao wamekwishanitumia vitisho wakumbuke kwamba hata kama watafanikiwa kuvinyamazisha kwa hujuma zozote zile, vyombo vyangu vya habari, na hata kama mimi sitakuwepo tena, moto wa kupiga vita ufisadi uliokwishawashwa katika akili za wanajamii hauwezi kuzimika kamwe.

Ieleweke pia kwamba sauti za maskini na wanyonge katika jamii hazisikiki kwa urahisi. Vyombo vya habari husaidia kupaaza sauti na vilio vyao katika vita dhidi ya maovu. Ni wajibu wa kila mtu aliye na uwezo kusema kwa sauti kubwa kwa niaba ya wanyonge na maskini ili kutokomeza ufisadi.

Nachukua fursa hii kumpongeza sana Rais wetu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuguswa na sauti na vilio vya wanyonge na maskini wa Tanzania kuhusu ufisadi na hatua za kijasiri zinazochukuliwa na Serikali yake dhidi ya ufisadi. Sisi sote ni lazima tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu azidi kumpa ujasiri, nguvu na hekima nyingi wakati huu wa majaribio makubwa.




____________________
Reginald A. Mengi
Mwenyekiti Mtendaji
IPP Limited
3 Desemba,2008

NB: Vyanzo mbalimbali vimeihakikishia KLHN kuwa Waziri huyo ni yule mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani ya nchi. Vyanzo hivyo toka kwenye Jumba letu Kuu vimeihakikishia KLHN kuwa siku za hivi karibuni Waziri huyo amekuwa akijikuta akitajwa na vyombo mbalimbali vya habari na vile vya udaku wa mtandaoni akihusishwa na tabia mbalimbali ambazo kwa mujibu wa Jumba hilo vinaiweka vibaya sura ya uongozi wa Taifa.

Kuna uwezekano mkubwa katika mabadiliko madogo ya Mawaziri ambayo yanatarajiwa wakati wowote Waziri huyo akatemwa.



Sasa wanataka kumwadapisha sio ahahaaaaaaaaaaaaa jamaa bwana.
Ila na yeye katoa maelezo mazuri na ujumbe mzuri kwao kuwa hata yeye wakimtoa kwenye ramani ya dunia moto huu dhidi ya ufisadi ndio kwanza unawaka.

Huyu waziri juzi pia si elenda kuwaona wakina mramba na yona rumande mhhhhhh ,mwenye conection jamani.Pia tukumbushane sehemu alizonufaika kwenye ufisadi.

Je alikuwa akimshauri muungwana kuwa IPP media anamwalibia muungwana au inawaalibia mafisadi?
 
Kuna vilaza wanafikiri wana nguvu za kuzuia tsunami kwa kujenga ukuta wa mchanga ama wanaota tu !!
 
Watu walitegemea Masha Msomi kijana ametoka NYC atakuja kuweka mambo yaende kisasa, ameshindwa. Kama hizi habari ni kweli (who know with Tanzanian real-politik) basi Masha zaidi ya kushindwa, amedidimia kabisa katika lindi la ufisadi.Tunasubiri tu washkaji zake wazee wa datazz waje kumtetea hapa, watatetea sana mwaka huu lakini hili ni sinking ship kama Titanic.

Na huyo Mengi naye kujifanya mstari wa mbele ananunua popularity kwa bei rahisi tu hana lolote.

hayawi hayawi yamekuwa. Jamaa vision yake ni kumrithi Kikwete... kazi kweli kweli unaweza kwenda shule lakini ukashindwa kuelimika. A noble person never condone ufisadi ... Keep connecting the dots kuanzia ziara za ajabu ajabu Lupango ... JK, it was a big mistake kumpa huyu jamaa uwaziri wa mambo ya ndani sijui nani alimfanyia vetting na kumpitisha??
 
Nina maswali mawili hapa. Kama Mengi ana uhakika na anachokisema kwa nini hakumtaja huyo waziri kwa jina, anaogopa nini?

Na huyu Masha tunaambiwa ni msomi. Ni msomi wa nini na kwa kiwango gani?
 
Huyu Masha naona naye ameshaanza kulewa madaraka. Na kujiona ni miongoni mwa wale wasiogusika. Kimsingi, nashindwa kuelewa ameingia vipi katika siasa na kufikia wadhifa wa juu na kuwa mkuu wa Wizara nyeti kama hiyo ya Mambo ya ndani.Pumbafu sana huyu kijana!! Soma pumba yake nyingine hapa chini!!


Walemavu: hatumtaki Masha
Mambo yanazidi kuwa si mambo kwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Lawrence Masha, kutakiwa kujiuziru kwa kile kinachodaiwa kutoa kauli siku a usoni juu ya mauaji ya albino.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) liliweza kufanya mahojiano na Waziri huyo na kusema kwamba mauaji ya albino ni kitu kidogo.

Kutokana na kauli hiyo albino pamoja na walemavu wote nchini, walitangaza kutokuwa na imani naye na kumtaka awaachiye wengine nafasi aliyokuwa nayo.

Mpaka sasa wananchi huzidi kusikitishwa na jinsi Serikali inavyoshindwa kuwalinda albino hao, huku wanyama walioko katika mbuga mbalimbali wakipatiwa ulinzi wa kutosha.

Mtaalamu wa ushauri wa Jamii ya Albino Tanzania (TAS), Bw. Kondo Seif alisema kuwa ni lazima watahakikisha kuwa Bw. Masha anawajibishwa kwa kauli yake hiyo na kuahidi kuwa 'asipokufa' na waziri huyo basi atauawa na wauaji na kumtaka Rais Jakaya Kikwete amwajibishe waziri wake huyo haraka.

Aliongeza kuwa mpaka sasa hakuna takwimu sahihi za mauaji ya albino, ambapo kwa makadirio ni 32 tu ndio wanaotambulika kuuawa kinyama, lakini idadi hiyo ni ndogo sana kutokana na idadi kubwa ya albino wanaouawa kutotolewa taarifa iwe kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

"Tulisikia kauli ya Mheshimiwa Rais Kikwete katika kilele cha maadhimisho ya kulaani mauaji ya albino kuwa ni lazima atasambaratisha mtandao wa wauaji kama dola lilivyofanikiwa kusambaratisha mtandao wa majambazi nchini.

Kauli hiyo ya JK iliweza kuleta faraja kubwa sana kwa albino, lakini kwa bahati mbaya kuanzia siku ile hadi leo, albino kadhaa wamepoteza maisha yao na wengine kuongezewa kiwango cha ulemavu kwa kunyofolewa viungo vyao.

Jamii ya albino imepungukiwa imani kwa viongozi wao na vyombo vya dola kwa ujumla kwa ujumla
 
In his own words Lawrence Marsha, Excerpts:

"Upon completion of my LL.B at the University of Dar es Salaam I once
again travelled to the United States where I obtained a Masters Degree
in Law from Georgetown University in Washington DC.

Many people who look at the United States from afar only see a
nation of great power and great wealth. Many don't go beyond the visibly
obvious to see that this great land of power and wealth was created through
the hard work and sweat of very many Americans no different from you
and I.

In the US as I said earlier, the lessons I learned that shaped my life
were more clear to me after having come back to Tanzania to take my
undergraduate degree and then going back to states to take my Masters.

This was because I now began to wonder why Tanzania with all its
potential could not be more like the United States in terms of
development.
That is when I as a person decided to do what I hope
all of you will when you go to the States and that is to take the time to
understand American history as well as its people. An understanding of
its history and its people is probably the greatest gift you can give to
yourself during your stay in the States.

You will come to learn that most Americans have an incredible love
for their country and have a willingness and desire to serve their
country whenever called to do so.
When the Late John Fitzgerald Kennedy
said at his inaugural address in January 1961 "Ask not what your country
can do for you, but ask what you can do for your country", this message
touched a chord in the heart of majority of Americans, and still does.

Reflecting on this spirit I began to ask myself, what have I done
for Tanzania?
Is my desire to stay in the United States or that of my
friends driven by our personal search for the creature comforts
available to a Georgetown law graduate such as myself in the States.

Isit not possible, I asked myself, to achieve a comfortable lifestyle in
Tanzania, and if not why? Could I not help to remove those impediments.
Do I not owe Tanzania as a patriotic Tanzanian to use my knowledge to
turn Tanzania into the place I would like it to be."


Keynote speaker Lawrence Masha, delivering his Keynote address
during the Pre-departure Orientation to the students who are admitted to
U.S. universities and Colleges, at the American Embassy. August 2005.


My take,.. inaonekana baada ya kuonja power kidogo ameshasahau the so called his"lessons from the United states".
 
Matokeo ya kupeana vyeo kiuanamtandao. Kampuni ya uwakili - Ridhiwan - Deep Green - - - uwaziri. Muungwana hawezi kukwepa hili la kuwa na mawaziri butu kimaadili na kuitendaji. Kazi kwelikweli kuunawisha uso wa muungwana!
 
Kama kweli kutatokea mabadiliko madogo katika baraza la Mawaziri, Masha hawezi kuachwa bila cheo chochote. Mnaweza kusikia kapewa ubalozi somewhere maana huyu fisadi ndiyo anajua siri kati ya Deep Green na SISIEMU. Kazi iko kweli kweli ila serikali iangalie na iwe makini maana wananchi wakichoka wanaweza kuchukuwa style ya THAI.
 
Amakweli nchi imekwisha sasa,

Unapoona kina mzee ngombale wanawekwa pembeni wanachukuliwa vijana na kupewa nafasi, mtu unapata hope kuwa sasa tutapata new thinking, new way of doing and accomplishing things and thus move faster towards development...

Kumbe ndo unakuta vifisadi vidogo vimepewa meno kila kona...mara Masha, mara Makala, mara nchimbi. Yani wale vijana wa kuleta hope ndo wamekua wafanya madudu ya ajabu...Jk turudishie kina sozigwa tujue moja tumekwama... kuliko vijana walioelimika vizuri ila wameoza inside na hawana wito kwa nchi...Na hapo wana miaka miwili tu!


Huyu mheshimiwa kama kweli ni yeye anongelewa na mzee Mengi basi naweza kuweka conclussion kubwa kuwa huyu mheshimiwa ni hopeless. Nilitaraji kuwa damu mpya kama yeye watasaidia kuleta mambo mapya, kama mambo mapya ndio haya naona sasa itabidi nile matapishi yangu na kutotaka tena uongozi wa vijana. Toka alipoenda Keko na kushindwa kutetea kwenda kwake na kupiga porojo isiyoeleweka, na sasa kuanza kutaka kuleta siasa zile za chuki, na kusikia kuwa amekuwa hata akiingia kwenye makala za udaku, naona ni much better kuwa na wazee kama kina Malecela kwenye uongozi wanaoongea yenye sense, na kufanya mambo sensible. Kama mh JK akifanya reshuffle ni vizuri kama akamrudisha huyu jamaa US, hatusaidii hata kidogo zaidi ya kutudisappoint.
 
Nina maswali mawili hapa. Kama Mengi ana uhakika na anachokisema kwa nini hakumtaja huyo waziri kwa jina, anaogopa nini?

Na huyu Masha tunaambiwa ni msomi. Ni msomi wa nini na kwa kiwango gani?


Kuna mtu kakujibu nadhani it all about libel labda ikitakiwa kufanya hivyo atafanya.

Kuhusu usomi wa Masha mimi naona kaenda shule to get stupid kamakasoma kweli.
Ameshindwa kuongea hata shwala la mauaji ya albino na wamemjia juu,stupid!
 
Watu walitegemea Masha Msomi kijana ametoka NYC atakuja kuweka mambo yaende kisasa, ameshindwa. Kama hizi habari ni kweli (who know with Tanzanian real-politik) basi Masha zaidi ya kushindwa, amedidimia kabisa katika lindi la ufisadi.Tunasubiri tu washkaji zake wazee wa datazz waje kumtetea hapa, watatetea sana mwaka huu lakini hili ni sinking ship kama Titanic.

Na huyo Mengi naye kujifanya mstari wa mbele ananunua popularity kwa bei rahisi tu hana lolote.

Umem discredit Masha based on maneno ya Mengi (umesema kama hizi habari ni kweli basi Masha fisadi) halafu hapo hapo ume kandya maneno ya Mengi kwamba anatafuta popularity. Kama maneno ya Mengi nayo ni discreditable wawezaje kuyatumia kumhukumu Masha ?

tafsiri yako ya kujiamini ni ipi?

Kwanza habari za siku Mwanamke wa Kiafrika, unapotea mno kwenye mapambano na kuibuka siku za ushindi, huna mpango!

Mengi amefanya udaku kwa kudokezadokeza identity ya "waziri kijana" akiogopa, akishindwa kujiamini, kuanisha anatachotaka kusema. Ndio nilivyomaanisha, aache kuwa wussy na mdaku.
 
Huyu Waziri Masha amezidi sana, kuna habari kwamba hupenda kupiga maji na akilewa huwa hutoa siri za serikali kwa watu anaokunywa nao na kwa vimada wake. Vitisho kwa Bwana R.Mengi mwenye gazeti la ThisDay alivisema lakini hakujua aliyekuwa anaongea nae alimrecord na kupeleka kwa Mengi. Bwana Mengi akamwasilishia Waziri Mkuu Mizengo Pinda na finaly kumfikia mheshimiwa.

Nasikia wale wazee wa vyombo vya usalama wa taifa waliingia kwenye ofisi za Partner zake katika law firm yake, ambao wote walikutwa hawapo.Nasikia computer zote zimechukuliwa na investigation inaendelea, only one left is Ridhwan. Masha alifikiria kumweka Ridhwan Kikwete kwenye Lawfirm yake kungempa immunity.

Sasa uwaziri umekwisha, the law firm is going down na US citizenship hana.
 
commentary yangu ndiyo imesema "Waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Ndani".. yawezekana source yangu ikawa off kabisa (so far haijaniangusha kwani na mimi sikutaka kuirusha hii habari hadi nijue nini kinaendelea). Halafu msihukumu tu kilichoandikwa hapo kwani waandishi waliokuwepo walipata nafasi ya kuuliza na kuzungumza na Mengi (unless na sisi tumtafute atufafanulie).

Tusubiri magazeti yatakavyoripoti kwani mimi nimepata hard copy to ilivyo na nilisikiliza kidogo ITV kwenye taarifa ya habari ya saa nne usiku. Wakati wakirudia sehemu ya hayo mahojiano.

Ninachofahamu kwa uhakika ni kuwa jana (jumanne) kulikuwa na mkutano Jumba Kuu ambapo mojawapo ya mada ni hili na walikuwa wanajua Mengi atasema nini leo. Sasa, naambiwa hakwenda kule mikono mitupu....(sasa asiyejua maana siwezi kumsaidia!)
 
Umem discredit Masha based on maneno ya Mengi (umesema kama hizi habari ni kweli basi Masha fisadi) halafu hapo hapo ume kandya maneno ya Mengi kwamba anatatufa populatity. Kama maneno ya Mengi nayo ni discreditable sasa wawezaje kuyatumia kumhukumu Masha ?



Mengi amefanya udaku kwa kudokezadokeza identity ya "waziri kijana" akiogopa, akishindwa kujiamini kuanisha anatachotaka kusema. Ndio nilivyomaanisha, aache kuwa wussy na mdaku.


Nakuunga mkono swali unalomuuliza Pundit.

Ila la Mengi kushindwa kuainisha anachotaka kusema mimi nadhani unapoongea unatakiwa uzingatie zaidi kwenye kutuma ujumbe ukiwa kwenye safe side.Strategic & tactics needed when it comes to issue like this,small error hata kama ulikuwa una sue wewe they countersue.
Kuna mtu ame bring abour ribel nadhani hiyo ndio anacheza nayo kwanza ,kama kibidi nadhani anaweza kukizi matakwa yako.
 
Nafikiri waziri Masha anasikitisha sana.

Ungetegemea ujana wake, kuijua dunia na pia kuwa na pesa za kutosha kungemfanya huyu kijana mwenzetu afanye yale tunayoyaamini wengi, lakini inaelekea ni mjinga kama Watanzania lundo nzima ambao tumekuwa tukigongana nao. Ukiwakuta huku majuu utafikiri watu wa maana, wakirudi nyumbani ni wabaya kuliko hata watu ambao hawana exposure kubwa.

Hii ni aibu kubwa sana kwa vijana wote. Hatuna tofauti na watu kama akina Yona, Ballali, Chenge na wengine.

Kushindwa kwake kushughulikia matatizo ya Albino ni dalili tosha kwamba huyu kijana mwenzetu yuko out of touch na hana jipya zaidi ya ujinga ambao inaelekea mungu ametulundikia sisi watu weusi.

Hivi tuna matatizo gani? Aibu kweli kweli.

Mkuu FMES, mwambie huyo kijana aache ujinga na achape kazi, mambo mengine yatafuata.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom