Mengi vs Manji: Ukweli ni upi?

Ili kuondoa miingiliano ya threads na maelezo basi naona bora mambo yote yawe humu

na nadhani mdahalo utakuwa mtamu zaidi humu
 

Kwenye hili jamani mimi naomba nimtetee Mengi.Benzi kanunua kwa pesa zake,katumia (mimi sijui kama ni kweli) jina la chama cha walemavu kupata exemption,mbona hayo mambo yanafanyika sana hapa! Zamani watu walikuwa wanatumia waalimu...unaagiza gari kwa jina la mwalimu then unamkatia kidogo.
90% na magari ya kifahari hapa mjini yote ni exempted!And that is a fact! Wengi wanakuwa na TIC certificates za makampuni ambayo hata haya-qualify lakini they are in possession of such certificates.Watu wanatumia makanisa,misikiti...haohao mnaosema matajiri,lakini Mengi si huwa tunamwona anawajaza wasiojiweza Diamond Jubilee mule na kuwapa chakula cha mchana? Au mara ngapi tunasoma kwenye magazeti huyo Mengi katoa shs milioni kumi kwa wasiojiweza,mimi binafsi nimeshasoma habari kama hio zaidi ya mara mbili.
Lakini,pamoja ya yote hayo,wakati yeye mwenyewe anajitafutia balaa.
Mashambulizi mengine anajiletea yeye mwenyewe.Haya mambo yake ya kuwa anatembelewa na mabalozi ofisini kwake na kutoa kwenye TV watu wanaya-translate vibaya,na mimi sioni kama yanamsaidia,hao wafanyabiashara wenzake ndio wanaommaliza kutokana na vitu kama hivyo.
He is a champion at miscaluculating!
There was a time alijiingiza Yanga,matokeo yake ni kutaka kupigwa mawe kule na wale wazee kumtukana na kumwambia kuwa ya nyumbani kwake kayashindwa ndio aje kutatua ya Yanga! Ndio maana sasa Manji kaingia Yanga,Mengi hawezi kurudi tena Yanga,maana hawataki hata kumsikia!Mara kaingia kwenye biashara za Tanzanite,na huko wakavurumishana na wenyewe,doesnt he ever learn! Ndio maana Mwalimu alimwambia kuwa hawezi kujiita ana viwanda,yeye kazi yake ni packing tu,kama Colgate,sabuni(then) etc..LOL! Achukue huo ushauri wa doctor,amrudie mkewe wapumzike wale pesa yao!
 
Zanaki,

Kwa nini umtete? kama kweli mengi ana hela angeingiza hiyo pesa na kulipa ushuru. Ni bora hata aisngetoa hiyo misaada na kulipia ushuru. Kama ni kweli amejishushia sana credibility. Ingekuwa ni kwenye nchi za watu ndio ingekuwa mwisho wake kibiashara. Tatizo letu waTz tunapenda sana cheap popularity na mambo ya misheni town. Matokeo yake we are bleeding our country to death. I hate the fact that some people in our country seem to be above the law. I wish JK and his government had balls of steel to bring some discipline in our society. They just need to nail a few of the so called vigogo and the rest will fall in line.
 
Nashukuru kwa michango yenu zaidi nimefurahishwa na mada kurudi kwenye mstari.
Hongera Tafiti pia karibu swahiba yangu Fikiraduni ingawa kule Mzumbe bado hatujamaliza.
Hizi ni pesa nyingi na hazikuletwa kwa manufaa ya kikundi cha watu nami naingia msituni kujua Kulikoni?
 
nakuunga mkono mkono Mtz kwa mara ya kwanza.
kuwapa chakula walemavu just a lunch for the whole year is not proportional kwa Ushuru na kodi ya TRA yenye thamani ya ya bilioni 6.
Nazidi kufurahi yanaibuka mambo mengi zaidi ya uchafu.
Nadhani JK anahitajika kuifumua TRA kwa haraka sana maana kule ndio ma home boy wa Mengi wamejazana.
niliona makala ya MMANDA afisa uhusiano wa TRA alipodai kuwa wachagga kujazana TRA sio issue. watu waulize na jeshi mbona kuna wakurya wa kumwaga? sikutegemea majibu kama haya toka kwa kiongozi wa TRA. kwani kama mwenzio mwizi basi na wewe uibe?
Nina hakika akina Kittilya(mkurugenzi mkuu wa TRA) wana ten percent zao kwenye deni hili. naingia msituni wanaforum
 
hiyo ililetwa na DR. WHO tayari nadhani Msanga ulikuwa bado hujaingia.nisaidie Administrator
 
ndio nime confirm ilikuwepo na ipo na aliianzisha Dr.WHO kama kuna mchango Msanga utoe iko page ya 2 au 3. TENA ina hadi Manji.
 
Zanaki,

Duh .. Kumbe ndivyo ilivyokuwa hivyo?!

Una jina la angalau mmoja wa hawa vijana?
 

Kawaibia walemavu?where is the evidence?Mimi nawachukia sana watu wanaokuja hapa wakiwa hawana data bali tetesi.Dunia haiendeshwi na tetesi bali facts.Kulikoni,dont try to hide your true colours...unataka kuthibithisha unachokiamini...kwamba tuhuma dhidi ya Mengi ni za kweli ndo maana unadai kuwa kama kawaibia walemavu hawezi kukwepa kodi.

Pengine hujapitia topic anazochangia huyo anaelaumiwa
ndio maana unakurupuka kusema asilaumiwe.Ok,ripoti ya NSSF umeiona,unashauri tu-discuss ukweli/uongo/apungufu ya ripoti hiyo.Hilo halina tatizo,lakini wewe binafsi mchango wako ni nini hasa katika discussion hiyo kabla ya kuwaomba wengine wadiscuss?Je kwa mtizamo wako ripoti ina ukweli au uongo?
 

Mujahidina on the move
 

Mzee Unanishangaza sana jinsi hili suala la Mengi lilivyokugusa na unavyojitahidi kumtetea hata bila data. Ile misimamo yako against watu corrupt naona katika suala hili umeiweka pembeni. Yaani haionyeshi kuwa uko keen kujua whether hizi allegations ni za kweli au la .. umeshaamua tu kutetea.

Suala la walemavu, nimetoa mfano ambao uko clear, na nimesema "kama ni kweli", there is still a room for you to convince us otherwise. Kama una data si uzimwage hapa? .. wasomaji tutaamua wenyewe nani msema kweli. Na kama huna data on this issue NYAMAZA, it works.. sio kuleta hasira tuuu kwa Mengi kusemwa! Na inaonekana wazi umekasirishwa kwa hii mada kurudi back on track.

Masuala ya kuleta ushahidi yalishapingwa katika forum hii, wakati admin alipoleta initial proposal ya sheria za forum. Na ikasemwa kuwa ni vigumu kuleta ushahidi humu kama wa mahakamani .. mwenye data azimwage tuu wasomaji tutaamua wenyewe mbivu na mbichi. Kama ukiletwa ushahidi basi ni big bonus.

Ripoti ya NSSF nimemuomba Admin aihamishie kunakostahili lakini hajafanya hivyo,.. I hope he will... maoni yangu nitayaweka huko, hapa sitaki kuharibu topic.

E jama ee, achaneni nae huyu. Leteni data on the topic kama bado zipo! FD tunasubiri maelezo kutoka NBC. Kama Mengi ni mwizi, haitaandikwa katika ippmedia wala THISDAY. Ni forum kama hizi ndimo wenye data watakapozimwaga. I recently saw a similar discussion in Darhotwire..which is associated with ippmedia... and guess what, as of today, the whole thread has been deleted.. na wachangiaji against Mengi wamekuwa banned! Sasa humu ni wazi wakina Mlalahoi nao wanataka hii discussion ife. Haifi mpaka iwe exhausted.
 
Mlalahoi said:
Mujahidina on the move

Once again,.. ujahidina umeingiaje hapa? You keep on repeating this without any justification.

Usitutoe kwenye mada, tumekushtukizia, respond to the points.. kama huna data za kumtetea jamaa yako KAA KIMYA!
 

Hizo data zako ziko wapi?
 
Mlalahoi said:
Hizo data zako ziko wapi?

Sijaclaim kuwa na data.

Ni wazi kuwa kuna ambao wanazo na wameshaanza kuzimwaga humu.. but for some reasons zinakukera. Tulia mzee tufaidike na data za pande zote, then kila mtu na maamuzi yake.
 

Unajua kila kitu huwa kinakufa.Nothing lasts forever.Hate him or love him,Mengi has done a lot to the society.Mimi na-appreciate efforts zake hususan katika sekta ya habari,na if he were to be compared with Manji nadhani kila mtu anaelewa what's the outcome.Whether misaada yake kwa walemavu inatafsiriwa kama utapeli,the fact remains that he's at least done something (eg kuwa-entertain walemavu from time to time).Kwangu mie,Mengi amefanya vitu kadhaa vya kizalendo contrary to akina Manji ambao kimsingi allegiance yao iko India kuliko Tanzania.

Simtetei Mengi kama Reginald bali kama mzalendo ambaye at least ameonyesha njia kwa Watanzania wengine.Tuhuma dhidi yake (ambazo pamoja na urefu wa mada hii hazijaweza kuthibitishwa) zatapata maana pale tu zitapoletwa data kuzithibitisha na sio tetesi zisizo na kichwa wala miguu.

You surely know why I associate this with ujahidina,and I dont need to clarify that.
 
Mzee Zanaki,

Great points, na kuna data nyingi humo ndani yake, that is what we are talking about, yaani data means data that is it!

Jamani hii forum huko majuu inaitwa BLOG, ni mahali pa wananchi kutoa maoni yao kwa haraka, haraka! The matter of fact ukiangalia hizo BLOG za majuu huwa zina sentensi moja tu au mbili, sasa it is no question kuwa hapa tumeamua kufanya mambo kibongo bongo, GREAT!, lakini tusisahau kuwa ni at the end of the daty bhii ni BULOGU tu!, sio kongamano hapa au workshop, mahakamani au bungeni, au kamati ya rais, au kamati ya ukweli, HAPANA!

hapana, hapa ni mahali wananchi wote wake kwa waume, waliosoma, wasisoma, wakulima, wajenzi, wavuvi, na kila sekta mpaka machinga, wana haki ya kuingia na kutoa machungu yao dhidi ya system inayowatala, sasa kama kuna mwanachi ameandika bilka ya kuwa na FACTS, dawa ni mwenye FACTS, au data kuziweka, kama alivyofanya Mzee Zanaki, sasa kama haziko sawa na unazijua zilizo sawa ziweke na tuendelee na mjadala, lakini tabia za kujaribu kujikakamua kwa kutumia majina ya wajumbe wengine ni kupotosha nia hasa ya forum na mjadala kwa ujumla, ninamuunga mkono mjumbe mmoja aliyesema kuwa kuna watu ambao kwa makusudi wanataka kuharibu mjadala kutokana na sababu wanazozijua wenyewe maana wakishaingiza majina fulani basi wanajua kuwa mjadal utaharibika tu kwani yatatokea mashambuliza ya binafsi,

Ninatoa SALUTE maalum kwa wazee Muggy, Mlalahoi, na Kulikoni kwa kulielewa hilo na kusisitiza wajumbe wa-stick na majadala, jamani nchi yetu inayumba kwa sababu ya wananchi wasioelewa kama alivyosema Mzee Tambwe Hizza, sasa inakuwaje hata sisi pia tuyumbishwe humu?

Jamani kuwa au kutokuwa na data ni sawa tu, nia na madhumuni ni kumkoma nyani giladi, tuache utoto na tuangalie picha kubwa! Kama huna data kaa pembeni waachie wenye nazo issue ni nyingi humu kama huna data za issue moja lazima utakuwa na data za issue zingine hakuna haraka!
 


Alright mzee,

You are entitled to your own opinion.

Based on IPPMEDIA reports, Mengi is super clean. With years of reading his bright side, i know more good of him than evil.. but that doesn't stop me from hearing what is 'the other side'.

Leteni vitu vijana.. both good and bad.. especially what we don't read elsewehere. No deliberate lies please. Peace.
 
Nungwi,

Nimetoka kapa NBC, jamaa hataki kulizungumzia kabisa, anayeyusha kwa kuulizia mambo yetu binafsi na familia. Nadhani mambo yalisukwa vizuri mno.

Kuna njia nyingine nitatumia, nikipata kitu nitawajulisha.

FD
 
pole mkuu Fikiraduni
mimi bado niko msituni ila nasikia kuna file la mheshimiwa Mengi limeanza kushughulikiwa na DCI Manumba ambalo uchunguzi wake ulianza mwaka jana November na IGP Mahita alisimama kidete kuzuia huo uchunguzi. sasa Manumba analifuatilia ila nazidi kuchimba hilo file linahusuana na nini kama huu mlungula ya UN au usanii mwingine? jamani mwenye data zaidi anisaidie.
na watu wangu pale Mambo ya ndani wamesema nisubiri kidogo kwani wanajipanga.
ila haitachukua siku mbili.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…