Mene mene tekeli na peresi - Lema

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,205
Salamu Watanzania,

Naomba tusome andiko hili kutoka katika Biblia. Daniel 5: 19-21 na mstari wa 25 hadi 28.

Na kwa sababu ya ule ukuu aliompa, watu wa kabila zote, na mataifa, na lugha, wakatetemeka na kuogopa mbele yake; aliyetaka kumwua alimwua; na aliyetaka kumwacha hai, alimwacha hai; aliyetaka kumtukuza, alimtukuza; na aliyetaka kumshusha, alimshusha.

Lakini moyo wake ulipoinuliwa, na roho yake ilipokuwa ngumu akatenda kwa kiburi, aliuzuliwa katika kiti chake cha enzi, nao wakamwondolea utukufu wake.

Akafukuzwa mbali na wanadamu moyo wake ukafanywa kuwa kama moyo wa mnyama, na makao yake yalikuwa pamoja na punda - mwitu; akalishwa majani kama ng'ombe, mwili wake ukalowa maji kwa umande wa mbinguni; hata alipojua ya kuwa Mungu aliye juu ndiye anayewatawala katika ufalme wa wanadamu, na ya kuwa humweka juu yake yeye amtakaye, awaye yote.

Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI NA PERESI. Na tafsiri ya maneno haya ni hii;

MENE - Mungu ameuhesabu Ufalme wako na kuokomesha.

TEKELI - Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.

PERESI - Ufalme wako umegawanyika na wamepewa Wamedi na Waajemi.
 
Nami binafsi nashukuru sana kuona maandiko yanatimia!! Ni kutimia huku kwa maandiko; ndiko wale wenye macho na hawaoni na wana masikio lakini hawasiki; hatimae wataanza kuona wazi wazi "Malaika" akianza kunywa damu za kondoo wa Bwana!!!

Si wote walishaona ukuu aliopewa ameanza kuutumia kuua kwa aliyemtaka na kumwacha hai yule aliyemtaka!! Lakini taratibu, kadri siku zinavyoenda, maandiko yanaaza kudhihiri hata miongoni mwa wale wenye masikio ambao walishindwa kusikia kwa kipindi kirefu au wale wenye macho na kushindwa kuona!!!

Huyu Mtoto pekee ndio muujiza mkuu tulioletewa wanadamu ili hatimae vipofu waweze kuona na viziwi kusikia!!
 
Pamoja na maandiko funzo lingine tunalopata kwa issues zinazoendelea ni kwamba tunahitaji kuwa na Katiba imara yenye kuweka na kusimamia mihimili ya dola iliyo huru; yenye maamuzi yasiyoingiliwa au kuingiliana iwe moja kwa moja au kwa usiri (indirectly).

Kiufupi, bila Katiba imara hali itaendelea kuwa hivi hivi miaka nenda miaka rudi; hata aje malaika bila Katiba imara hakuna kitakachobadilika. 1. KATIBA 2. KATIBA 3. KATIBA. Kumbukeni yale maneno maarufu ya Mwl; "Kwa Katiba hii ..."
 
Nami binafsi nashukuru sana kuona maandiko yanatimia!! Ni kutimia huku kwa maandiko; ndiko wale wenye macho na hawaoni na wana masikio lakini hawasiki; hatimae wataanza kuona wazi wazi "Malaika" akianza kunywa damu za kondoo wa Bwana!!!

Si wote walishaona ukuu aliopewa ameanza kuutumia kuua kwa aliyemtaka na kumwacha hai yule aliyemtaka!! Lakini taratibu, kadri siku zinavyoenda, maandiko yanaaza kudhihiri hata miongoni mwa wale wenye masikio ambao walishindwa kusikia kwa kipindi kirefu au wale wenye macho na kushindwa kuona!!!

Huyu Mtoto pekee ndio muujiza mkuu tulioletewa wanadamu ili hatimae vipofu waweze kuona na viziwi kusikia!!

Nape , karibu Chadema tufanye kazi yenye nia njema kwa Taifa.
 
Nape , karibu Chadema tufanye kazi yenye nia njema kwa Taifa.
Na kwa Nape huyu sina shaka nae kwa hilo...!! Huko kwa JK aliendelea kuwa nao miaka yote hiyo kwa sababu JK anajua jinsi ya kuwa-handle watu wa aina ya Nape!!! Ndo maana kila wakati nawasisitizia watu tusimhukumu Nape kwa yale aliyokuwa anayafanya wakati akiwa Katibu Mwenezi wa CCM kwa sababu he's doing his job and there's no way anti-CCM angeweza kuyapenda yale... it's politics!! Kwahiyo nami nitafarijika sana akichukua huo uamuzi and I bet; atauchukua tu haidhuru hata kama sio leo au kesho!!!!
 
Back
Top Bottom