Men Talk 3: Mwanaume usizae na mchepuko

Men Talk 3: Mwanaume usizae na mchepuko

Bwana wee muda mwingine mitoto anayototolesha mke ni mijinga bora ukajaribu bahati nje huko.

Alafu hili suala la urithi, pale ambapo kuna watoto zaidi ya mmoja tegemea kabisa hizo mali kupigwa bei maana kila mtu na mtazamo wake na mipango yake maishani.
JF ni home of Great Thinker, Mkuu nawewe ni mmojawapo?
 
Mi nilikuwa naambiwa nataka nizae na wewe ntalea mwenyew.Baada ya kuzaa mambo yamekuwa tofauti.Hamna mwanamke kati ya wote niliozaa nao niliyepanga kuzaa naye.

Sent from my SM-G920F using JamiiForums mobile app
Kwamba na wewe ukaamua kweli kutoa mbegu zako zawadi? Haikugusa nafsini mwako kwamba unazalisha watoto ambao hutokuwa sehemu ya maisha yao, hutokuwa baba kwao?
 
Dunia hii ina kila aina ya matukio.

Wakati nasoma huu ujumbe, kuna Dada katoka kuniomba ushauri. Yeye ni mke wa mtu na mume wake amesafiri kikazi huu ni mwezi wa tatu yupo Mkoa mwingine. Dada amechanganyikiwa ametoka kupima amekutwa ana ujauzito. (Ni ujauzito wa mchepuko).

Ushauri niliompa: Nimemwambia aende huko alipo mumewe akamuonjeshe wiki nzima kisha arudi, halafu baadae aje amwambie mumewe kuwa ana ujauzito.

Dada kakubali ushauri wangu, pia ameniambia kuwa hata mtoto wake wa kwanza sio wa mumewe ni wa jamaa mwingine.

Aisee, wanawake Mungu anawaona.
Aiseee
 
Kwangu mie hizo titles ni ubatili. Maishani mie nataka kuwa kwenyewe kundi la people with great happiness.
 
Kuna uncle wetu mmoja, alikuwa ana mke karibia kila mkoa utafikiri jogoo wa kuazima...

Sasa alipofariki ishu ikawa ndugu kuanza kusomesha watoto wa marehemu, wanandugu wengine ikawalazimu hadi kuuza mali zao ili watoto wa kaka walau wasome...
Huyo alikua sugu
 
Dunia hii ina kila aina ya matukio.

Wakati nasoma huu ujumbe, kuna Dada katoka kuniomba ushauri. Yeye ni mke wa mtu na mume wake amesafiri kikazi huu ni mwezi wa tatu yupo Mkoa mwingine. Dada amechanganyikiwa ametoka kupima amekutwa ana ujauzito. (Ni ujauzito wa mchepuko).

Ushauri niliompa: Nimemwambia aende huko alipo mumewe akamuonjeshe wiki nzima kisha arudi, halafu baadae aje amwambie mumewe kuwa ana ujauzito.

Dada kakubali ushauri wangu, pia ameniambia kuwa hata mtoto wake wa kwanza sio wa mumewe ni wa jamaa mwingine.

Aisee, wanawake Mungu anawaona.
Mungu anawaona wakti wewe umemshauri akampe jamaa damu ambayo sio yako,wewe ndio umebeba dhambi zake
 
Dunia hii ina kila aina ya matukio.

Wakati nasoma huu ujumbe, kuna Dada katoka kuniomba ushauri. Yeye ni mke wa mtu na mume wake amesafiri kikazi huu ni mwezi wa tatu yupo Mkoa mwingine. Dada amechanganyikiwa ametoka kupima amekutwa ana ujauzito. (Ni ujauzito wa mchepuko).

Ushauri niliompa: Nimemwambia aende huko alipo mumewe akamuonjeshe wiki nzima kisha arudi, halafu baadae aje amwambie mumewe kuwa ana ujauzito.

Dada kakubali ushauri wangu, pia ameniambia kuwa hata mtoto wake wa kwanza sio wa mumewe ni wa jamaa mwingine.

Aisee, wanawake Mungu anawaona.
 
Hamna mwanamke atakayekidhi vigezo bwana wewe...ingekuwa hivyo watu tusingechepuka.

Mie baba kwakuendekeza kuchepuka tayari nina ujinga sasa ukikutana na mwanamme mjinga sii majanga
Mkuu sio kila mwanaume anamtazamo kama huo wa kwako. Kuwa na watoto wa nje sio sifa.

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Leo naomba tuongee kiume, wanaume wenzangu. Najua ni vigumu kuridhika na mwanamke mmoja uliyenae, ila hata kama tamaa ikikuzidia sio lazima uzae na mchepuko. Unajua katika familia, Baba ni kichwa, ila anayeifanya familia iwe na umoja ni Mama. Ndio maana Baba akitangulia, familia inatetereka sana, ila ni nadra sana umoja kupotea.

Makuzi na malezi ya watoto yanamtegemea sana Mama. Leo hii mwanaume ukiwa na watoto let say wanne, na kila mmoja akawa na mama yake, ni vigumu sana hao watoto kuishi kama familia moja, maana kila mmoja anamwalim wake, na pengine kila mmoja akawa anajiona ana haki kuliko wengine.

Ikitokea umechepuka leo, basi kidhi haja za mwili wako tu, ila ukihitaji mtoto rudi home kwa mkeo. Maana mzigo mkubwa utarudi kwa wanao hapo baadae na sio mkeo.

Ngoja nikupe mfano. Kuna familia moja ambayo mzee alikuwa na watoto watano, aliowapata kwa wanawake wanne tofauti. Watoto watatu wa mwanzo kila mmoja alikuwa na mama yake, ila hawa wawili wamwisho ndio walikuwa wa mama mmoja. Watoto wote wanajuana, ila kila mmoja alikulia kwa mama yake. Mtoto wa kwanza wakiume, wapili na watatu ni wakike, wawili wa mwisho ni wakiume pia. Bahati mbaya mzee alikuja akafariki, baada ya muda mwanamke (aliyezaa watoto wawili) nae akafariki. Misiba ilifatana kiasi. Baada ya msiba wa pili tu, watoto wakike wakubwa wakaibua mada ya kuuza nyumba. Mtoto wa kwanza alikuwa wa kiume na ni mtu mzima tayari mwenye familia yake, akajaribu kushauri kwamba hakuna haja ya kuuza nyumba. Akatoa wazo iendelee kupangishwa ili ipatikane hela ya kumhudumia mdogo wao wa mwisho aliyekuwa form 3.

Baada ya kubishana sana, kaka mkubwa ikabidi awaambie wale wadogo zake wakike ambao walikuwa wanataka nyumba iuzwe, kuwa endapo nyumba itauzwa basi wakubali jukumu la kumlea mdogo wao. Madada wakagoma. Kaka mkubwa akasema nyumba haitouzwa. Siku zikaenda, dogo alivyomaliza tu mtihani wa form 4, mada ya nyumba kuuzwa ikarudi maana dogo kamaliza shule. Baada ya vuta ni kuvute nyingi, nyumba ikauzwa, kila mmoja akaenda na njia yake hakuna aliyetaka kujua mdogo wao wa mwisho anaendeleaje.

Mfano mwingine ni jamaa alizaa nje ya ndoa, mkewe akamwambia ruka uwezavyo ila hapa kwangu sitolea mtoto wa mtu mwingine aliyechini ya umri wa wanangu. Matokeo yake mtoto anazurura tu, leo anaishi kwa bamdogo, kesho kwa mjomba n.k...mtoto wa hivi hata malezi yake hayawezi kuwa mazuri.

Mifano ya hivi ipo mingi sana, na victims ni watoto wala sio mkeo.

Chagua vizuri mke, then jenga familia. Ukichepuka sio lazima uweke mimba. Na mwanamke kama humuelewi, usiuze mechi. Hakuna mimba inayoingiaga bahati mbaya.

Mwanadam ametawaliwa na tamaa na kutoridhika, ila starehe yako ya leo haitakiwi kuwa mzigo kwa wengine siku zijazo.

Msibani inasomwa risala fupi ya marehemu kuwa aliacha watoto wanne, ila baada ya wiki wanajitokeza wengine wanne,kumbe anao 8. Alafu wengine mlivyo na damu kali, sio mpaka DNA kutambua watoto wenu.

Tuwaonee huruma watoto wetu. Our past may somehow define their future. Play safe.

Analyse
Ukifikiri (kwa kichwa kikubwa) hii hoja ina mantiki sana. ila sasa "wakati ule" ukifika hicho kichwa kikubwa hakifanyi kazi, kinaacha kazi zooote zifanywe na kichwa kidogo
 
Alikuwa na 'mawe', yakampa kiburi....

Alivyokata kamba akapotea na mawe yake, tabu akaiacha kwa ndugu zake...
Sasa hiyo timu yake amewaachia viamba vingapi?ukute shamba lake eka moja watoto wa kiume 12
 
Kuna uncle wetu mmoja, alikuwa ana mke karibia kila mkoa utafikiri jogoo wa kuazima...

Sasa alipofariki ishu ikawa ndugu kuanza kusomesha watoto wa marehemu, wanandugu wengine ikawalazimu hadi kuuza mali zao ili watoto wa kaka walau wasome...
Mmmm Kuna mtanzania kwel wa kufikia atua ya kuuza Mali zake ili watoto wa kaka zake wau watoto wa mdogo wake wasomee mswahili afanye hivyo?
 
Bwana wee muda mwingine mitoto anayototolesha mke ni mijinga bora ukajaribu bahati nje huko.

Alafu hili suala la urithi, pale ambapo kuna watoto zaidi ya mmoja tegemea kabisa hizo mali kupigwa bei maana kila mtu na mtazamo wake na mipango yake maishani.
Kama unazaa na mkeo watoto, wote wanakua wajinga, unahitimisha vipi kuwa ni sababu ya mkeo na sio wewe?
 
Mmmm Kuna mtanzania kwel wa kufikia atua ya kuuza Mali zake ili watoto wa kaka zake wau watoto wa mdogo wake wasomee mswahili afanye hivyo?
Hapa naongelea miaka mingi iliyopita wakati wanadamu walikuwa na imani, hiyo ilikuwa in the 80's

Pengine kwa sasa isiwe rahisi vile watu wapo radhi kuchangiana mambo ya starehe/sherehe na si ya maendeleo
 
Back
Top Bottom