Men Talk 3: Mwanaume usizae na mchepuko

Analyse

JF-Expert Member
Jan 19, 2014
16,266
41,060
Leo naomba tuongee kiume, wanaume wenzangu. Najua ni vigumu kuridhika na mwanamke mmoja uliyenae, ila hata kama tamaa ikikuzidia sio lazima uzae na mchepuko. Unajua katika familia, Baba ni kichwa, ila anayeifanya familia iwe na umoja ni Mama. Ndio maana Baba akitangulia, familia inatetereka sana, ila ni nadra sana umoja kupotea.

Makuzi na malezi ya watoto yanamtegemea sana Mama. Leo hii mwanaume ukiwa na watoto let say wanne, na kila mmoja akawa na mama yake, ni vigumu sana hao watoto kuishi kama familia moja, maana kila mmoja anamwalim wake, na pengine kila mmoja akawa anajiona ana haki kuliko wengine.

Ikitokea umechepuka leo, basi kidhi haja za mwili wako tu, ila ukihitaji mtoto rudi home kwa mkeo. Maana mzigo mkubwa utarudi kwa wanao hapo baadae na sio mkeo.

Ngoja nikupe mfano. Kuna familia moja ambayo mzee alikuwa na watoto watano, aliowapata kwa wanawake wanne tofauti. Watoto watatu wa mwanzo kila mmoja alikuwa na mama yake, ila hawa wawili wamwisho ndio walikuwa wa mama mmoja. Watoto wote wanajuana, ila kila mmoja alikulia kwa mama yake. Mtoto wa kwanza wakiume, wapili na watatu ni wakike, wawili wa mwisho ni wakiume pia. Bahati mbaya mzee alikuja akafariki, baada ya muda mwanamke (aliyezaa watoto wawili) nae akafariki. Misiba ilifatana kiasi. Baada ya msiba wa pili tu, watoto wakike wakubwa wakaibua mada ya kuuza nyumba. Mtoto wa kwanza alikuwa wa kiume na ni mtu mzima tayari mwenye familia yake, akajaribu kushauri kwamba hakuna haja ya kuuza nyumba. Akatoa wazo iendelee kupangishwa ili ipatikane hela ya kumhudumia mdogo wao wa mwisho aliyekuwa form 3.

Baada ya kubishana sana, kaka mkubwa ikabidi awaambie wale wadogo zake wakike ambao walikuwa wanataka nyumba iuzwe, kuwa endapo nyumba itauzwa basi wakubali jukumu la kumlea mdogo wao. Madada wakagoma. Kaka mkubwa akasema nyumba haitouzwa. Siku zikaenda, dogo alivyomaliza tu mtihani wa form 4, mada ya nyumba kuuzwa ikarudi maana dogo kamaliza shule. Baada ya vuta ni kuvute nyingi, nyumba ikauzwa, kila mmoja akaenda na njia yake hakuna aliyetaka kujua mdogo wao wa mwisho anaendeleaje.

Mfano mwingine ni jamaa alizaa nje ya ndoa, mkewe akamwambia ruka uwezavyo ila hapa kwangu sitolea mtoto wa mtu mwingine aliyechini ya umri wa wanangu. Matokeo yake mtoto anazurura tu, leo anaishi kwa bamdogo, kesho kwa mjomba n.k...mtoto wa hivi hata malezi yake hayawezi kuwa mazuri.

Mifano ya hivi ipo mingi sana, na victims ni watoto wala sio mkeo.

Chagua vizuri mke, then jenga familia. Ukichepuka sio lazima uweke mimba. Na mwanamke kama humuelewi, usiuze mechi. Hakuna mimba inayoingiaga bahati mbaya.

Mwanadam ametawaliwa na tamaa na kutoridhika, ila starehe yako ya leo haitakiwi kuwa mzigo kwa wengine siku zijazo.

Msibani inasomwa risala fupi ya marehemu kuwa aliacha watoto wanne, ila baada ya wiki wanajitokeza wengine wanne,kumbe anao 8. Alafu wengine mlivyo na damu kali, sio mpaka DNA kutambua watoto wenu.


Tuwaonee huruma watoto wetu. Our past may somehow define their future. Play safe.

Analyse
 
Be responsible
1538149479.jpg
 
Bwana wee muda mwingine mitoto anayototolesha mke ni mijinga bora ukajaribu bahati nje huko.

Alafu hili suala la urithi, pale ambapo kuna watoto zaidi ya mmoja tegemea kabisa hizo mali kupigwa bei maana kila mtu na mtazamo wake na mipango yake maishani.
 
Sisi wanaume wengi wa kiafrika ni selfish sana. Kwa sababu tu unakuwa na uwezo wa kuwahudumia wanawake wengi, unakuwa unaona kwamba ni ufahari kuwa na familia zaidi ya moja, mbaya zaidi matokeo yake yanakuja kuonekana muda umeshaenda na hakuna cha kurekebika tena.
 
Acha woga, wapo watoto wa nje wenye mafanikio
Swala sio uoga au mafanikio. Yawezekana ukawa na watoto na mke mmoja ila wasipate mafanikio makubwa.

Kuzaa kila sehemu ina side effects kubwa sana, hasa katika migogoro isiyokuwa na tija. Maana ya familia ni ukaribu na umoja. Pasipo na umoja, familia lazima ilege lege, then ndio mtaanza kusema zile kauli zenu "DAMU ILIKUWA NZITO ZAMANI, SIKU HIZI KUNA MARAFIKI WANAOTUELEWA KULIKO NDUGU."
 
Bwana wee muda mwingine mitoto anayototolesha mke ni mijinga bora ukajaribu bahati nje huko.

Alafu hili suala la urithi, pale ambapo kuna watoto zaidi ya mmoja tegemea kabisa hizo mali kupigwa bei maana kila mtu na mtazamo wake na mipango yake maishani.
Take time, chagua mke atayekidhi vigezo vyako. What if ukienda kujaribu nje, ila nako ukatoa watoto wajinga then unagundua ujinga unatoka kwako na sio kwa mama watoto?
 
Sisi wanaume wengi wa kiafrika ni selfish sana. Kwa sababu tu unakuwa na uwezo wa kuwahudumia wanawake wengi, unakuwa unaona kwamba ni ufahari kuwa na familia zaidi ya moja, mbaya zaidi matokeo yake yanakuja kuonekana muda umeshaenda na hakuna cha kurekebika tena.
Tunafikiria kuhudumia wengi, ila kidogo kidogo, badala ya kuhudumia wachache kwa kiwango sahihi
 
Take time, chagua mke atayekidhi vigezo vyako. What if ukienda kujaribu nje, ila nako ukatoa watoto wajinga then unagundua ujinga unatoka kwako na sio kwa mama watoto?
Hamna mwanamke atakayekidhi vigezo bwana wewe...ingekuwa hivyo watu tusingechepuka.

Mie baba kwakuendekeza kuchepuka tayari nina ujinga sasa ukikutana na mwanamme mjinga sii majanga
 
Back
Top Bottom