Men Talk 3: Mwanaume usizae na mchepuko

Men Talk 3: Mwanaume usizae na mchepuko

Swala sio uoga au mafanikio. Yawezekana ukawa na watoto na mke mmoja ila wasipate mafanikio makubwa.

Kuzaa kila sehemu ina side effects kubwa sana, hasa katika migogoro isiyokuwa na tija. Maana ya familia ni ukaribu na umoja. Pasipo na umoja, familia lazima ilege lege, then ndio mtaanza kusema zile kauli zenu "DAMU ILIKUWA NZITO ZAMANI, SIKU HIZI KUNA MARAFIKI WANAOTUELEWA KULIKO NDUGU."
Mi niseme tu.
Napenda sana aina yako ya kufikiri.

Reasoning yako huwa nakuelewa mpk dah!!
 
Acha kuchepuka mara moja kabla sijascreenshot na kupost kwenye uzi wa selfie braza angu Jack aone..sawa?

Kaka yako anajua kabisa kuwa napachikwa majina humu na watu..
Ila anajua jinsi ninavyompenda na nilivyo mwaminifu..
I love that man acha kabisa , tena ile bahati inaweza mdondokea.
 
Wewe ndio baba yao na watoto ni ndugu zako hawana ndugu mwingine zaidi yako, na wewe ndio kichwa Chao hivyo ni jukumu lako kuwakusanya na kuwaunganisha na wafahamiane mapema Sana na uwajengee misimgi ya umoja tangu wakiwa wadogo.

Hawa wanawake sio wa kuwagikiria Sana ndio maana hata kesho akisepa anabadilisha tu kutoka Mrs x to Mrs y na hakuna wa kumpangia.

So pamoja na mifano yako mwanaume kuwa na msimamo pamoja na madhaifu yako. Hata Kama umezalisha inje simamia msimamo wako juu ya matunda ya uzinzi wako.

Watoto ndio ndugu zako na ni damu yako , kabila lako , dini yako Kila kitu chako hivyo ni jukumu lako kuwalinda na kutungua miladi ya kuwaunganisha.

Usiache tamaana na roho mbaya ya huyo mwanamke kwa jina la mke/mchumba/mzazi mwenza vitese damu yako .....maana mwisho wa siku machozi ya hao watoto yatakulilia wewe na sio huyo mwanamke wako.


Men wakeup....... it's time for Sex and money not love and sex Hawa wanawake wame change sio wale tulio kalilishwa na Bibi na mama zetu....Hawa ni wengine kabisa....

mbona huu mwandiko kama naujua
Anyway hii mada wacha niwe msomaji maana inanigusa kunako nisije kujiharibia siku bure
 
Leo naomba tuongee kiume, wanaume wenzangu. Najua ni vigumu kuridhika na mwanamke mmoja uliyenae, ila hata kama tamaa ikikuzidia sio lazima uzae na mchepuko. Unajua katika familia, Baba ni kichwa, ila anayeifanya familia iwe na umoja ni Mama. Ndio maana Baba akitangulia, familia inatetereka sana, ila ni nadra sana umoja kupotea.

Makuzi na malezi ya watoto yanamtegemea sana Mama. Leo hii mwanaume ukiwa na watoto let say wanne, na kila mmoja akawa na mama yake, ni vigumu sana hao watoto kuishi kama familia moja, maana kila mmoja anamwalim wake, na pengine kila mmoja akawa anajiona ana haki kuliko wengine.

Ikitokea umechepuka leo, basi kidhi haja za mwili wako tu, ila ukihitaji mtoto rudi home kwa mkeo. Maana mzigo mkubwa utarudi kwa wanao hapo baadae na sio mkeo.

Ngoja nikupe mfano. Kuna familia moja ambayo mzee alikuwa na watoto watano, aliowapata kwa wanawake wanne tofauti. Watoto watatu wa mwanzo kila mmoja alikuwa na mama yake, ila hawa wawili wamwisho ndio walikuwa wa mama mmoja. Watoto wote wanajuana, ila kila mmoja alikulia kwa mama yake. Mtoto wa kwanza wakiume, wapili na watatu ni wakike, wawili wa mwisho ni wakiume pia. Bahati mbaya mzee alikuja akafariki, baada ya muda mwanamke (aliyezaa watoto wawili) nae akafariki. Misiba ilifatana kiasi. Baada ya msiba wa pili tu, watoto wakike wakubwa wakaibua mada ya kuuza nyumba. Mtoto wa kwanza alikuwa wa kiume na ni mtu mzima tayari mwenye familia yake, akajaribu kushauri kwamba hakuna haja ya kuuza nyumba. Akatoa wazo iendelee kupangishwa ili ipatikane hela ya kumhudumia mdogo wao wa mwisho aliyekuwa form 3.

Baada ya kubishana sana, kaka mkubwa ikabidi awaambie wale wadogo zake wakike ambao walikuwa wanataka nyumba iuzwe, kuwa endapo nyumba itauzwa basi wakubali jukumu la kumlea mdogo wao. Madada wakagoma. Kaka mkubwa akasema nyumba haitouzwa. Siku zikaenda, dogo alivyomaliza tu mtihani wa form 4, mada ya nyumba kuuzwa ikarudi maana dogo kamaliza shule. Baada ya vuta ni kuvute nyingi, nyumba ikauzwa, kila mmoja akaenda na njia yake hakuna aliyetaka kujua mdogo wao wa mwisho anaendeleaje.

Mfano mwingine ni jamaa alizaa nje ya ndoa, mkewe akamwambia ruka uwezavyo ila hapa kwangu sitolea mtoto wa mtu mwingine aliyechini ya umri wa wanangu. Matokeo yake mtoto anazurura tu, leo anaishi kwa bamdogo, kesho kwa mjomba n.k...mtoto wa hivi hata malezi yake hayawezi kuwa mazuri.

Mifano ya hivi ipo mingi sana, na victims ni watoto wala sio mkeo.

Chagua vizuri mke, then jenga familia. Ukichepuka sio lazima uweke mimba. Na mwanamke kama humuelewi, usiuze mechi. Hakuna mimba inayoingiaga bahati mbaya.

Mwanadam ametawaliwa na tamaa na kutoridhika, ila starehe yako ya leo haitakiwi kuwa mzigo kwa wengine siku zijazo.

Msibani inasomwa risala fupi ya marehemu kuwa aliacha watoto wanne, ila baada ya wiki wanajitokeza wengine wanne,kumbe anao 8. Alafu wengine mlivyo na damu kali, sio mpaka DNA kutambua watoto wenu.


Tuwaonee huruma watoto wetu. Our past may somehow define their future. Play safe.

Analyse
Picha
 
acha tu my dear
Wanaume kuna stress wanajitakia wenyewe hata kama hapa wana jimwambafy kuwa hawajali etc ila chamoto wana kiona
Wafate tu ushauri wa mleta mada hapa kama wanaipenda amani ya moyo
Natamani ushee kidogo stori yako jamani

Ukweli ni kwamba hapa watajikaza tu kukataa lakini alichoongea mtoa mada ni Cha kweli kabisa na anajua anachokiongea maana naye yupo kwenye hilo kundi(samahani Analyse)
 
Natamani ushee kidogo stori yako jamani

Ukweli ni kwamba hapa watajikaza tu kukataa lakini alichoongea mtoa mada ni Cha kweli kabisa na anajua anachokiongea maana naye yupo kwenye hilo kundi(samahani Analyse)

Siku nikipata nguvu nitalielezea hili
Maana kwa sasa nimelitoa akilini ili lisinisumbue kichwa
Ila huko mbeleni nitalirudia
Nawaza kama mimi linanisumbua hivi je baba muhusika mkuu sipati picha anapitia hali gani
So sad
 
Siku nikipata nguvu nitalielezea hili
Maana kwa sasa nimelitoa akilini ili lisinisumbue kichwa
Ila huko mbeleni nitalirudia
Nawaza kama mimi linanisumbua hivi je baba muhusika mkuu sipati picha anapitia hali gani
So sad
Elezea hata kidogo best..
 
Back
Top Bottom