Men Talk 3: Mwanaume usizae na mchepuko

Men Talk 3: Mwanaume usizae na mchepuko

Kuna uncle wetu mmoja, alikuwa ana mke karibia kila mkoa utafikiri jogoo wa kuazima...

Sasa alipofariki ishu ikawa ndugu kuanza kusomesha watoto wa marehemu, wanandugu wengine ikawalazimu hadi kuuza mali zao ili watoto wa kaka walau wasome...
Ohooo...
 
Hujui convincing power ya mama kwa mtoto. Kama huishi nao, basi jua kwa asilimia kubwa atasikilizwa mama
Hata wewe ukiwa karibu na mwanao utakuwa na convincing power .....sema madingi tunajitenga Sana na sisi tinazani kazi yetu ni kufoka foka tu na kuchapa
 
Hata wewe ukiwa karibu na mwanao utakuwa na convincing power .....sema madingi tunajitenga Sana na sisi tinazani kazi yetu ni kufoka foka tu na kuchapa
Nature ya kazi zetu ndio inaminya muda wa kutulia chini na watoto.

Ila pia ki hasilo tu, mtoto yupo attracted sana kwa mama kuliko baba.
 
Mbona mnapingana na kauli na usia wa Rais wetu Marehemu JPM alisema zaeni sana msiwasikilize wazungu.
Sasa mm mke wangu niliyenaye anaonesha kachoka na nyodo kibao, huduma sipewi na nina hamu bado ya watoto kwanini mnifunge niwe mpweke kwani watoto nilionao ni wa kike wawili tu wakikua wataolewa.
Tuige mifano ya viongozi wetu tusiwafuate wazungu au wachina kuwa na mtoto mmoja sio deal kabisa
Mishe mishe unazofanya zinaruhusu kupata hela ya kula siku hiyo. Alaf bado unataka umiliki watoto kila mtaa
 
Aisee binafsi hadi mda huu nina watoto 4 ila mtoto mmoja ndio mama mwingine kusema kweli changamoto zipo na ukiwa kichwa panzi unaweza ukatelekeza damu yako hivihivi.

Halafu haya mambo sometimes mpangaji ni Sir God ndugu zangu mana unaweza kujitahidi kujichunga wee lakini wapi unakujakuta paah...! kitu kimejipa.

Hivyo kwa sisi tuliozalisha nje ya ndoa tusiogope maneno ya jamii, wanaukoo, dini wala mke tubebe jukumu la kulea watoto.

Tusikimbie watoto wetu, damu zetu, ndugu zetu tena kama unao na unajificha jitahidi kuwapeleka na kuwatambulisha kwenu kwa ndugu, jamaa, marafiki, mke wako na watoto wako.
 
Leo naomba tuongee kiume, wanaume wenzangu. Najua ni vigumu kuridhika na mwanamke mmoja uliyenae, ila hata kama tamaa ikikuzidia sio lazima uzae na mchepuko. Unajua katika familia, Baba ni kichwa, ila anayeifanya familia iwe na umoja ni Mama. Ndio maana Baba akitangulia, familia inatetereka sana, ila ni nadra sana umoja kupotea.

Makuzi na malezi ya watoto yanamtegemea sana Mama. Leo hii mwanaume ukiwa na watoto let say wanne, na kila mmoja akawa na mama yake, ni vigumu sana hao watoto kuishi kama familia moja, maana kila mmoja anamwalim wake, na pengine kila mmoja akawa anajiona ana haki kuliko wengine.

Ikitokea umechepuka leo, basi kidhi haja za mwili wako tu, ila ukihitaji mtoto rudi home kwa mkeo. Maana mzigo mkubwa utarudi kwa wanao hapo baadae na sio mkeo.

Ngoja nikupe mfano. Kuna familia moja ambayo mzee alikuwa na watoto watano, aliowapata kwa wanawake wanne tofauti. Watoto watatu wa mwanzo kila mmoja alikuwa na mama yake, ila hawa wawili wamwisho ndio walikuwa wa mama mmoja. Watoto wote wanajuana, ila kila mmoja alikulia kwa mama yake. Mtoto wa kwanza wakiume, wapili na watatu ni wakike, wawili wa mwisho ni wakiume pia. Bahati mbaya mzee alikuja akafariki, baada ya muda mwanamke (aliyezaa watoto wawili) nae akafariki. Misiba ilifatana kiasi. Baada ya msiba wa pili tu, watoto wakike wakubwa wakaibua mada ya kuuza nyumba. Mtoto wa kwanza alikuwa wa kiume na ni mtu mzima tayari mwenye familia yake, akajaribu kushauri kwamba hakuna haja ya kuuza nyumba. Akatoa wazo iendelee kupangishwa ili ipatikane hela ya kumhudumia mdogo wao wa mwisho aliyekuwa form 3.

Baada ya kubishana sana, kaka mkubwa ikabidi awaambie wale wadogo zake wakike ambao walikuwa wanataka nyumba iuzwe, kuwa endapo nyumba itauzwa basi wakubali jukumu la kumlea mdogo wao. Madada wakagoma. Kaka mkubwa akasema nyumba haitouzwa. Siku zikaenda, dogo alivyomaliza tu mtihani wa form 4, mada ya nyumba kuuzwa ikarudi maana dogo kamaliza shule. Baada ya vuta ni kuvute nyingi, nyumba ikauzwa, kila mmoja akaenda na njia yake hakuna aliyetaka kujua mdogo wao wa mwisho anaendeleaje.

Mfano mwingine ni jamaa alizaa nje ya ndoa, mkewe akamwambia ruka uwezavyo ila hapa kwangu sitolea mtoto wa mtu mwingine aliyechini ya umri wa wanangu. Matokeo yake mtoto anazurura tu, leo anaishi kwa bamdogo, kesho kwa mjomba n.k...mtoto wa hivi hata malezi yake hayawezi kuwa mazuri.

Mifano ya hivi ipo mingi sana, na victims ni watoto wala sio mkeo.

Chagua vizuri mke, then jenga familia. Ukichepuka sio lazima uweke mimba. Na mwanamke kama humuelewi, usiuze mechi. Hakuna mimba inayoingiaga bahati mbaya.

Mwanadam ametawaliwa na tamaa na kutoridhika, ila starehe yako ya leo haitakiwi kuwa mzigo kwa wengine siku zijazo.

Msibani inasomwa risala fupi ya marehemu kuwa aliacha watoto wanne, ila baada ya wiki wanajitokeza wengine wanne,kumbe anao 8. Alafu wengine mlivyo na damu kali, sio mpaka DNA kutambua watoto wenu.


Tuwaonee huruma watoto wetu. Our past may somehow define their future. Play safe.

Analyse
Seconded! unajua kuzaa nje ya ndoa ni utovu wa nidhamu, unajidhalilisha wewe kama mwanaume kichwa cha familia. Huwa najiuliza kitu fulani, hivi hayo unayotafuta huko nje, unashindwa kumwambia mke afanye? au ndio hela ikizidi inabidi utafute wa kutumia nae.

Ni vizuri wanaume muanze kukaa kwenye nafasi zenu. Kama kuna kitu mkeo anashindwa kukufanyia ndio kinaplekea wewe kwenda nje kutafuta matatizo, kuna shida hapo.

Mawasiliano ni muhimili wa mahusiano!
 
Nature ya kazi zetu ndio inaminya muda wa kutulia chini na watoto.

Ila pia ki hasilo tu, mtoto yupo attracted sana kwa mama kuliko baba.
Ingekua rahisi ningekukaribisha kwangu uone ....wanangu wote wananikubali ...na kina huyo mdogo wa miezi asilimia kubwa kwa mama yake zinampeleka shughuli za kunyonya tu Hadi mama yake anakamind ......

Sema watu wengi wanafeli hasa sisi wanaume ...unapo kuwa na mtoto kuwa mtoto hadi na kimfanyisha utoto wenye kumkuza kwenye kumjenga kimichezo/kinidham/ nk ..

Kama wamama wafanyavyo kuimba vinyimbo vya kitoto kucheza nao michezo ya kitoto ndio maana wanakuwa connected nao sana na wakizingua wanawachapa lkn connection haifi.


Lean to copy with them pale unapo pata muda wa kuwa nao hapo ndio uyashika akili zao na kuwaongoza katika Yale upendayo wawe na ukifanikisha hili huki kutumia kiboko maana utakua unasema tu na wanakusikiliza .


Mtoto ana utoto kichwani kwake hivyo ili kwenda nae sawa nenda nae kupitia utoto wake.
 
Seconded! unajua kuzaa nje ya ndoa ni utovu wa nidhamu, unajidhalilisha wewe kama mwanaume kichwa cha familia. Huwa najiuliza kitu fulani, hivi hayo unayotafuta huko nje, unashindwa kumwambia mke afanye? au ndio hela ikizidi inabidi utafute wa kutumia nae.

Ni vizuri wanaume muanze kukaa kwenye nafasi zenu. Kama kuna kitu mkeo anashindwa kukufanyia ndio kinaplekea wewe kwenda nje kutafuta matatizo, kuna shida hapo.

Mawasiliano ni muhimili wa mahusiano!
Akili za watu walio tawaliwa na wake zao ndio hua zipo hivi

Ukisha ona Jambo linafanywa na watu wengi na jamii haidhuriki tatuta njia ya kulifanya lisiwe la kihalifu ila liwe la kujenga.kwa sasa watoto walio nje ya ndoa ni wengi mno kwa nini waendelee kuzurumiwa haki zao kwa kisingizio Cha heshima ya mke sijui jamiii..?

Wanume unatakiwa tuwe responsible na matokeo ya matendo yetu maana ndio fungu tulilo lichagua .

Okoa watoto wa nje ya ndoa sio kuwakandamiza. Wale hawana makosa
 
Bwana wee muda mwingine mitoto anayototolesha mke ni mijinga bora ukajaribu bahati nje huko.

Alafu hili suala la urithi, pale ambapo kuna watoto zaidi ya mmoja tegemea kabisa hizo mali kupigwa bei maana kila mtu na mtazamo wake na mipango yake maishani.
Kwahiyo mitoto mijinga inatoa ujinga kwa mama yao? Unakosea si ajabu maujinga yakawa yanatoka kwako mwenyewe kila unakopanda ujinga ule ule acha hizo!
 
Ninacho kiamini nikwamba hakuna mwanaume anaependa kua na watoto wa mama tofauti bila sababu za msingi. Ni changamoto tu ndizo hupelekea mwisho wa siku hilo kutokea.
Hakuna kitu kama hicho
 
kuna mzee mke wake alikuwa anazaa watoto wa kike tu akaenda nje kutafuta wa kiume
Kwahiyo hapo shida ilikuwa ni mkewe kuzaa watoto wa kike au yeye mwenyewe, na huko nje mara nyingi huwa wanapewa au kuuziwa mbuzi kwenye gunia
 
Kwann usimchukue mmoja kati ya hao unao wagegeda ukamuweka ndani kama mke?
Kwa sababu tumekubaliana kuwa hapa sie ni kigegedana tuu
Kwahiyo mitoto mijinga inatoa ujinga kwa mama yao? Unakosea si ajabu maujinga yakawa yanatoka kwako mwenyewe kila unakopanda ujinga ule ule acha hizo!
Ah sasa ili kuthibitisha kuwa ujinga ni kutoka kwangu mie sii ndio lazima nikazalishe huko nje tuone ukweli wa mambo
 
Kwa sababu tumekubaliana kuwa hapa sie ni kigegedana tuu

Ah sasa ili kuthibitisha kuwa ujinga ni kutoka kwangu mie sii ndio lazima nikazalishe huko nje tuone ukweli wa mambo
Aise ili uwe nao wengi haaa haaa
 
Back
Top Bottom