Freeland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2012
- 14,481
- 10,233
Hawa akina Museveni, Kagame na Kenyata baada ya kupima kina cha maji ya Kikwete na kukuta yana kina ambacho hawawezi wala kuthubutu kuogelea, wamejikuta ndani ya minority group kwa siku zijazo, hivyo kuamua kivyao kujaribu kutafuta njia mbadala kujinusuru.
Jambo moja la Msingi ambalo Kikwete atakumbukwa siku za usoni ni hili la kuitangaza Tanzania kwa mataifa, Tanzania ya leo si ile ya siku za nyuma iliyotumiwa na Kenya vivutio vyake kutumika kupitishia watalii Kenya.
Binafsi naona tu njia walizotumia ni utashi wa viongozi wa juu wa nchi na wala si matakwa ya wananchi wao, hivyo mambo ya uchumi wa dunia ya leo unabaki kuwa huru na katu huwezi Kikwete hawezi niwekea mipaka mie kupitishia mizigo yangu bandari ya Beira - Msumbiji au kwengineko ndivyo yatakayowapata hawa viongozi wa utatu.
Tanzania inahitaji tu kuboresha njia za usafirishaji na hivyo ukaribu wa bandari ya Tanzania kwa nchi za Rwanda na Burundi una nafasi bado. Uganda nao wako katikati, lakini kuna kilichowavutia wakati ule kupitishia mizigo yao bandari ya Dar sijui kama sababu zimetoweka kwa hoja zipi.
Tishio la ugaidi la Wasomali lisipothibitiwa kutosha ni kitu kinachoweza kusitisha mipango ya kutumia bandari ya Mombasa.
Mkuu kuna njia njingi za kuzuia importation kutoka nchi fulani.Ni rahisi kwa nchi hizo kupandisha Import Tarrifs ili ku discourage importation from Tanzania.Lakini hili hua linafanyika kwa bidhaa ambazo sio necessities kwa sababu ukipandisha tarrifs kwa necessities ambazo nchi yako lazima ifanye importation utakua uanatengeneza njia ya Inflation.