Membe sio mmiliki wa Naf Beach Hotel

Membe sio mmiliki wa Naf Beach Hotel

Hili suala lilishafanyiwa uchunguzi na vyombo husika na ukweli umeshajulikana: Membe sio mmiliki wa NAF, FAN city, wala NAF blue Hotel.

NAF inasimama badala ya herufi za majina ya wototo wa mmiliki halali Shaibu Mohamed Juma. Watoto wanaounda NAF au FAN city ni Nadhir Abdul na Farid. Hotel hizo zilijengwa tangu enzi za utawala wa Mkapa kabla Membe hajawa Waziri. NAF beach ilichelewa kuanza kazi kwasababu ya kuchelewa kwa mkopo kutoka crdb uliombwa na mmiliki. Mkopo ulitoka mwakajuzi na hivyo hotel kuanza.

Ifahamike kwamba Chadema, takukuru, usalama wa Taifa, kamati ya maadili ya ccm na Cuf walishafanya uchunguzi juu ya hotel hii na wote wakaja na jibu moja: Membe hana biashara ya hoteli sehemu yeyote duniani. Wote wamejiridhisha kwamba upo uhusiano wa kawaida wa kirafiki kati ya bwana Shaibu Juma na familia ya Membe. Sawa na uhusiano uliopo kati ya mmiliki wa Serena hotel na Membe.

Uchunguzi wa mwisho na wakaribuni ni ule uliofanyika na mahasimu wa Membe ndani ya CCM. Huu nao haujamweka Membe kama mmiliki wa hotel lakini mahasimu hawa wameamua walazamishe kesi kwasababu hawana kesi. Wakati EPA Richmond Rada Tokomeza na Escrow vimekuwa vikiwasumbua mahasimu wa Membe, Membe amekuwa msafi Wakati wote.

Mahasimu hao pia wamekuwa wakitapatapa kwamba Membe kala ela za Ghadafi. Ni nchi gani duniani ambapo misaada au msamaha wa madeni unapitishiwa kwenye account ya waziri wa mambo ya nje? Kwa taarifa zilizo sahihi ni kwamba wanasheria waliotuingiza mkenge Escrow ndio wanaosambaza habari za uongo kwasababu Membe alikataa ombi lao la kuitambua kampuni ya MELt kuwa mmiliki halali wa fedha zilizopo TIB badala yake akatambua MEIS company kama ambavyo ilihainishwa na serikali ya Libya. Huwezi kumwingiza Membe mkenge hata siku moja na Tz tungepata viongozi wa aina ya Membe ambao wako makini na wametenganisha siasa na biashara tungekuwa mbali. Mbali sana.

Naona Mgonjwa umeongea facts ambazo wadau wamekuwa wapole kupingana na taarifa yako. Basi Nimekubali BCM hausiki na umiliki wa hizo hotel.
 
Ahaaa Haa Haaa, yaani wa kukanusha wako wengi hata chenge atasema jina mliloliona kwenye paylol ya Ruge si jina langu bali mdogo wangu aitwaye endrew
 
That is a good statement though wanaoeneza uongo huo watakuja kutuambia kama wana ushahidi wa tuhuma zao
 
Mkuu unajitahidi kufanya "racking " ya nguvu kwa mh.
Yote tisa kumi ni kama angekuja mh. mwenyewe hapa jukwaani kukanusha
​ndugu yangu kutengeneza ID ni suala la DK tu unaweza kukuta huyo aliyeweka bandiko ndo Membe mwenyewe
 
membe sio fisadi km yule ****vi wa kaskazini watu wa pwani sie wastaarabu hatuna khulka ya wizi
 
Uraisi shida kweli..Membe nae kaingiza jeshi.by the way naomba kuuliza maswali kama manne tuu

1. Ni nani huyu Shebby mix?historia yake.

2.Ni nan washirika wa biashara,watu wa karibu wa Sheby mix.(hapa kuondoa dhana Shebby mix sio watchdog)

3.Biashara zq huyu bwana uki reflect a.k.a yake ya Shebby MIXX.

4.ushahidi wa huo mkopo(maana inaonekana unalifaham hili suala vizur kias cha kujua hadi chanzo cha mtaji wa kujenga hiyo hotel).

Ni hayo tuu

Bwana Mapesa maswali yako ni mazuri sana. Niseme tu kwamba Membe hayuko responsible kuelezea maisha ya Shebby (Shaibu Mohamed Juma) na sidhani kama sisi hapa tupo responsible. Swali lililo mbele yetu ni je Membe anamiliki hotel Mtwara? Kuchunguza Shebby ni nani kihistoria hakujibu swali la msingi.

Ajabu tumedangamywa na kuaminishwa kwamba Shebby ni masikini huwezi kujenga hotel. Hata baada ya mmiliki kuongelea kupitia TV na radio historia yake na jinsi alivyopata utajiri wake. Lakini hao wanaotuaminisha hawana hesabu ya utajiri wa Sheby ambao unaweza kuwa wa urithi au umiliki wa maeneo mengi ya ufukweni ambayo kwa miaka ya karibuni yamenufaisha wakazi wa Mtwara.

Ifahamike Shebby ni dalali makubwa wa ununuzi wa korosho kutoka vyama vya ushirika kwenda kwa makampuni ya wahindi. Kinadhalia Udalali auhitaji mtaji na malipo yake ni makubwa nayapamoja. Kama Shebby anaweza kushinda mnada moja na akamchaji muhindi shilingi 10 kwa kila kilo aliyoshinda manake anapata billion moja kwenye tani laki moja. Hapo hajafanya organization ya transport kwa kilo kutoka mnadani hadi ghalani.

Shebby alikuwa mfanyabiashara wa simu kariakoo lakini mwanzoni mwa miaka ya 2000 alirudi kwao Mtwara mara baada ya kugundua kwamba udalali wa korosho unalipa. Akauza maduka yake ya simu aliyokuwa anamiliki kariakoo. Madalali wengine walioungana naye ni pamoja na bwana Salum Mkemi ambaye bado makazi yake ni Dar.

Shebby ni mfano wa kuigwa kwa vijana wanaodhani Dar ndio kila kitu. Shebby amekuwa akiiomba serikali iwawezeshe wanunuzi wa korosho wakizalendo kuuza korosho zao moja kwa moja inchi za nje. Tatizo, alijibiwa kwamba wahindi wamezuia kununua korosho kutoka kwenye nchi zinazolima pasipo kupitia makampuni yao ya India. Kila miezi kadhaa Shebby amekuwa akifanya mahojiano na TV akielezea jinsi alivyopata utajiri wake na ujumbe wake kwa vijana. Kwa kudhani Shebby huwezi kujenga hotel ni kudharau jitihada zake.

Tujifunze kupongeza na kutia nguvu vijana waliotoka jasho na wakafanikiwa. Tusiache wanasiasa watukatishe tamaa kwa kusema hatuwezi.
 
Habari watanzania wenzangu wapenda amani na maendeleo.Napenda kuchukua nafasi hii kutolea ufafanuzi suala la nani ni mmiliki wa Naf Beach Hotel iliyopo mkoani Mtwara.Kumekuwa na habari zikisambaa kwa muda mrefu sasa juu ya kuhusishwa kwa Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika umiliki wa hoteli hii ya nyota tano.

Ukweli ni kwamba Membe hajawahi kumiliki au kuwa sehemu ya umiliki wa hoteli hii.Membe hajawahi kufanya biashara.Kumhusisha Membe na umiliki wa Naf Beach Hotel ni kuchuma dhambi kwa muumba wa vyote duniani.Tusitumie siasa chafu kuchafua hata wasiohusika na mambo yanayozushwa mitaani.Hoteli ya Naf Beach ni mali ya Shabaan maarufu kama Shebby Mix aliyoijenga kwa mkopo kutoka Crdb.

Hakuna uhusiano wowote kati ya Membe na Shabaan iwe kiundugu,kiurafiki au kibiashara na ndio maana inakuwa sio afya kuleta mijadala inayosema uongo kuhusu hoteli hii isiyokuwa na jina lenye nasaba yoyote na Membe katika umiliki wake.Nasisitiza tujadili kweli na kuikataa uongo kwasababu itatuweka huru kifikra na kimaamuzi.Nawasilisha!

getlstd-property-photo.jpg

Mimi sioni tatizo kwa Membe kumiliki hoteli,hadhi yake kama mwanasiasa na waziri wa wizara anayoongoza,maslahi kama mbunge waziri,na akipata ziada toka marafiki,akichukua na mkopo kuna shida gani? Mbona Dewj,Abood,na wengine wengi na wafanyabiashara wapo katika siasa za Tanzania kuna shida gani?

Nahisi hii inahusiana na Urais ambao umekuwa ukisemwa kuwa Mh Membe anahitaji.Lakini Membe ni mwanasiasa ambaye mpaka leo hajawahi tamka kuwa anautaka Urais,isipokuwa vyombo vya habari vinamsemea.Kwangu mimi Membe kumiliki hoteli ile au kutomiliki hakumpunguziii kitu katika mbio zake ambazo wanahabari wanamsemea,naam 2o15 Rais atatoka Bara ,atakuwa Mkristo tena Mkatoliki.huo ndo ukweli mchungu bila kujali atakuwa wa chama gani.
 
Bwana Mapesa maswali yako ni mazuri sana. Niseme tu kwamba Membe hayuko responsible kuelezea maisha ya Shebby (Shaibu Mohamed Juma) na sidhani kama sisi hapa tupo responsible. Swali lililo mbele yetu ni je Membe anamiliki hotel Mtwara? Kuchunguza Shebby ni nani kihistoria hakujibu swali la msingi.

Ajabu tumedangamywa na kuaminishwa kwamba Shebby ni masikini huwezi kujenga hotel. Hata baada ya mmiliki kuongelea kupitia TV na radio historia yake na jinsi alivyopata utajiri wake. Lakini hao wanaotuaminisha hawana hesabu ya utajiri wa Sheby ambao unaweza kuwa wa urithi au umiliki wa maeneo mengi ya ufukweni ambayo kwa miaka ya karibuni yamenufaisha wakazi wa Mtwara.

Ifahamike Shebby ni dalali makubwa wa ununuzi wa korosho kutoka vyama vya ushirika kwenda kwa makampuni ya wahindi. Kinadhalia Udalali auhitaji mtaji na malipo yake ni makubwa nayapamoja. Kama Shebby anaweza kushinda mnada moja na akamchaji muhindi shilingi 10 kwa kila kilo aliyoshinda manake anapata billion moja kwenye tani laki moja. Hapo hajafanya organization ya transport kwa kilo kutoka mnadani hadi ghalani.

Shebby alikuwa mfanyabiashara wa simu kariakoo lakini mwanzoni mwa miaka ya 2000 alirudi kwao Mtwara mara baada ya kugundua kwamba udalali wa korosho unalipa. Akauza maduka yake ya simu aliyokuwa anamiliki kariakoo. Madalali wengine walioungana naye ni pamoja na bwana Salum Mkemi ambaye bado makazi yake ni Dar.

Shebby ni mfano wa kuigwa kwa vijana wanaodhani Dar ndio kila kitu. Shebby amekuwa akiiomba serikali iwawezeshe wanunuzi wa korosho wakizalendo kuuza korosho zao moja kwa moja inchi za nje. Tatizo, alijibiwa kwamba wahindi wamezuia kununua korosho kutoka kwenye nchi zinazolima pasipo kupitia makampuni yao ya India. Kila miezi kadhaa Shebby amekuwa akifanya mahojiano na TV akielezea jinsi alivyopata utajiri wake na ujumbe wake kwa vijana. Kwa kudhani Shebby huwezi kujenga hotel ni kudharau jitihada zake.

Tujifunze kupongeza na kutia nguvu vijana waliotoka jasho na wakafanikiwa. Tusiache wanasiasa watukatishe tamaa kwa kusema hatuwezi.

Ningekuwa mimi ni Team Membe nisinge anzisha uzi wa aina hii eti kujitetea kwa issue ambayo iko wazi! Hii kitu wakiisikia watu wa Mtwara mjini kwamba Ndugu Membe anakana kumiliki hotel yake watapata mstuko mkubwa!
 
Nafurahi kuona watu mkibishaba kuhusu mmiliki wa Naf beach.Mm nimewahi kufika kwenye hizo hotel tatu,NAF BLUE,NAF BEACH NA FAN CITY kwa kazi MAALUM ambayo siwezi iweka wazi kwa sababu za kiusalama.Nillikaa hapo kwenye hotel kwa zaidi ya wik mbili kutokana na kazi husika.
Naweza kusema kwa uhakika hotel za NAf blue na Fan city ni mali ya Sheb mix.
Hotel ya NAF BEACH ndo kizingumkuti;watu wanasema mara ya Sheb na wengine mara ya Membe.Sheb na familia yake ndo wanaonekana wamiliki wa NAF BEACH kwa 100%.Lkn kuna doc ambazo niliziona (siweze kuzisema) mh.Membe na vigogo wengine wakiwa copied.
Kwa ss kuna hotel nyingine mpya mbili zinazosemekana ni za Sheb zitafunguliwa siku yoyote.Moja ipo Lindi na nyingine Mtwara.

NB:Nashindwa kuweka hii habari na "supporting documents" vizuri kwa sababu za kiusalama.
 
Back
Top Bottom