Membe jiandae kisaikolojia

1-Imetajwa dola million ishirini (20)za Gaddafi ,unatakiwa utoe maelezo ya kutosha.
Pumbavu kabisa, na vipi mwizi wa nyumba za serikali ambaye aliuza nyumba zote na zingine akawahonga malaya wake?

2-kutamalaki kwa dawa za kulevya awamu yako.

3-utakatishaji fedha uliokithiri awmu yako.
Hivi kumbe Awamu ya 4 Membe ndo alikuwa Rais? Na Magufuli alikuwa nani?
 

Mtaongea weeee ila ukweli ndio huo. Watanzania tunataka mabadiliko. Hapa ni Membe tuuu.
 
Kama mambo hujui jitahidi basi utumie japo common sense! Eti JK alikuwa anafuatana na Membe kwenye safari zote za nje! Nimezungumzia safari za nje hapa? Btw, kwani ni watu wa mataifa ya nje ndio wanaopiga kura kumchagua rais?! Kusoma hujui, hata picha ukutani huzioni?

Wewe ni miongoni mwa wale waliokariri kwamba mawaziri wa mambo ya nje huwa wanaandaliwa kuwa marais! Uchaguzi unahitaji sana kuwa na exposure ya ndani vinginevyo, itabidi ufanye kazi ya ziada kumtangaza mgombea kama ambavyo Mwalimu alivyokuwa amefanya kazi ya ziada kumtangaza Mkapa ambae exposure yake kubwa ilikuwa nje!

Kinyume chake safari nyingi za mikoani JK alikuwa anaambatana na Magu kwa kigezo cha waziri anayehusika na barabara ambazo ilikuwa wanazunguka huku na huko ama kuzindua, au kuweka jiwe la msingi kumbe alikuwa anamtangaza! Btw, kwanini arudi kuomba msaada kwa Mr. Clean wakati tayari Mkapa ni Mjumbe wa Kamati ya Maadili ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Rais?! Inaelekea hata Kamati ya Maadili yenyewe huijui ndo maana unadai alirudi kwa Mkapa!

Halafu acha kuongea mambo usiyoyajua wewe! JK hakurudi kwa Mkapa kuomba msaada bali Mkapa na wastaafu wengine wa nafasi za juu ni wajumbe wa Kamati ya Maadili na Usalama! Ni hii kamati ndio inapokea maoni ya rais kama yalivyowasilishwa kwake kutoka intelligence community!! Mkapa ambae hakuwa rais hawezi kuwa na official info kuhusu wagombea kwa sababu hizo info anapewa rais!! Ni huyu Rais ambae ndie pia Mwenyekiti wa National Security Council ambayo wajumbe wake ni top military chiefs, TISS pamoja na some top government officials! Kote huko Mkapa hakuwepo!! Rais hawezi kuomba msaada kwa rais mstaafu kwa sababu kazi kubwa ya vetting inakuwa imeshafanywa na wenye nchi yao huku rais akiwa ndie mwamuzi wa mwisho kulingana na mapendekezo aliyopewa! Anachoweza kufanya kwa huyo rais mstaafu ni kuomba tu ushauri na sio msaada; ushauri ambao anaweza kuupiga chini!!
 

[emoji120][emoji120][emoji120]
 
PAMOJA NA HIZO NGUVU MWAMBIE KUWA 2020 ANARUDI CHATTLE HAKUNA NAMNA YA KUMSAIDIA YEYE AENDELEE NA MAMBO YA KE KADRI AWEZAVYO ILA AJUE TU KUWA MBIO ZAKE MWISHO NI 2020

Amen [emoji120]
 
Wewe hakuna unachpkijua, unajua Philip Mangula alichofanya na team Jk baada ya Uchaguzi wa mwaka 2005, unadhani ingekuwa rahisi kwa Mangula kukubali kufanya kazi tena na JK. Ukweli Kikwete baada ya Maji kuzidi unga ilibidi awaangukie wahafidhina( Mkapa, Mangula & the Co) ambao kwao Membe na Lowassa hawakuwa machaguo!
Narudia Kama Membe alishindwa kuwa Rais akiwa waziri wa Mambo ya nje he will never become ever! Unless otherwise Kama hujui what does it means to be a Foreign Affairs Minister hasa kwenye mikakati ya kuwa next president!
 
Angalia unavyochanganya madesa huku ukijitia ujuaji kumbe hujui lolote! Kikwete alimwangukia Phillip Mangula kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM, na hiyo ilikuwa back 2012! Narudia, Mkapa ni Mjumbe wa Kamati ya Maadili, kwahiyo huwezi kumwangukia mtu ambae tayari yupo kwenye kamati! Btw, kwahiyo unaamini after Magu, rais ajae ni Palamagamba Kabudi?! We jamaa una uelewa mdogo sana wa siasa za Tanzania na wala hufahamu ni kwanini nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje inahusishwa sana na urais!

FYI, pamoja na kujitia kujua kwako wakati hujui lolote; inaonekena ukiwa Waziri wa Mambo ya Nje unaepushwa na scandal za ndani ambazo ni rahisi sana kwa senior ministers wa ndani kuzipata! Na ndio maana mawaziri kama wa fedha, mambo ya ndani, nishati n.k mara kwa mara huwa wanabadilishwa! Lakini kwavile Waziri wa Mambo ya Nje ha-deal sana na internal issues, basi hiyo inamfanya kuwa salama zaidi!

Lakini pili, ni kukariri tu kwa watu aina yako ambao critical thinking yao ni ndogo! Baada ya kuona Mkapa aliyekuwa foreign minister na akafuatiwa na JK ambae alikuwa foreign minister wote wakawa marais, basi watu aina yako wakahusisha moja kwa moja nafasi hiyo na urais!! Kitu ambacho mnashindwa kujua ni kwamba, Mkapa tangia hapo alikuwa mwana pendwa wa Mwalimu! JK nae wakati yupo foreign affair na waziri wa fedha wakati wa Mwinyi, alifanya kazi mzuri sana ambayo ikawa imeshamjengea nguvu kubwa sana ndani ya nchi! Na ndio maana haikushangaza kuibuka na 80% kwa sababu kila mtu believed on him si kwa sababu alikuwa foreign minister bali ni kwavile alishajenga foundation ya kutosha including ile ambayo ilimtoa kamasi Mwalimu mwaka 1995 hadi akalazimika kumbeba wazi wazi Mkapa kwa sababu tayari JK alishakuwa na foundation ya kutosha na wakati huo wala hakuwa waziri wa nje!!

Najua mashabiki wa Magufuli inawauma sana mkisikia Mungu mtu wenu kabebwa tu na JK kuwa pale na ndio maana pamoja na madudu yote ya utawala wa JK, Magu hana ubavu wa kumgusa zaidi ya kutoa ubunge kwa mke wake ili kulipa fadhila! Na wale mashabiki wa EL bado wana hasira za bosi wao kukatwa na hawaamini kwamba JK angeweza kuwa gaidi namna hiyo kwa EL!
 
Tatizo hujui siasa inavyofanya kazi,subiri utajua kwanini anatajwa yeye badala ya kikwete
Pumbavu kabisa, na vipi mwizi wa nyumba za serikali ambaye aliuza nyumba zote na zingine akawahonga malaya wake?


Hivi kumbe Awamu ya 4 Membe ndo alikuwa Rais? Na Magufuli alikuwa nani?
 
Report ya CAG mliijibu kwa hoja gani?
 
Membe asiyajue ya system wewe official punda uyajue Acha basi Kula muwa Kwa kutumia tundu la haja
 
Hakuna mtanzania anayemhitaji Jiwe. Msijidanganye. Ni hero tuongozwe na Member au hata Joti kuliko huyu mbinafsi na katili asiye na huruma. 2020 Jiwe must go.
Sema wewe ndiyo umtaki jiwe
Sisi wenye kujitambua tunasema ikiwezekana aongezawe Miaka mingine 10! Baada ya 2025
 
Hakuna mtanzania anayemhitaji Jiwe. Msijidanganye. Ni hero tuongozwe na Member au hata Joti kuliko huyu mbinafsi na katili asiye na huruma. 2020 Jiwe must go.
Yani mkuu kuna typos kibao lakini watu wameelewa ujumbe na kuonyesha kuwa wameupenda sana! Kweli watu wamechoshwa, huu uchaguzi ccm wasiibe aisee.
 
Mbona magufuli alipiga pesa za kivuko, billion 251 wizara ya ujenzi, kauza nyumba za serikali akajiuzia nyumba nyingi kinyume cha Sheria, barabara ya ubungo fire ilijengwa chini ya kiwango ikiwemo standa ya mwendo kasi na sasa kapiga mchongo kibao yeye magufuli humuoni umekalia kumkomoa membe peke yake
 
Sauli alimwinda sana Daudi ili kulinda madaraka yake ila ni Daudi aliyekuja kutawala mahali pa Sauli tena bila kutumia nguvu kubwa dhidi ya Sauli aliyekuwa mtawala wakati huo

Mtu kuwa mtawala haimaanishi unaweza kufanya kila kitu unachojisikia kufanya kuna mengine yanapokuja ukiwa mkaidi yanakuangusha tu

Mimi nimesema kibiblia zaidi
 
 
Nikiweka kumbukumbu vizuri wakati huo Raisi alikua mzee JK waziri mkuu mzee Pinda na mheshimiwa wa sasa alikua sehemu ya baraza. Nani amfunge paka kengele?
 
Membe hta akigombea pekeake hawez kushinda kivuli chake, CcM kama wanataka kosea wamchangue membe kuwania uraisi, ndo watakuwa wamekizika chama chao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…